Mh Rais,
Kitu kikubwa sana ulichoshinda pamoja na changamoto zilizojitokeza ni kuruhusu mjadala juu ya mkataba wa DP World. Huu ni uhuru wa kikatiba lakini tunajua upo udhaifu wa kikatiba ambao ukiamua kuutumia kikamilifu tusingepata uhuru wa kiwango hiki.
Kwahili lazima tukusifu kukubali mawe yanayorushwa kila kona kwako ingawa baadhi ya wasaidizi wako ni kama wamefikia ukomo wa uvumilivu na badala kukazana na hoja sasa wameamua kutumia njia zisizo salama.
Lakini mkuu wetu kwanini vitisho kwa wanaohoji juu ya mkataba wa Dp world?
Kwanini kukamatwa kwa akina Mdude Nyangali?
Kuacha mjadala kushika hatamu na kuamua hatma ya taifa ni kitu cha pekee umefanya na usiruhusu machawa kuvuruga jambo hili jema sana kwako.
Hii ni sauti ya kiungwana kutoka Kaisho, Kyerwa! Asante sana Mh Rais!