PostGE2025 Rais Samia: Sisi wazazi wenu tungefanya mliyofanya nchi hii isingekuwa na neema kama sasa

PostGE2025 Rais Samia: Sisi wazazi wenu tungefanya mliyofanya nchi hii isingekuwa na neema kama sasa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ina maana hamjui anayebomoa?? Hamjui aliyetufikisha hapa??
 
Mwambie
Akifungua Bunge la 13 Jijiji Dodoma, leo Novemba 14, 2025, Rais Samia Suluhu Hassan amesema "Niwasii sana wanangu vijana wa Tanzania, nchi hii ni yenu, msikubali hata siku moja kuchoma nchi yenu, msikubali kukata tawi la mti ambalo mmeukalia. Nawasii kamwe msijekuwa wabomoaji wa taifa lenu."
Mama Wazazi wetu hawakuwa na sababu ya kufanya hivyo hapakuwa na mtu aliyekuwa anateka watu, mafisadi na wezi wa mali za umma walipata hadhabu kali enzi za wazazi wetu viongozi walikuwa ni watu wa mfano wa kuigwa k5k jamii..
Walivyo ishi familia ya nyerere ndio watanzania wengi waliishi hivyo hadi leo.
 
Rais Samia kasema kama wao wazazi wangefanya waliyofanya vijana (maandamano) basi nchi hii isingekuwa na neema.

Amewaambia vijana wasikate kuti walilokalia!

Kanali Samson Mande '- hatukubweteka kama vijana wa sasa wa 2025, sisi tukiwa vijana wadogo tulipigania kuikomboa nchi kutoka utawala usio halali


Vijana walipofanya mapambano baada ya kukataa uchaguzi feki walifanikiwa kuungoa utawala usio halali, asimulia harakati zao ...

November 2025

Kanali Samson Mande arudi Nyumbani Kutoka Uhamishoni Sweden, baada ya kupakaziwa kashfa Dar es Salaam

Part 2 : Kanali Samson Mande Kutoka kuwa kijana mwenye mwamko wa mabadiliko akiwa sekondari hadi kupigana vita, kuwa recruited kama afisa usalama na kisha kuingia msituni... kuangusha serikali isiyo halali


View: https://m.youtube.com/watch?v=AUNz6o1GWaU

November 2025

Kanali Samson Mande arudi Nyumbani Kutoka Uhamishoni Sweden, baada ya kupakaziwa kashfa Dar es Salaam
1763129849761.jpeg

Picha : Kanali Samson Mande

Rais Yoweri Kaguta Museveni amsifia kanali Samson Mande kwa mchango katika harakati za ukombozi wa Uganda, akibainisha utumishi wake kama skauti kijana mbichi kabisa wa kujitolea wa Kikosi Kazi cha TPDF / JWTZ chini ya Meja Jenerali Silas Mayunga mwaka 1979, na baadaye kama kamanda wa Kikosi cha 15 wakati wa Kuzingirwa kwa mji wa Masaka mwaka 1985.

"Nakumbuka Samson Mande mwaka 1979 akifanya kazi kama skauti wa kujitolea katika Kitengo cha Kikosi Kazi cha TPDF / JWTZ chini ya Meja Jenerali Silas Mayunga huko Mbarara
 
Akifungua Bunge la 13 Jijiji Dodoma, leo Novemba 14, 2025, Rais Samia Suluhu Hassan amesema "Niwasii sana wanangu vijana wa Tanzania, nchi hii ni yenu, msikubali hata siku moja kuchoma nchi yenu, msikubali kukata tawi la mti ambalo mmeukalia. Nawasii kamwe msijekuwa wabomoaji wa taifa lenu."
It's very important to read and understand what's in the holy scriptures otherwise it become hard to differentiate GOD and SATAN.
 
Ila Samia anazidi kuongezea watu hasira tu, kwahiyo wazazi wao walitoa polisi nje kuua watgoto wao?

Ndio anahalalisha yaliyotokea kwa kusema mkubwa hakosei?

Rais Samia kasema kama wao wazazi wangefanya waliyofanya vijana (maandamano) basi nchi hii isingekuwa na neema.

Amewaambia vijana wasikate kuti walilokalia!
Nimefurahi kuona upo hai maana ulikuwa katikati ya mapambano.. Msifadhaike, mi Captain Tesha nipo salama naendelea kufanya maandalizi.
 
TOKA MAKTABA :

TULIKINUKISHA BILA WOGA

27 May 2022
Luteni Mwamba Luchembe

View: https://m.youtube.com/watch?v=yY6JDPWaHuY
Former Zambian army officer Mwamba Luchembe reflects on the day he tried to overthrow Kenneth Kaunda in a military coup. (This interview was recorded while PF were in power and Kenneth Kaunda was still alive.)
Tulikuwa katika kambi yetu kilometa 500 kutoka mji mkuu wa taifa la Zambia, jiji la Lusaka.

1990 hali ya kisiasa na kiuchumi ilikuwa mbaya, wananchi walikuwa na manunguniko mengi ikiwemo ugumu wa maisha, ughali wa bidhaa muhimu kama unga wa sembe, ukandamizaji wa kisiasa uliokuwa unafanywa na chama dola kongwe kimoja UNIP

Maandamano yakatokea jeshi la Polisi likatumwa kudhibiti mandamano hayo lakini wakazidiwa na nguvu ya umma uliojitokeza .

Rais Kaunda akatoa amri jeshi la ulinzi la Zambia watoke kambini kuongeza nguvu kudhibiti maandamano.

Hivyo mimi nilikuwa katika Battalion 5 Kaoma, nasi tukapewa amri tuende Lusaka kuongeza nguvu kudhibiti maandamano.

Wakati tukiwa mesi tunakula chakula cha jeshi ambacho hatulipii, mawazo yetu yakaguswa na madhila ya wananchi wasiokuwa na uwezo wa kula ambao walijitokeza kwa wingi kuandamana huku sisi tukila chakula kwa uhakika kupitia kodi zao.

Hivyo tukaona nchi inaenda kubaya kutokana na kuwa na chama kimoja kongwe tawala kilichoishiwa mawazo ya kutanzua changamoto za raia.

Wazo letu likawa kuchukua nchi na kuiongoza kwa miezi sita huku tukijenga mazingira vyama angalau vitatu makini viundwe ili demokrasia iwepo nchini. Hatukutaka kuona vyama zaidi ya vitatu maana tunajua vyama vingine ni vya mfukoni ( briefcase) siyo vyama vya ukweli vya mawazo mbadala

Tukiamini demokrasia ya uwazi, uchaguzi huru, bunge makini vingeweza kuiondoa nchi ktk changamoto iliyokuwa nchi inapitia ...

Ndiyo maana niliongoza platoon iliyokuwa na wanajeshi 32 huku mimi ni kiwa ofisa wao hivyo jumla ya wanajeshi 33 tulivamia kituo cha taifa cha ZBC nami nikatoa tangazo la serikali kupinduliwa...

Tulikuwa tumekubaliana na kambi zingine za Kitwe, Mufulira n.k nao waingie ktk sehemu nyeti za utawala wa kiserikali ktk majimbo ili kukamilisha mapinduzi hayo...

Wananchi walijitokeza kwa wingi mtaani kufurahia tangazo la mapinduzi ya kijeshi. Hata hivyo wenzetu tuliokubaliana kuikamilisha kazi hivyo kote nchini walitugeuka.

Akatumwa askari mmoja mwandamizi atushawishi kuwa mapinduzi yetu hayakufanikiwa.

Nilikamatwa na kupelekwa kituo kikuu cha Central police nikafungiwa katika mahabusu upande wa wanawake, na wale mahabusu wote wanawake kwanza walihamishwa.

Wakaja wanajeshi wa idara ya utambuzi, maofisa wa usalama wa taifa na wa vyombo vingine kunihoji kwa muda wa wiki moja ktk selo hiyo ya wanawake.

Baada ya hapo walinipakiza ktk helicopter tukaelekea katika kambi nilitotokea iliyopo kilometa 500 kutoka Lusaka. Wakafanya upekuzi katika ofisi nikiyokuwa natumia kambini na katika nyumba niliyokuwa naishi kambini.

Wakanirejesha Lusaka hata hivyo usiku ulikuwa umeanza kuingia hivyo rubani wa helicopter akazima mawasiliano yote na kutua eneo mojawapo kwani rubani alitoa taarifa ya kuwa helicopter haina uwezo wa kusafiri usiku wa giza kufika Lusaka. Walizima mawasiliano ili kama kuna njama za wenzangu kuja kuniokoa zisifanikiwe.

Alfajiri na mapema tukamalizia safari yetu kwa usafiri wa barabara hii yote ikiwa ni njia ya medani, kwa waliopanga nami kufanya mapinduzi wasijue nilipo wala nini kimetokea kwangu mimi.

Mahojiano yakaendelea mjini Lusaka ktk nyumba maalum (safe house) kujaribu kupata habari zote za Mapinduzi na wahusika wote katika njama hii ya kupindua nchi.

Walitumia koleo / pliers kutoa meno yangu kavukavu bila ganzi, lakini situwasaliti wala kutaja wenzangu waliotayarisha jaribio la kuangusha serikali.

Baada ya kunisulubu hivyo, wakanirudisha kwa kificho kituo kikuu cha Polisi huku nikiwa na maumivu makali. Wakanipandisha ghorofani, watu wa Idara ya Usalama na wale wa Idara ya Utambuzi jeshini wakapanga mipango watawaambia nini raia hata polisi na wanajeshi watakaoniona.

Hivyo basi wakanivua nguo zote tukiwa ghorofani na kuzitupa kupitia dirishani. Kutoka juu ghorofani wakanitelemsha mzobemzobe mbiombio uchi wa mnyama nikiwa mtupu, kisha wale wote walikuwapo kituo kikuu cha Polisi wakanishangaa si polisi, raia na waandishi wa habari hata wapita njia wakabaki wanajiuliza kulikoni..

Watu wa Idara na Vyombo wakasema huyu ni kichaa aliyewehuka siku nyingi kabla ya mapinduzi, faili lipo jeshini na kwa vile alikunya sana Pombe na bangi ndiyo maana akatimka kwenda, kutangaza mapinduzi yale.


Baada ya miezi miwili nikastaafishwa jeshi kwa sababu za 'kiafya' yaani ugonjwa wa akili. Hata hivyo vyombo vya usalama vikamwambia rais pamoja na hii hadaa tuliyoitengeneza ukweli watu wanataka na wanaamini mabadiliko ya kuleta vyama vingi vya kisiasa. Hivyo ni bora rais aanzishe mchakato wa mabadiliko ya katiiba kuruhusu na kuafiki kwa moyo mkunjufu vyama vingi, demokrasia na uchaguzi huru kupitia tume huru ya uchaguzi.

Hivyo mwaka 1991 mchakato wa vyama vingi na katiba mpya vikapitishwa na bunge la Zambia kwa usimamizi wa karibu wa rais Kenneth Kaunda.

Mapinduzi yale yaliyoshindwa hata hivyo yalileta jambo chanya kuwa watu wanataka mfumo wa vyama vingi, yalionesha kuwa ukiritimba wa chama dola kongwe cha UNIP na rais nguvu yao ya ushawishi wa chama kimoja umepungua na wajitayarishe kuwa chama cha upinzani.

Kwa ujasiri wa Luteni Mwamba Luchembe kuongoza jaribio la mapinduzi , sasa anahesabika kama baba wa mabadiliko / reforms za kupatikana katiba mpya na demokrasia ya vyama vingi nchini Zambia.

Katika mitaala vya masomo ya uraia / civic Luteni Mwamba Luchembe anatokea ktk vitabu mashuleni kuwa alikuwa chachu ya mabadiliko yaliyoleta vyama vingi kuruhusiwa nchini Zambia.

Mbali ya watoto wa shule kusomeshwa mchango wake Luteni Mwamba Luchembe kuleta mabadiliko, sasa katika Makumbusho ya Taifa mjini Lusaka na makumbusho ya majimbo mbalimbali nchini Zambia picha yake ipo miongoni mwa watu waliotoa mchango kwa taifa la Zambia hadi kufikia lililopo sasa.

Rais Frederick Chiluba aliposhinda uchaguzi wa vyama vingi kupitia chama cha upinzani alimrejesha Luteni Mwamba Luchembe kazini na kumpa cheo mserereko hadi kuwa Captain kisha kumstaafisha kwa kumpatia pensheni stahiki ya cheo alichofikia.

Source :
 
Vuguvugu halipoi

 
Ila Samia anazidi kuongezea watu hasira tu, kwahiyo wazazi wao walitoa polisi nje kuua watoto wao?

Ndio anahalalisha yaliyotokea kwa kusema mkubwa hakosei?

Rais Samia kasema kama wao wazazi wangefanya waliyofanya vijana (maandamano) basi nchi hii isingekuwa na neema.

Amewaambia vijana wasikate tawi walilokalia!
Yaani kama bado haelewi kuwa Amani ina anza kwa kutoa haki, basi ni kwamba hataki maridhiano, Bali anataka maridhiano ya mdomoni na sio ya vitendo.
Huo mkono alitoa, Naye alipewa kwa kuambiwa aendele kutawala ili kufanyike mabadiliko yakayo akisi uchaguzi wa haki.

Hiyo misingi ya kumtumia Mwl Nyerere ni kutafuta Mahali pa kujificha. Na hizo nchi za nje sio kwamba wanataka kuingilia mambo yetu, Bali ukatili umezidi na yeye ana Mahakama, Polisi, Jeshi na fedha
 
Back
Top Bottom