Rais Samia Suluhu aitaka Wizara ya Habari kuvifungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa. Avitaka kufuata Sheria na Kanuni

Rais Samia Suluhu aitaka Wizara ya Habari kuvifungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa. Avitaka kufuata Sheria na Kanuni

Hoja yangu Kama Sheria hazitabadilishwa zilizotungwa kipindi Cha magu,vyombo vya habari vitakuwa huru kwa huduma ya mama na not according to the law,Sheria kandamizi ziondolewe Kama kweli mama anamaanisha
 
Ni dalili za mwanzo mzuri wa uongozi wa serikali ya awamu ya sita. Muhimu kazungumzia uwazi wa kanuni ambazo zilikuwa zinatumika kuhukumu watu na vyombo vyao vya habari. Kanuni ziwe waz,i ubabe unaumiza wananchi na kuifedhehesha serikali.
 
Rais Samia Suluhu ameiagiza Wizara ya Habari kuvifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa, na kuhakikisha vinafuata sheria. Aidha, ameagiza sheria kanuni na adhabu ziwe wazi, ifahamike kosa fulani adhabu yake ni fulani, ili isionekane kuwa serikali inaminya uhuru wa habari.

Rais Samia amesema haya...

Wizara ya habari, mnapaswa kusimamia vyombo vya habari, nasikia kuna vyombo vya habari mmevifungia, vifungulieni lakini vifuate sheria na kanuni. Tusiwape mdomo mdomo wa kusema tunabinya uhuru wa habari na nataka kanuni ziwe wazi. Tusifungie tu kibabe

Huyu rais utafikiri siyo mTz, tena ccm.. maana anaona mbali mnoo.

Mh. Bi mkubwa, Big up!
 
Back
Top Bottom