Rais Samia Suluhu aitaka Wizara ya Habari kuvifungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa. Avitaka kufuata Sheria na Kanuni

Rais Samia Suluhu aitaka Wizara ya Habari kuvifungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa. Avitaka kufuata Sheria na Kanuni

Hivi unajua maana ya upinzani?
upinzani unazikwa rasmi.
Huoni rais anayetoka chama cha sisiemu anasema na kuagiza wateule wake wakahakikishe wanatekeleza ilani ya sisiemu alafu bavicha wanashangilia kuwa sisiemu kwisha habari yake, unaona kuna upinzani hapo? Itafika wakati mtaamini sasa kuwa hamkua mnaibiwa kura...
 
Rise & Fall of the Republic of Twitter!

Kuleta uhuru wa habari, habari zote tutazipata bila kificho.

Maafisa vipenyo wanaenda kuwa jobless.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Good start! Sikumuelewa pale aliposema hii ni "awamu ya sita"

Kumbe anataka kujitofautisha kabisa na mtangulizi wake. Mabadiliko aliyofanya so far, yanatosha kuelezea maono na msimamo wake. Ni msikivu na kwa hilo atafanikiwa pakubwa.
 
Mbona hajazungumza kuhusu ufutwaji wa sheria kandamizi?

Maana bado zinampa waziri mandate ya kuvifungia vyombo vya habari kama ilivyokua utawala wa jiwe waziri anajipendekeza na kufungia bila sababu au kuleta utetezi upande wa pili.
 
Mataga mtapata tabu sana. Magufuli aliwadekeza sana. Ni wakati kwenu kumkubali Rais wenu mpya. Mkikosa utii kwake, mtaishi maisha magumu sana kuanzia sasa.

Wajulishe na wenzako akina Jane Lowassa , Elitwege, Kawe Alumni , nk ya kwamba mambo yamebadilika sasa. Jeuri na majivuno yenu yote, kwisha!!
Pale juu panahitaji mtu mwenye msimamo,anachofanya yeye ni kama kutaka kuwafurahisa watu fulani,anajizungusha zungusha tu hakuna cha maana anachofanya.ngoja amalizie hii miaka mtakuja kuona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAWIO Oyeeeee,😆😆😆😆😆🖖🖖
MWANAHALISI Oyeeeee😄😄😄😄🖖🖖
TANZANIA DAIMA Oyeeeee😆😆😆😆😆🖖🖖🖖
Q
WASAFI Oyeeeee😆😆😄😄🖖🖖🖖

ABUNUASI Ziiiiiiiiiiiiiiiiii😭😭😭😭😭😭😭😗😗😗😗

Asanteni kwa kunisikiliza.
hadi nimekumbuka magazeti yangu pendwa Rai nguvu ya hoja na Tanzania daima
MWANAHALISI ya Ndimala Tegambwage? Oyeeeee 😆😆
MAWIO Oyeeeee 😆😆😆😆
Tanzania daima , Oyeeeee😄😄😄😄
 
Niliwahi andika huko nyuma kuwa Mama Samia is a breath of Fresh Air, tena marashi mazuri ya visiwani.

Leo amethibitishia dunia kuwa yuko tofauti na misimamo tuliyoiona kwa miaka miatano iliyopita.

Mama Samia amesisitiza uhuru wa kujiekeza pamoja na uhuru wa vyombo vya habari.

Amonyeshwa kukerwa na ule ubabe wa kuvufungia vyombo vya habari, tabia iliyokithiri kutoka TCRA na Idara ya Habari.

Viongozi wote wawili wa zidara hizo wamepigwa chini, Eng Kilaba wa TCRA, na Abbas wa Wizara ya Habari na aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali.

Na Mama Samia ameelekeza kuwa vyombo vyote vilivyofungiwa vifunguliwe mara moja.

Huu msimamo wa Mama ni dalili ya kiongozi anayetumwa na dhamira safi na isiyo na hila ndani yake.

Vile vile ni msimamo wa Kiongozi anayejiamini.

Kwa msimamo huu, nampongeza sana Mama Samia.
 
Wapi ww, mahali pa kikosewa wanapewa ukweli wao. Naona kimekuuma utawala wa dhalimu rasmi unafutwa nchini. Mungu nakushukuru kwa kuamua kufanya mabadiliko bila damu kumwagika. Ndani ya miaka mitano iliyopita nchi hii ilikuwa mikononi mwa shetani, sasa Mungu ameamua wananchi waishi kwa amani, kwani shetani hana mamlaka hapa duniani.
Najua ni jambo ambalo halitakua na muda wale wakora mtafungiwa tena.
Kama amesema mfuate sheria na ninyi kufuata sheria huwa hamtaki sasa unategemea nini kitafuata?

Angesema mpewe uhuru kwa chochote bila kufuata sheria mko huru ningewaza kidogo.
 
Aisee utawala wa dikteta Magufuli unashambuliwa kila kona.
 
Back
Top Bottom