Rais Samia Suluhu aitaka Wizara ya Habari kuvifungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa. Avitaka kufuata Sheria na Kanuni

Rais Samia Suluhu aitaka Wizara ya Habari kuvifungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa. Avitaka kufuata Sheria na Kanuni

Angekuwa anaamini katika uhuru wa habari asngesema malalamiko ya waandishi ni "mdomo mdomo kwamba tunabinya."

Samia Hassan is a lightweight, kila anachoongea huwa kinaelea tu hewani, hakina sense. Amesema walofungiwa waachiwe lakini wafuate sheria. Nani alifungiwa bila kufuata sheria? Au sheria ndio zilikuwa mbovu, aseme!

Kama walionewa kwa nini unawaambia wafuate sheria?

Makosa na adhabu yaeleweke. Kwani jbo gani halieleweki kama ni kosa ama sio kosa, kwa mfano?

Haeleweki huyu Mama.
Hakuna haja ya hofu kiongozi, kauli ya rais ni agizo pana..zile sheria kandamizi zote zinakwenda kuondolewa.. Na ndo maana kasema atakutana na kila sekta /taasisi ili kuweka kila kitu sawa. Mungu ambariki huyu Mama
 
Mara paap Maxence Melo naye kafungulia Majukwaa yake na kusisitiza Sheria zifuatwe adhabu zitafuta tukizinguana.
Huyu jamaa yetu aliteseka sana kwa ajili ya kucover majina yetu, alikuwa na kesi nyingi kuliko za Tundu Lissu akitetea uhuru wa Habari
Mkuu ukwaju lile jukwaa letu pendwa la kule chinii kabisa lipo?
 
Dah yaan saiv mfumo mzima umebadilika wa kiserikali kutoka ONE MAN SHOW mpaka serikali kujiendesha kimfumo..
 
Ngoja tuone mwanzo huu utakavyoendelea
Tutaelewana tu. Sasa makufuli yote yaliyofungwa TUPILIE KULE. Shetani aliyeombwa kuja kufunga media Tupilia Kule. Vyombo vya habari jitanuenina zingatieni sheria tu.

Kumbe huyu ni Mama RUKSA! Sasa ni Mama mi 5 tena.
 
Enheee Picha la kutisha limeanza. Wapi Tanzania Daima, Kwanza TV
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Aendelee Mpaka Bhasii

Kwenye Mchezo Wa Karata Wanasema Umelamba Mali
Tuombe Mungu Tusije Kulamba Garasa Ama Nnyaa
 
Nimemuona yule kifutu aliyekua msemaji na mfungiaji mkuu wa media kafyumu anataka kupasuka hajazoea mambo ya diplomasia yaani kavimba anataka kupasuka alizoea funga ua bambikia waite wajieleze nyambaf , sasa leo mama kasema wafungue vyombo kukosoa sio adhabu yake ndio iwe kufungia , tatizo la kuokota makanjanja mtaani na kuwapa vyeo ndio madhara yake haya, Mama kasema wafunguliwe umbwa nyie , Abasi alitakia awe the Hague kama sio kaburini na meko wake
 
Kitaa wanasema: mama anafanya aliyepita aonekane mjinga tuu
 
Kuna msemo wa Kizamani unaosema hivi , nanukuu , " MATATIZO HAYAWEZI KUTATULIWA KWA KUTUMIA AKILI ZILE ZILE ZA WATU WALEWALE WALIOYATENGENEZA" mwisho wa kunukuu .

Natambua dalili ya nia njema ya Rais mpya wa Tanzania ya kubadilisha uozo mwingi wa awamu iliyopita , na naunga mkono , lakini ni wazi kabisa kwamba ndani ya serikali bado wale viongozi waliosababisha vyombo vya habari kufungiwa wangali madarakani , hatuwezi kutatua jambo hili ikiwa watu hawa wataendelea kukalia ofisi zile zile walizozitumia kukandamiza vyombo vya habari .

Hassan Abbass ni kinara wa ubabe wa kufungia magazeti na vyombo vingine vya habari , huku akitumia lugha ya kejeli , majigambo na dharau kubwa as if hii nchi ilikuwa kaiumba yeye , tukiamua kweli kwa dhati kuanza ukurasa mpya basi huyu mtu aondolewe wizara ya habari haraka sana , hana cha kujitetea kutokana na unyama ule , hana ! ikiwa kama bado serikali hii inamhitaji basi ni bora akahamishiwa wizara nyingine , chuki aliyoijenga huyu mtu haiwezi kusameheka .

Naomba kuwasilisha .

Kweli kabisa, Nashauri apelekwe wizara ya kilimo akafungie kabichi. Kwenye habari hapamuhusu kabisa.
 
Rais Samia Suluhu ameiagiza Wizara ya Habari kuvifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa, na kuhakikisha vinafuata sheria. Aidha, ameagiza sheria kanuni na adhabu ziwe wazi, ifahamike kosa fulani adhabu yake ni fulani, ili isionekane kuwa serikali inaminya uhuru wa habari.

Rais Samia amesema haya...

Wizara ya habari, mnapaswa kusimamia vyombo vya habari, nasikia kuna vyombo vya habari mmevifungia, vifungulieni lakini vifuate sheria na kanuni. Tusiwape mdomo mdomo wa kusema tunabinya uhuru wa habari na nataka kanuni ziwe wazi. Tusifungie tu kibabe

Acha tu! Mi pumzi zilikuwa zinaniishia kipindi kile. Key board tulikuwa tunaziogopa. Jamani Tanzania imebarikiwa, yaani mabadiliko yanapangwa na Mwenyeezi Mungu bila kumwaga damu. Nchi hii ni baraka tupu na neema kibao.

Sasa ni wakati wa waliokimbia nchi kurudi nyumbani. Kweli ule mwimbo wa taifa uko sawa, hauna makosa.... Mungu ibariki......
 
Mama ananikosha sana!

Nasubiri kumsikia meimosi anatueleza nini.
toka aingie madarakani hata hewa imekuwa rahisi kuvuta hapa nchini, zamani hewa ilikuwa nzito sana😂 (natania)
ila nchi iliharibika kila kona mapambio ambayo hadi yule kiranja aliyekuwepo kuna muda aliyachoka na kuyakana hadharani, vijana wa lumumba walikana akili zao
 
Back
Top Bottom