Kuna msemo wa Kizamani unaosema hivi , nanukuu , " MATATIZO HAYAWEZI KUTATULIWA KWA KUTUMIA AKILI ZILE ZILE ZA WATU WALEWALE WALIOYATENGENEZA" mwisho wa kunukuu .
Natambua dalili ya nia njema ya Rais mpya wa Tanzania ya kubadilisha uozo mwingi wa awamu iliyopita , na naunga mkono , lakini ni wazi kabisa kwamba ndani ya serikali bado wale viongozi waliosababisha vyombo vya habari kufungiwa wangali madarakani , hatuwezi kutatua jambo hili ikiwa watu hawa wataendelea kukalia ofisi zile zile walizozitumia kukandamiza vyombo vya habari .
Hassan Abbass ni kinara wa ubabe wa kufungia magazeti na vyombo vingine vya habari , huku akitumia lugha ya kejeli , majigambo na dharau kubwa as if hii nchi ilikuwa kaiumba yeye , tukiamua kweli kwa dhati kuanza ukurasa mpya basi huyu mtu aondolewe wizara ya habari haraka sana , hana cha kujitetea kutokana na unyama ule , hana ! ikiwa kama bado serikali hii inamhitaji basi ni bora akahamishiwa wizara nyingine , chuki aliyoijenga huyu mtu haiwezi kusameheka .
Naomba kuwasilisha .