Rais Samia Suluhu aitaka Wizara ya Habari kuvifungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa. Avitaka kufuata Sheria na Kanuni

Rais Samia Suluhu aitaka Wizara ya Habari kuvifungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa. Avitaka kufuata Sheria na Kanuni

MAMA SAMIA FANYA YAFUTAYO KWENYE HIYO WIZARA YA HABARI :

1. Tunataka tuzo za Muziki zirudi. Wizara ya habari ifanye partnership na kampuni kama Coca-Cola, coral paints au hata Spotify waturudishie tuzo.

2. Abbas afukuzwe awekwe mtu mwenye akili. He was a perennial threat to freedom of press.

3. Wizara ipige marufuku wakina YINGA MEDIA na kina DJ mwanga wanaouza kazi za wasanii kiholela. Faini ziwe kubwa sana.

4. Media service act 2016 itolewe au irudiwe upya kwa sababu inampa nguvu kubwa waziri wa habari.

5. Kuanzisha YouTube channel iwe bure na yale makodi ya kila mwaka yafutwe kama wanataka kodi wakawabane kina Barrick sio vijana wa kitanzania.

6.BASATA ifutwe na iwe ya kisasa kama Recording academy au RIAA ya marekani. Fukuza wale WAZEE wasiojua chochote. Waweke hata COUNTRY BOY / WAKAZI / VANESSA MDEE kama viongozi wa hilo bara za sio hao wazee.

7 Local channels zirudi na ziwe ZINALIPWA royalties na makampuni km STARTIMES na DSTV hii itasaidia media kuacha kutegemea matangazo pekee kama source of income.

8. Wizara ya michezo na utamaduni iandae show zenye kiwango cha lami na zenye hadhi kama Coachella, Summer Jam au OVO Festival za marekani ili kukuza wasanii wetu.

9. Samia asain EXECUTIVE ORDER kukataza manyimbo ya nje kutokea Nigeria sijui US kupigwa mchana. Mchana ni nyimbo za bongo tu.

10. Watangazaji wa redio inabidi at least wawe na diploma huku TV wawe na degree ndo wafanye kazi.

Ukifanya hivyo tutakuwa marafiki sana
 
Angekuwa anaamini katika uhuru wa habari asngesema malalamiko ya waandishi ni "mdomo mdomo kwamba tunabinya."

Samia Hassan is a lightweight, kila anachoongea huwa kinaelea tu hewani, hakina sense. Amesema walofungiwa waachiwe lakini wafuate sheria. Nani alifungiwa bila kufuata sheria? Au sheria ndio zilikuwa mbovu, aseme!

Kama walionewa kwa nini unawaambia wafuate sheria?

Makosa na adhabu yaeleweke. Kwani jbo gani halieleweki kama ni kosa ama sio kosa, kwa mfano?

Haeleweki huyu Mama.
What she means in a nutshell ni TUANZE UPYAAA. Anajaribu kuponya majeraha

Waliofungiwa au kutozwa kodi kubwa kwa halali au kwa makosa kipindi kile sasa tunafuta hiyo “adhabu” na tunaanza upya huku kila upande ukiaswa kufuata sheria, kanuni, taratibu na misingi iliyowekwa.

Hao wenye magazeti wakivunja tena sheria, utaratibu wa kuwaadhibu utafuatwa bila uonevu kwa kipimo kilekile na uzito wa kosa husika

Mama anaeleweka tu ukiamua kumuelewa
 
Mimi nashangaa! Hivi Rais wetu mpendwa anamaanisha vyombo hivyo vya habari vilionewa! Ati vilifungiwa bila kufuata sheria kweli? Sasa anaposema vifunguliwe vifuate sheria, na hizo sheria zieleweke, kwani Mwanzo walipofungiwa hizo sheria zilikuwa hazieleweki? Kutofahamu sheria si utetezi wa kukuondolea kosa.

Kwa hivyo Rais wetu, anamaanisha kama hivi vyombo vilionewa tu kufungiwa bila kuvunja sheria basi vinauwezo kwenda mahakamani, kuishitaki serikali kudai fidia. Make vimepoteza fedha nyingi ambazo vingepata wakati vimefungiwa kwa kuonewa.
Ushauri wangu, mama awe makini asitake cheap popularity, uwezi sema unafungulia vyombo ili wasiseme kuwa mnafunguia uhuru wa habari.
Rais wetu anamuogopa nani? Huyu atakae sema! Kumbe tuna Rais muoga, anaogopa kusemwa.....! Mmmmh! Yangu macho......!

Rais wetu kumbuka uwezi kumpendezesha kila mtu. Usiogope kusemwa, wewe ni Amiri Jeshi Mkuu.
Hata hawa wanao kusifia, subiri watakusema tu. Rais Kikwete (Mstaafu) Aliwapa uhuru, lakini huyo huyo walimtukana, hadi kumwita ni Dhaifu.
Duniani uwezi ridhisha kila mtu.
Rais wetu chapa kazi, usifanye maamuzi kisha unataka fulani acheke, akuone weye mzuri. Kuwa makini na angalia sheria za nchi zinasemaje.
The past has gone! Mambo yenu ya kutuweka kwenye dhiki ya maisha yameisha wakati wake. Sasa ni wakati wa Faraja, wakati wa maridhiano, wakati wa matumaini. Kaa hapo na roho yako mbaya!!!
 
Relax Abbas yaani hamuwezi kutengeneza sheria za kijinga tukawaangalia tu.

Hivi unajua kutokea 2015 mpaka 2020 ni sheria ngapi kandamizi zimetungwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari?

Yaani imefikia hatua waziri wa Habari ana uwezo wa kufungia media? Hiyo ni nchi au danguro?
Hata hizo nchi mnazoiga mambo, kuna sheria za nchi ambazo haziruhusu watu kubwatuka tu wakidhani wako huru kuandika au kusema lolote. Angalia sheria za habari za mataifa kadhaa Ulaya hata Amerika. Yetu macho tuone kama hakuna chombo kitakachofungiwa. Mie si umdhaniae!
 
Duuu hii nimeipenda ntaamia ccm nisifu nakuabudu kama nikiliona gazeti langu tena Tz Daima aaaaaaaah mama kumi tena aaaaaah kudadadeki oyoooopp aaaaah Mataga Keisha habari yao.
Kipya kinyemi ingawa kidonda. Let's go, we shall see the second page of our book.
 
Mama kaanza kuchukua ushauri wa Kigogo 14

Ni jambo lenye kutia faraja sana

Naona sasa genge la yule Veronica mwenye gololi kwenye suluwale limetupiliwa mbali
Aongeze na mishahara basi ndo ataeleweka. Vinginevyo ni mfyuuuu tu.
 
Mimi nashangaa! Hivi Rais wetu mpendwa anamaanisha vyombo hivyo vya habari vilionewa! Ati vilifungiwa bila kufuata sheria kweli? Sasa anaposema vifunguliwe vifuate sheria, na hizo sheria zieleweke, kwani Mwanzo walipofungiwa hizo sheria zilikuwa hazieleweki? Kutofahamu sheria si utetezi wa kukuondolea kosa.

Kwa hivyo Rais wetu, anamaanisha kama hivi vyombo vilionewa tu kufungiwa bila kuvunja sheria basi vinauwezo kwenda mahakamani, kuishitaki serikali kudai fidia. Make vimepoteza fedha nyingi ambazo vingepata wakati vimefungiwa kwa kuonewa.
Ushauri wangu, mama awe makini asitake cheap popularity, uwezi sema unafungulia vyombo ili wasiseme kuwa mnafunguia uhuru wa habari.
Rais wetu anamuogopa nani? Huyu atakae sema! Kumbe tuna Rais muoga, anaogopa kusemwa.....! Mmmmh! Yangu macho......!

Rais wetu kumbuka uwezi kumpendezesha kila mtu. Usiogope kusemwa, wewe ni Amiri Jeshi Mkuu.
Hata hawa wanao kusifia, subiri watakusema tu. Rais Kikwete (Mstaafu) Aliwapa uhuru, lakini huyo huyo walimtukana, hadi kumwita ni Dhaifu.
Duniani uwezi ridhisha kila mtu.
Rais wetu chapa kazi, usifanye maamuzi kisha unataka fulani acheke, akuone weye mzuri. Kuwa makini na angalia sheria za nchi zinasemaje.
Pole...naona umeumia sana.
 
Ndugu zangu, Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri!!!! Kazi mtindo mmoja!!.

Vikosi vya ulinzi na usalama, chondechonde tulindie Rais wetu. Hatutaki kuja kusikia habari za oooh! unajua!, ohh Umeme!, Sijui Mzena! Sijui nini, Patachimbika hapa!!! Tena Patachimbika bila Sururu!!!! Oohoooo!!!
Tulindie Rais wetu tafadhali!!!! Akina Polepole kaeni mbali msije muambukia itikadi zenu za kununua wapinzani na kubagua raia!!!! Nchi yetu wote.
 
Vifunguliwe na wafuate taratibu

Habari na taarifa ni muhimu sana kwa jamii

Wakianza kuandika tena habari za uchochezi na kuhamasisha hujuma kwa nchi yetu washughulikiwe ipasavyo
Mataga unateseka ukiwa wapi? [emoji3][emoji3][emoji3] Lile dikteta lenu is no more... Mama kashika usukani sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata hizo nchi mnazoiga mambo, kuna sheria za nchi ambazo haziruhusu watu kubwatuka tu wakidhani wako huru kuandika au kusema lolote. Angalia sheria za habari za mataifa kadhaa Ulaya hata Amerika. Yetu macho tuone kama hakuna chombo kitakachofungiwa. Mie si umdhaniae!

Yes vitu vizuri tunaiga. Ulitaka tuige wapi mkuu kama sio huko Amerika na Ulaya?

Kwani mkuu wewe kinachokuuma ni nini ukiacha vyombo vya habari vifanye kazi yake? What are you afraid of?
 
Demokrasia na utawala bora ni muhimu katika ustawi wa binadamu.

YESU NI MWOKOZI
IMG-20210405-WA0009.jpg
 
Back
Top Bottom