Rais Samia Suluhu akiendelea kumkumbatia Majaliwa na Baraza lake Serikali yake haitofanikiwa, Hawana jipya

Kila Rais huwa na Vision yake na ambitions zake, vision ya hayati Magufuli ilikuwa Tanzania ya viwanda ambayo ilishindwa chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, sijajua vision ya rais mpya Mama Samia kuwa ni ile ile ya Tanzania ya viwanda au atakuja na nyingine au hana vision kabisa.

Mwelekeo wa uongozi wa Serikali ya mama Samia haujawa na sauti moja means mwelekeo mmoja, nafikiri hili linatokana na labda na mama Samia kutoonyesha msimamo wake.

Jana Waziri mkuu kaja na vipaumbele 6, kimojawapo ni ‘Hakuna kurudi nyuma’ means wanaendeleza ya mtangulizi kana kwamba Rais aliyepo hana vipaumbele vyake, huku Spika akisema hayati Magufuli alikuwa akishauriwa vibaya means tubadilike.

Mimi naona kama kuna mkakati wa makusudi wa kumkwamisha Rais Samia au kumlazimisha afate vision ya mtangulizi wake. Pamoja na kwamba alisema atayaenzi ya mtangulizi wake haina maana yeye hajui anataka Tanzania ya aina gani.

Mkapa alipoingia madarakani alisema atayaenzi ya muasisi wa Taifa Mwalimu Nyerere ‘yale mazuri’ lkn alikuja kubinafsisha mashirika ya umma kinyume na mwasisi wake tena Mwalimu angali akiwa hai.

Bila ya Rais Samia kuja na serikali yake iliyobeba maono yake itamuwia ngumu kuipeleka Tanzania aipendayo, kwa sababu baraza zima bado ni lilelile, linataka kuendeleza yaleyale maana yake ‘halina jipya’, Waziri mkuu bado ni yule yule aliye na vision ya Tanzania ya viwanda iliyoshindwa. Tutegemee miujiza.
Hivi unajua Gharama Kubwa ambayo Rais akiachana na Waziri Mkuu wa sasa na Kumchagua mwingine Serikali inaingia / itaingia?

Hivi siyo Sisi Watumiaji wa Mitandao ( Keyboard Warriors ) kila Siku tunalalamika Matumizi mabaya ya Fedha na kwamba Serikali ijitahidi kubana Matumizi?

Hivi ni kwanini Watanzania wengi tuna Upako Mkubwa wa Unafiki na Kigeugeu kuliko Raia wa nchini zingine hasa Majirani wanaotuzunguka?

Maamuzi ya Mama ( Rais ) ni sahihi kabisa na hata Mimi nimeyapenda kwamba acha amalize miaka hii Minne ( 4 ) na Premier Majaliwa, ila kama akigombea Urais 2025 na Kushinda nadhani hapo ndipo atamteua Waziri Mkuu wake.

Na binafsi ukiniuliza leo hii niseme naonaje Utendaji wa Premier Majaliwa nitasema kwa 75% anajitahidi na kufanya vyema ila hizo 25% za Mapungufu yake ya Kiutendaji au ya Kibinadamu yako hata Kwako ( Mleta Mada ) na Mimi ( Mchangia Mada ) vile vile.
 
Eti " serikali ya Magufuli ilikua ya viwanda lakini ikafeli" mnadhani viwanda ni gari unanunua tu na kukamilisha usajili? Unapoongelea viwanda kuna factors nyingi wawekezaji wanaangalia kabla ya kujenga viwanda. Ya kwanza kabisa ni amani na utulivu wa nchi
2) nishati ya umeme wa uhakika na bei rahisi
3) miundombinu ya barabara,reli, ndege, bandari nk
4) malighafi (raw materials)
5) cheap and competent labours
6) tax system ya nchi
Nk

Magufuli alianza na miundombinu ya umeme, tunashukuru pia Kikwete aliwekeza kwenye miundombinu ya barabara. Nchi ya viwanda inaandaliwa si chini ya miaka 20, it's not an overnight process, mzee Magufuli alikua na maono, weka reli, weka mabwawa ya umeme, tanua bandari ya dsm, tanga na Mtwara nk bahati mbaya kaondoka bila miradi kukamilika

Sasa huyu anayekuja aamue kama ataendelea au ataacha, mwisho wa siku serikali ni ileile ya CCM. Lakini tumpe credit yule mzee.. alikua na jicho pana
Hakuna kitu alifanya ndo maana mungu katuondolea takataka
 
Ninaendelea kujiuliza kwann mama hajafukuza hawa watesi??? Hawa watu wote kuanzia Kwemye baraza la Mawaziri na Makatibu wakuu waliopo ndio wale wale walioumiza sana Watanzania wenzao...

MAKATIBU WAKUU WA WIZARA NI WALE WALE....akina Joseph Malongo waliolalamikiwa sana kunyanyasa watumishi kuwazushia uongo
 
Sasa yale mahesabu ya viwanda siju elfu 50 na ngapi yalikuwa ya Atoka wapi. Au ndiyo hayo maandalizi?
 
Mama asafishe jumba lake haraka sana kabla hajasafishwa.Aanzie kwa Waziri Mkuu na IGP
 
Hivi unajua Gharama Kubwa ambayo Rais akiachana na Waziri Mkuu wa sasa na Kumchagua mwingine Serikali inaingia / itaingia?

Hivi siyo Sisi Watumiaji wa Mitandao ( Keyboard Warriors ) kila Siku tunalalamika Matumizi mabaya ya Fedha na kwamba Serikali ijitahidi kubana Matumizi?

Hivi ni kwanini Watanzania wengi tuna Upako Mkubwa wa Unafiki na Kigeugeu kuliko Raia wa nchini zingine hasa Majirani wanaotuzunguka?

Maamuzi ya Mama ( Rais ) ni sahihi kabisa na hata Mimi nimeyapenda kwamba acha amalize miaka hii Minne ( 4 ) na Premier Majaliwa, ila kama akigombea Urais 2025 na Kushinda nadhani hapo ndipo atamteua Waziri Mkuu wake.

Na binafsi ukiniuliza leo hii niseme naonaje Utendaji wa Premier Majaliwa nitasema kwa 75% anajitahidi na kufanya vyema ila hizo 25% za Mapungufu yake ya Kiutendaji au ya Kibinadamu yako hata Kwako ( Mleta Mada ) na Mimi ( Mchangia Mada ) vile vile.
Hakuna wa kumzuia mama asigombee na kushinda 2025....she is there to stay na kuliongoza Taifa.
 
suluhu ya kuondoa sintofahamu zote hizi za kila rais kuwa na vision yake ni kuwa na Katiba Mpya tu.

tatizo watu wakidai Katiba Mpya wanaitwa magaidi.
 
Ninaendelea kujiuliza kwann mama hajafukuza hawa watesi??? Hawa watu wote kuanzia Kwemye baraza la Mawaziri na Makatibu wakuu waliopo ndio wale wale walioumiza sana Watanzania wenzao...

MAKATIBU WAKUU WA WIZARA NI WALE WALE....akina Joseph Malongo waliolalamikiwa sana kunyanyasa watumishi kuwazushia uongo
Mpaka umtaje mtu jina basi huo siyo wivu?
Kwanini tunapenda majungu ndugu zangu? Chapeni kazi, heshimu viongozi wako, hatuwezi kuwa wote viongozi bali aliyechaguliwa ndiye afaaye kwa wakati huo.
 
Mpaka umtaje mtu jina basi huo siyo wivu?
Kwanini tunapenda majungu ndugu zangu? Chapeni kazi, heshimu viongozi wako, hatiwezi kiwa wote viongozi bali aliyechaguliwa ndoye afaaye kwa wakati huo.
Aliemtaja Majaliwa sio jina?? Sio wivu ?? Ukitenda ubaya utatajwa kwa ubaya huo huo...
 
Hivi unajua Gharama Kubwa ambayo Rais akiachana na Waziri Mkuu wa sasa na Kumchagua mwingine Serikali inaingia / itaingia?

Hivi siyo Sisi Watumiaji wa Mitandao ( Keyboard Warriors ) kila Siku tunalalamika Matumizi mabaya ya Fedha na kwamba Serikali ijitahidi kubana Matumizi?

Hivi ni kwanini Watanzania wengi tuna Upako Mkubwa wa Unafiki na Kigeugeu kuliko Raia wa nchini zingine hasa Majirani wanaotuzunguka?

Maamuzi ya Mama ( Rais ) ni sahihi kabisa na hata Mimi nimeyapenda kwamba acha amalize miaka hii Minne ( 4 ) na Premier Majaliwa, ila kama akigombea Urais 2025 na Kushinda nadhani hapo ndipo atamteua Waziri Mkuu wake.

Na binafsi ukiniuliza leo hii niseme naonaje Utendaji wa Premier Majaliwa nitasema kwa 75% anajitahidi na kufanya vyema ila hizo 25% za Mapungufu yake ya Kiutendaji au ya Kibinadamu yako hata Kwako ( Mleta Mada ) na Mimi ( Mchangia Mada ) vile vile.
Yes amalize na Majaliwa ili 2025 aje na wake ingawa kew VP alichemka sana ila ndo hivyo tena
 
Kila Rais huwa na Vision yake na ambitions zake, vision ya hayati Magufuli ilikuwa Tanzania ya viwanda ambayo ilishindwa chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, sijajua vision ya rais mpya Mama Samia kuwa ni ile ile ya Tanzania ya viwanda au atakuja na nyingine au hana vision kabisa.

Mwelekeo wa uongozi wa Serikali ya mama Samia haujawa na sauti moja means mwelekeo mmoja, nafikiri hili linatokana na labda na mama Samia kutoonyesha msimamo wake.

Jana Waziri mkuu kaja na vipaumbele 6, kimojawapo ni ‘Hakuna kurudi nyuma’ means wanaendeleza ya mtangulizi kana kwamba Rais aliyepo hana vipaumbele vyake, huku Spika akisema hayati Magufuli alikuwa akishauriwa vibaya means tubadilike.

Mimi naona kama kuna mkakati wa makusudi wa kumkwamisha Rais Samia au kumlazimisha afate vision ya mtangulizi wake. Pamoja na kwamba alisema atayaenzi ya mtangulizi wake haina maana yeye hajui anataka Tanzania ya aina gani.

Mkapa alipoingia madarakani alisema atayaenzi ya muasisi wa Taifa Mwalimu Nyerere ‘yale mazuri’ lkn alikuja kubinafsisha mashirika ya umma kinyume na mwasisi wake tena Mwalimu angali akiwa hai.

Bila ya Rais Samia kuja na serikali yake iliyobeba maono yake itamuwia ngumu kuipeleka Tanzania aipendayo, kwa sababu baraza zima bado ni lilelile, linataka kuendeleza yaleyale maana yake ‘halina jipya’, Waziri mkuu bado ni yule yule aliye na vision ya Tanzania ya viwanda iliyoshindwa. Tutegemee miujiza.
Mama hana vision yeye ni bendera fuata upepo tu, akiwa na lengo la kuwaita vyama vya upinzani kuleta usawa wa kisiasa huambiwa achana nao na yeye anasema sawa, akiambiwa sasa mbowe ashtakiwe kama gaidi anasema sawa, akiwa na nia ya kuleta katiba mpya akiambiwa sasa haina mana anasema sawa tu, akiambiwa tozo za simu zitajenga barabara vijijini japo wananchi wanyonge wanaumizwa yeye anasema sawa tu, alivyoeka ahadi na Tundu Lissu kumpigia simu siku ya pili akaambiwa achana naye naye akaacha tu.

Alivyoingia madarakani akiitaja Zanzibar sana kwenye usawa wa mapato sasa amenyamaza na kutulia kama moja, Kuna watu wanamtibua tibua kwenye malengo yake kuhusu uviko19 kaamua kuwakalia kimya tu maana huenda wanatumwa kikundi kilichoko juu yake na yeye anaacha tu.

Mambo tele sasa nchi inakwenda ndivyo sivyo tu.
 
Hakuna kitu alifanya ndo maana mungu katuondolea takataka

Mkuu Mungu haondoi takataka. Anawachukua Wema na kuwaacha takataka kama wewe. Lugha ya Mungu Ni uvumilivu and Judge no one. One finger against four fingers. Take care jinga la dunia.
 
Una maana wote waliokufa ni wema.
 
I said it ukajifanya kiziwi.

"Kuna makundi wanajua wanayoyafanya ndani ya serikali,na yanageuka kusema serikali ya awamu ya 6 ufisadi umerudi mambo yako hovyo kumbe wao ndio wako hovyo,mambo hayo yalifanyika huko nyuma,gari bovu linaangushiwa awamu ya 6 sitakubali"-Rais Samia Suluhu
 
“Mimi naona kama kuna mkakati wa makusudi wa kumkwamisha Rais Samia au kumlazimisha afate vision ya mtangulizi wake. Pamoja na kwamba alisema atayaenzi ya mtangulizi wake haina maana yeye hajui anataka Tanzania ya aina gani”. -Quinine.
 
Huna akili kabisa!

Sasa yeye ni mjinga kama ana power yote alafu anakwamishwaje?
 
Back
Top Bottom