GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Hivi unajua Gharama Kubwa ambayo Rais akiachana na Waziri Mkuu wa sasa na Kumchagua mwingine Serikali inaingia / itaingia?Kila Rais huwa na Vision yake na ambitions zake, vision ya hayati Magufuli ilikuwa Tanzania ya viwanda ambayo ilishindwa chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, sijajua vision ya rais mpya Mama Samia kuwa ni ile ile ya Tanzania ya viwanda au atakuja na nyingine au hana vision kabisa.
Mwelekeo wa uongozi wa Serikali ya mama Samia haujawa na sauti moja means mwelekeo mmoja, nafikiri hili linatokana na labda na mama Samia kutoonyesha msimamo wake.
Jana Waziri mkuu kaja na vipaumbele 6, kimojawapo ni ‘Hakuna kurudi nyuma’ means wanaendeleza ya mtangulizi kana kwamba Rais aliyepo hana vipaumbele vyake, huku Spika akisema hayati Magufuli alikuwa akishauriwa vibaya means tubadilike.
Mimi naona kama kuna mkakati wa makusudi wa kumkwamisha Rais Samia au kumlazimisha afate vision ya mtangulizi wake. Pamoja na kwamba alisema atayaenzi ya mtangulizi wake haina maana yeye hajui anataka Tanzania ya aina gani.
Mkapa alipoingia madarakani alisema atayaenzi ya muasisi wa Taifa Mwalimu Nyerere ‘yale mazuri’ lkn alikuja kubinafsisha mashirika ya umma kinyume na mwasisi wake tena Mwalimu angali akiwa hai.
Bila ya Rais Samia kuja na serikali yake iliyobeba maono yake itamuwia ngumu kuipeleka Tanzania aipendayo, kwa sababu baraza zima bado ni lilelile, linataka kuendeleza yaleyale maana yake ‘halina jipya’, Waziri mkuu bado ni yule yule aliye na vision ya Tanzania ya viwanda iliyoshindwa. Tutegemee miujiza.
Hivi siyo Sisi Watumiaji wa Mitandao ( Keyboard Warriors ) kila Siku tunalalamika Matumizi mabaya ya Fedha na kwamba Serikali ijitahidi kubana Matumizi?
Hivi ni kwanini Watanzania wengi tuna Upako Mkubwa wa Unafiki na Kigeugeu kuliko Raia wa nchini zingine hasa Majirani wanaotuzunguka?
Maamuzi ya Mama ( Rais ) ni sahihi kabisa na hata Mimi nimeyapenda kwamba acha amalize miaka hii Minne ( 4 ) na Premier Majaliwa, ila kama akigombea Urais 2025 na Kushinda nadhani hapo ndipo atamteua Waziri Mkuu wake.
Na binafsi ukiniuliza leo hii niseme naonaje Utendaji wa Premier Majaliwa nitasema kwa 75% anajitahidi na kufanya vyema ila hizo 25% za Mapungufu yake ya Kiutendaji au ya Kibinadamu yako hata Kwako ( Mleta Mada ) na Mimi ( Mchangia Mada ) vile vile.