HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewapongeza Tabora United kwa ushindi wa goli 3-1 walioupata leo Novemba 7, 2024 dhidi ya Yanga SC.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rais Samia amendika hivi:
“Pongezi kwa Tabora United kwa ushindi wenu dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu.
“Ninyi na klabu zote washiriki mnaipa Ligi hii thamani inayovutia uwekezaji kibiashara na ajira, na yenye mvuto wa kipekee katika ukanda huu wa Afrika. Endeeleni kutoa burudani kwa mamilioni ya Watanzania ndani na nje ya nchi yetu.”
siku ya simba day ,tuliomwelewa modewj wachache, tukujiuliza inakuwaje aanze kumshukuru madam president na kutaka kulia wakati ni siku ya furaha sio msiba