Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Mama kachachamaa wapigaji wote na majizi yote awamu hii ya mama watakoma, big up Mheshimiwa.
Big up ya nini hapa? Kumsimamisha mtu kazi ilhali anaendelea kupokea mshahara wake kamili si jambo la kupongezwa, ni hasara kwa serikali inamlipa mtu bila kufanya kazi yeyote ile na hata hatujui ni kwa muda gani. Ningelimpa big up kama angelimsimamisha bila malipo au kumuachisha kazi moja kwa moja.
 
Mbona Magu alikuwa anateuwa na kutumbua wasipotekeleza wajibu!!? au hili swala umelisahau.....kwa ufupi wa fikra zako
Danganya toto tu hizo, alitumbua then? Tumia hizo fikra zako unazoziona ni ndefu kufikiri. Kila siku ilikuwa ni tumbua tumbua tu, kwa kiongozi mwenye dira ilipaswa akae na ajitafakari anakosea wapi ili arekebishe maana wateule wake walikuwa reflection yake.
 
Maana yake unatakiwa kufahamu kuanzia sasa ya kwamba huyo kigogo siyo mtu kama mtu! Ni wasaidizi wa chama na Serikali wa Rais aliyefariki, na ambao hawakupata/hawakupewa nafasi ya kumshauri mhusika! kutokana na aina ya mtawala mwenyewe aliye jisifia mara kadhaa ya kwamba si mtu wa kushaurika.

Hivyo waliamua kutumia social media kufikisha ujumbe wao kwa jamii kutokana na hayo madudu ambayo hawakufurahishwa nayo.
 
Ukiangalia jinsi rais alivyomsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa TPA ni uamuzi aliouchukua hapohapo baada ya kusomewa ripoti na CAG,sasa huyu kigogo alijuaje???..au kulikuwa na mipango ya mkurugenzi kutimuliwa kabla ya ripoti kusomwa??..huenda huyu kigogo anafanya kazi vizuri kabisa na serikali,baadhi ya viongozi wakubwa serikalini bila mzee pombe kujua..yaani rais alikuwa anazungukwa na wateuwa wake kwa maslahi Fulani!..
Jana vitasa vya ofisi ya huyu kibaka kiburi vilibadilishwa ili asiweze kuingia ofisini kuharibu taarifa. Natamani na ofisi ya Dotto James nayo ivamiwe leo. Ili tujue pesa alizo kuwa ana mlipa Musiba alikuwa anazitoa kutoka fungu gani. Hawa ngosha wakituhujumu mnoo!!!
 
Alimuambia Kakoko kesho asiende Kazini kwa Vitasa vya mlango vimeshabadilishwa na asubiri taarifa tu.
Na kweli Mh. Samia kashatoa taarifa ya kumsimamisha kazi.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Mbona hii post ya kigogo ni ya leo March 28 saa 5 na dk 17...sema ka ipost in a such a way ionekana ya jana...Muda ambao mama alikua keshatoa maelekezo
Screenshot_20210328-124310_Twitter.jpg
 
Hata aliekuwa boss wake (kwa sasa ni marehemu) kule mwanzo mwanzo alianza kwa speed hivyo kadri siku zilivyokuwa zinaenda mgigo ukawa unpugwa vile vile
Betri ilikuwa inaisha chaji, huyu hatumii betri
 
Na sijui anajuaje maana ripoti yenyewe Mama kaisoma usiku wa leo
Kunakuwa na summary ambayo inaelezea mambo muhimu anapewa. Yale ma-book yote ni mengi kwa Rais kusoma mwenyewe. Anakuwa na wasaidizi wengi ambao ndiyo wataipitia kwa undani.
 
Hivi mtu imethibitika kaiba tena baada ya uchunguzi wa muda... Adhabu ni kusimamishwa kazi au kuwekwa ndani?
Hizi Bil 3.6 serikali inarecover vipi na mwizi yuko hapo, je kusimamishwa kazi inatosha?
 
Ukiangalia jinsi rais alivyomsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa TPA ni uamuzi aliouchukua hapohapo baada ya kusomewa ripoti na CAG,sasa huyu kigogo alijuaje???..au kulikuwa na mipango ya mkurugenzi kutimuliwa kabla ya ripoti kusomwa??..huenda huyu kigogo anafanya kazi vizuri kabisa na serikali,baadhi ya viongozi wakubwa serikalini bila mzee pombe kujua..yaani rais alikuwa anazungukwa na wateuwa wake kwa maslahi Fulani!..
Kigogo ameongea baada ya Rais kumsimamisha kazi tu ndio akatweet. Tumieni akili zenu wakati mwingine sio kila kitu uambiwe na watu au kigogo
 
Back
Top Bottom