Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Ripoti ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ametoa agizo la kusimamishwa Mkurugenzi Mkuu wa Bandari(TPA) kutokana ubadhirifu mkubwa unaoikumba mamlaka hiyo.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema haya

“Ripoti nimeona, nimeipitia na nimebaini ubadhirifu mkubwa uliofanywa pale bandari, hili suala mnatakiwa kushirikiana, nakuomba Takukuru jishughulishe pale, alipita Waziri Mkuu alilishughulikia.

“Waziri Mkuu aliunda kamati na wakafanya uchunguzi kidogo ambao yaliyotoka, hatua chache zilichukuliwa lakini imani yangu ni kwamba kama kuna ubadhirifu pale waliosimamishwa ni hawa wa chini huku, ninaomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu hatua zaidi ziendelee,”
Mwendo ni ule ule wa Hapa kazi tu
 
Simlikuwa mnasema kuwa huyu CAG ameletwa hapo na Magufuri ili afiche madhaifu ya serikali, sasahivi anafichua madhaifu mnaanza Magufuri asingeliwatumbua, kwani Samia amejifunzia wapi kutumbua?huyo mkuu wa TPA alikuwa analiwa taming tu maana Muasibu wake mkuu Alisha simamishwa kitambo na Majariwa na kuagiza uchunguzi wa ubadhirifu ufanyike na lipoti itolewe,sasa kuna jipya gani hapo wakati watu tulikuwa tunasubiri lipoti ya Majariwa?
Tofauti na sasa ni kuwa iliagizwa Mkurugenzi Mkuu ndiye aongoze Uchunguzi! Toka lini mtuhumiwa anajichunguza!
 
Huyu ni hatari kwa usalama wa nchi, haiwezekani habari confidential ya nchi mtu wa pembeni anaipata within seconds, sio jambo la kufurahia japo najua wabongo kwa ujumla wetu tunapenda ubuyu. Binafsi sipendi, Rais anaandika kinote then within seconds kigogo ameipublish huko twitani, sio sawa hata kidogo...
Vyombo vya habari vikiwa huru hata Kigogo hataskika kwa ukubwa huo
 
Wizi na ubadhilifu ulikuwepo tulifichwa na bwana yule. Alitumbua baadhi wengine akawaacha, hasa wake wa Kanda pendwa.
Ni kweli kabisa ubadhilifu ulikuwepo ila sielewi hili ripoti ni ya wiki mbili hizi za msiba au ni ile ile amabayo marehemu angekabidhiwana CAG?
 
Jibu hoja mkuu, majibu ya namna hiyo yanadhihirisha how empty your pumpkin is...
Avator yako inaonesha jinsi you are still living in his era, in short you are under denial. Move on bwashee.
Kama sio ubuyu how could we have known the state of our former Chief?! Tell me how?!
Didn't you hear what PM had to say the whereabouts of our former chief when the nation was smelling smoke ? how could we have known that we were being told was a lie if it was not for what you call ubuyu!! Tafakar...chukua hatua.... move on.
 
Cjawahi pigia mtu kelele kwanza.. Pili cna haja ya kutafuta hutuba ninavojua alifukuza watu wengi hapo bandarini akidai ni wezi akaweka watu wake waaminifu sasa huu ubadhirifu imekuaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani huu wizi ni mfumo flani pale bandarinim maana waziri mkuu amekua akifuatilia bila mafanikio nadhani kuna kitu tusichofahamu pale
 
Mleta uzi hebu kunywa maji glass mbili kisha lala chali kwa dakika 15 halafu uje ufafanue vizuri uzi wako
 
Ni kweli kabisa ubadhilifu ulikuwepo ila sielewi hili ripoti ni ya wiki mbili hizi za msiba au ni ile ile amabayo marehemu angekabidhiwana CAG?
Report wala siyo ya wiki mbili. Report ndiyo hiyo hiyo ambayo angekabidhiwa marehemu. Lakini haya uliyoyasikia leo usongesikia CAG akisema. Angeanzaje kusema ATCL imefanya hasara kwa miaka 5 wakati marehemu alishawaambia watz shirika limeingiza faida ya bil 28 tangu ndege mpya zinunuliwe? Na serikali ilipata gawio?
Hiyo habari ya ATCL isingesomwa kabisa.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Injinia Deusdedit Kakoko kupisha uchunguzi "Kuna ubadhirifu mkubwa Bandarini naomba TAKUKURU ikafanye kazi, nimeletewa ripoti ya ubadhirifu wa Bilioni 3.6.

View attachment 1736617

Imani yangu ni kwamba ndani ya Shirika la Bandari kuna ubadhirifu kama wa Tsh. Bilioni 3.6 lakini Waziri Mkuu amefanya ukaguzi na waliosimamishwa ni wa chini, nimeomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu uchunguzi uendelee" --- Rais Samia Suluhu.
Mwanzo mzuri.
 
Anaembuliwa ni marehemu kwa kulinda watu wake na huu ni mwanzo tu.
Wewe naweeeee
Hivi ukifa kabla ya kutekeleza baadhi ya mipango yako unaumbuliwa🤔🤔
Basi Jiangalie sana na wewe na mipango yako usijeumbuliwa ukiwa marehemu
 
Avator yako inaonesha jinsi you are still living in his era, in short you are under denial. Move on bwashee.
Kama sio ubuyu how could we have known the state of our former Chief?! Tell me how?!
Didn't you hear what PM had to say the whereabouts of our former chief when the nation was smelling smoke ? how could we have known that we were being told was a lie if it was not what you call ubuyu!! Tafakar...chukua hatua.... move on.
There's a sense in what you've written, I can't argue with you on that. But saying I'm under denial soon after the demise of our beloved is overstatement. He just died for goodness sake!

Bado nasimamia pale pale, huwezi kuruhusu info so confidential kutoka mamlaka zivuje kizembe namna hii, hili hatari hata kwa maadui wa nchi wakitaka kutuumiza wanamhonga huyo informer wenu then paaap we're all under threat. Think mkuu!
 
Kila la Kheri mama safisha uchafu wote, tupo pamoja, tunaomba utupandishe daraja ajira ya 2014, mimi ni mpinzani mwenye mahaba na mama kipenzi cha watanzania, Mungu akupe ulinzi inshaalah
Asitusahau na wa 2016
 
Haya mambo haya
IMG_20210328_134816.jpg
 
Ndio Raisi kasema nae asimame kupisha uchunguzi kama hana hatia atarudi.
Katika moja ya maneno ya PM kwenye ziara yake, alimuasa DG kutimiza wajibu wake baada ya kuwasimamisha baadhi ya watendaji kazi, it is as if alikuwa na kakinga Fulani kwakuwa PM alionekana kutofurahishwa na utendaji kazi wake ila hakuwa na namna ya kumuwajibisha
 
Back
Top Bottom