Kukaa kimya wakati unatakiwa kuzungumza siyo hekima hata kidogo!! Kukaa kimya wakati ni wewe peke yako unayetakiwa kutoa suluhisho siyo hekima hata kidogo! Ni woga! ni kukwepa jukumu ambalo ni wewe peke yako unasubiriwa ulitoe!! Kukaa kimya wakati suluhisho la haraka linatakiwa ni kutokujiamini!! Tukubali kuusema ukweli hata kama tunataka nafasi za uteuzi!!! Mama tunampenda lakini hapa amefeli!! Ameamua kuyaacha mambo yaende hivyo hivyo liwalo na liwe!! Historia itamhukumu!!
Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka 1990+ Zanzibar ilikuwa inataka kujiunga OIC binafsi, pamoja na kuwa yenyewe ni sehemu ya TANZANIA. Wakati huo, Rais wetu alikuwa ni M- Zanzibari, Ali Hassan Mwinyi.
Huku Bara, Watu wengi walipinga mpango huo. Wabunge Bungeni, nako wakaja juu. Rais Mwinyi, akaonyesha BUSARA yake, ya KUKAA KIMYA tu! Asasi mbali mbali zikapiga kelele, na hasa ukizingatia kuwa hiyo OIC ikitafsiriwa kuwa ni ya kidini dini, Kiislamu! Rais Mwinyi, akawa anapiga kimya tu!
Wakaibuka akina Njelu Kasaka na G55 yao, wakadai, kama ni hivyo, basi nasi tuifufue Tanganyika yetu, kwani wenzao Zenji wameshajionyesha ni NCHI, na wanaweza wakajiamulia mambo yao hata ya KIMATAIFA bila kuihusisha TANGANYIKA. Rais Mwinyi, kimya!
Mchakato wa KUIFUFUA TANGANYIKA ukaanza! Ukapelekwa Bungeni, Spika Pius Msekwa, Waziri Mkuu Malecela, Katibu Mkuu CCM Horace Kolimba. Rais Mwinyi, KIMYAA!
Watu wote tukajua, sasa Tanganyika inafufuka! Wakati wote huo, Mwalimu Nyerere yupo, anaangalia tu! Alivyoona hali imekuwa mbaya, na kutambua kuwa ule UKIMYA wa Mwinyi, si BUSARA, bali ni kushindwa kuliendesha gari. Akaingilia kati. Akamshauri aizime ile hali. Lakini Mwinyi, hakujua aanzie wapi! (Kwa wanao kumbuka, Nyerere alidai Mwinyi alikuwa DHAIFU, akamtungia na kitabu). Rais Mwinyi, akaomba Mwalimu, amsaidie, kwani pamoja na kuwa yeye alikuwa ndiye Rais, lakini alikuwa hajui atalimalizaje!
Mwalimu akamwambia, kwanza FUKUZA Malecela kama Waziri Mkuu, pia, FURUSHA Horace Kolimba kama Katibu Mkuu wa CCM. Kwani hawa hawakukushauri vizuri, mpaka hali kufikia hapo ilipokuwa. Pia, ZANZIBAR, IACHANE NA MPANGO WA KUJIUNGA NA OIC!
Yakafanyika hayo! Pia, tukaahidiwa kuwa, TANZANIA itaangalia KUJIUNGA kama Nchi, sio upande fulani. IKAWA IMETOKA HIYOOO! Mliokuwepo, mnakumbuka!
Lile suala la G55 na kuitaka TANGANYIKA, Mwalimu alilimaliza, kama KUMCHINJA NG'OMBE BILA KUTOKA DAMU! Alienda Bungeni, na kuhutubia Wabunge. Na wakati ule, Wabunge wote walikuwa ni wa CCM. Akawaambia akina Njelu Kasaka kuwa, sera ya CCM, Tanzania ni ya serikali mbili. Kama kuna mtu hataki hivyo, ahame chama, kwani vipo vyama vyenye kuamini Serikali tatu, nne nk. Nendeni huko, tunaoamini serikali mbili mtuachie CCM yetu!
Huo ndiyo ukawa mwisho wa G55.
Sasa, hili la BANDARI, naona linafanana! Rais, ni Mzenji! Pia, upande mmoja wa Muungano hauhusiki! Kelele zimekuwa nyingi kama wakati ule. Rais, yupo kimyaaaa! Na tunamsifu! Sidhani kama kukaa kimya ni vizuri! Kwa sasa, tumeona kila kukicha, watu wanaibuka wapya, tena wengine wanaongea maneno ya hatari, chuki, kutugawa!
Leo hii, Mwalimu hayupo. Inawezekana washauri waliopo karibu na Rais, sio wazuri. Wao, wapo kwa ajili ya masirahi yao. Wapo wanaotaka AHARIBIKIWE! Yupo kwenye boti ziwani. Ziwa limechafuka. Mizigo mingi botini. Usalama wa abiria na boti lenyewe, ni kupunguza uzito. Kama anaamini atafika nchi kavu salama bila kupunguza uzito kwa kutupa majini baadhi ya mizigo, sawa! Kinyume cha hivyo, asione aibu. Wala haitakuwa ni kushindwa. TUACHANE NALO!
Ila, inabidi, ZA KIKWETE, ZETU HUKU MITANDAONI,ZA WARAKA NK ACHANGANYE NA ZAKE!