Rais Samia Suluhu ana emotional intelligence, utulivu wa hali ya juu

Halafu mama ajue huko CCM kuna watu walikuwa wanamsubiri ateleze!! Muda huu wanachekea tumboni tu wakiwa mbele yake, lakini wakiwa wenyewe wanafanya sherehe!! Wakiwa mbele yake "wanaunga" mkono mkataba wa bandari kinafiki!! Kama mama anadhani ana watu huko labda ni ile aina ya kina Nape, tu lakini wale vigogo wenyewe hawako pamoja naye!! Atalazimika kunyoosha mikono mwenyewe!!
 
Kumsifia baba mwenye nyumba kwa kukaa kimya wakati watu wa nyumbani kwake wanampigia kelele mwizi aliyekwapua ng'ombe wa familia nao ni uchizi wa aina yake!!
 
Niliamuwa kunyamaza kimya, na naendelea kunyamaza kimya. - Mama Samia.
 
Pascal Mayalla una maoni yoyote hapa brother?

Mimi Kwa maoni yangu, huyu ndugu So special ndiye katoa jibu sahihi la hoja zote za mleta mada ndugu Robert Heriel Mtibeli.

Na nakubaliana kabisa na So special. Huu sio utulivu wa kawaida. Huu ni utulivu wa kupigwa na bumbuwazi ili ibilisi afanye kazi yake. Ni kiburi cha hovyo...

Kuna mambo ya kukaa kimya kama jibu na shida ikaisha. Lakini kuna mambo ambayo ni lazima kiongozi awe very pro - active, firm and intelligently aggressive bila kusahau kutumia hekima na busara katika kila hatua ya maamuzi ili kuleta usawazisho wa haraka ktk jamii iliyo ktk mgongano wa mawazo kabla ya uharibifu kutokea.

Kwa hili, bila shaka Kuna watakaosema, ooh mbona Hayati Magufuli alikuwa very aggressive na mkamsema sana..

Ni kweli, Magufuli alikuwa very aggressive lakini bila busara wala hekima. Hii ndiyo ilikuwa shida yake kubwa yule Mzee...
 
Waarabu wamemshika pabaya!! Hawana adabu wale!! Lazima watamwaibisha!!
Halafu hawana huruma. Jana BBC imetoa habari kuwa maaskari wa Saudi Arabia wakiwakuta wahamiaji haramu mpakani kutoka Afrika wanaokwenda kutafuta maisha hawana salia mtume, bali huwapiga risasi hapo hapo na kuwaua. Wameuawa wengi sana na wanawazika kwa kificho. Mijitu mikatili kweli kweli hii.
FaizaFoxy

 
Mtu amedakwa kuweupe hana pa kutokea uliktaka ajibu nini ,mkataba amesain youe hana wa kumsingizia
 
Tumefika hapa kwa kuonea aibu kama unavyosema ,kutowajibishana mtu anaiba hapa anapelekwa Pele, lazima wizi utaongezekaz tu
 
Sawa Samia anastahili pongezi. Je nani hastahili pongezi na kwa sababu zipi ? Hapo nd msingi wa hoja yangu ilipoanzia na nilikuwa namjibu mtoa mada kwa rejea kuntu.
 
Akili kubwa iliyo barikiwa utulivu mkubwa.
Ni binaadamu wachache walio barikiwa hivyo.
Mungu azidi kumlinda Rais wetu.
 
Tumefika hapa kwa kuonea aibu kama unavyosema ,kutowajibishana mtu anaiba hapa anapelekwa Pele, lazima wizi utaongezekaz tu

Wizi lazima uwepo ikiwa kuna Watu hawashtakiwi.
Katiba iwekwe Sawa. Yeyote ashtakiwe hapo ndio tutapata PA kuanzia
 
Utulivu wa kuagiza wanaopingwa washikiliwe bila kwenda mahakaman .utulivu ni kutoendana na mood ya mjadala ili kujipa muda kuamua vizuri.ukimya ni kukosa cha kujibu juu ya hoja 7 za TEC .MAMA Samia ni mkimya sio mtulivu
 
Utulivu wa kuagiza wanaopingwa washikiliwe bila kwenda mahakaman .utulivu ni kutoendana na mood ya mjadala ili kujipa muda kuamua vizuri.ukimya ni kukosa cha kujibu juu ya hoja 7 za TEC .MAMA Samia ni mkimya sio mtulivu

Ukimya ni sehemu ya utulivu Mkuu.
Ila ukimya sio utulivu
 
This should be laminated then thread closed.

Mleta mada anachanganya emotional intelligence na arrogance. Kwa circumstance ya hili sakata, na hiyo statement yake ni wazi ni mjivuni mwingi wa kiburi.
 
Ukimya ni sehemu ya utulivu Mkuu.
Ila ukimya sio utulivu
Sawa mama ni mkimya kwa kuwa hajibu hoja (hana majibu) ila sio mtulivu kwa kuwa kashatumia mabavu kuvunja katiba na quran kwa kulaza watoto wa wenzie wenye mama zao kama Rashid ndani kihuni
 
Isee hii tafakuri ni kama ume copy na paste toka mawazoni mwangu.
Nilijadili hili jana kijiwe cha soga. Wakapiga kimya watetezi wake wakabaki ku suffocate.
 
Sawa mama ni mkimya kwa kuwa hajibu hoja (hana majibu) ila sio mtulivu kwa kuwa kashatumia mabavu kuvunja katiba na quran kwa kulaza watoto wa wenzie wenye mama zao kama Rashid ndani kihuni

Unaweza kuwa Sawa kuwa Hana utulivu Kwa 100% ambalo ni Jambo la kawaida.
Ila hakosi 60%

Ukilinganisha na waliomtangulia.
Ngoja tusubiri amalize miaka yake tutakuja kuhitimisha.
 
Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka 1990+ Zanzibar ilikuwa inataka kujiunga OIC binafsi, pamoja na kuwa yenyewe ni sehemu ya TANZANIA. Wakati huo, Rais wetu alikuwa ni M- Zanzibari, Ali Hassan Mwinyi.
Huku Bara, Watu wengi walipinga mpango huo. Wabunge Bungeni, nako wakaja juu. Rais Mwinyi, akaonyesha BUSARA yake, ya KUKAA KIMYA tu! Asasi mbali mbali zikapiga kelele, na hasa ukizingatia kuwa hiyo OIC ikitafsiriwa kuwa ni ya kidini dini, Kiislamu! Rais Mwinyi, akawa anapiga kimya tu!
Wakaibuka akina Njelu Kasaka na G55 yao, wakadai, kama ni hivyo, basi nasi tuifufue Tanganyika yetu, kwani wenzao Zenji wameshajionyesha ni NCHI, na wanaweza wakajiamulia mambo yao hata ya KIMATAIFA bila kuihusisha TANGANYIKA. Rais Mwinyi, kimya!
Mchakato wa KUIFUFUA TANGANYIKA ukaanza! Ukapelekwa Bungeni, Spika Pius Msekwa, Waziri Mkuu Malecela, Katibu Mkuu CCM Horace Kolimba. Rais Mwinyi, KIMYAA!
Watu wote tukajua, sasa Tanganyika inafufuka! Wakati wote huo, Mwalimu Nyerere yupo, anaangalia tu! Alivyoona hali imekuwa mbaya, na kutambua kuwa ule UKIMYA wa Mwinyi, si BUSARA, bali ni kushindwa kuliendesha gari. Akaingilia kati. Akamshauri aizime ile hali. Lakini Mwinyi, hakujua aanzie wapi! (Kwa wanao kumbuka, Nyerere alidai Mwinyi alikuwa DHAIFU, akamtungia na kitabu). Rais Mwinyi, akaomba Mwalimu, amsaidie, kwani pamoja na kuwa yeye alikuwa ndiye Rais, lakini alikuwa hajui atalimalizaje!
Mwalimu akamwambia, kwanza FUKUZA Malecela kama Waziri Mkuu, pia, FURUSHA Horace Kolimba kama Katibu Mkuu wa CCM. Kwani hawa hawakukushauri vizuri, mpaka hali kufikia hapo ilipokuwa. Pia, ZANZIBAR, IACHANE NA MPANGO WA KUJIUNGA NA OIC!
Yakafanyika hayo! Pia, tukaahidiwa kuwa, TANZANIA itaangalia KUJIUNGA kama Nchi, sio upande fulani. IKAWA IMETOKA HIYOOO! Mliokuwepo, mnakumbuka!
Lile suala la G55 na kuitaka TANGANYIKA, Mwalimu alilimaliza, kama KUMCHINJA NG'OMBE BILA KUTOKA DAMU! Alienda Bungeni, na kuhutubia Wabunge. Na wakati ule, Wabunge wote walikuwa ni wa CCM. Akawaambia akina Njelu Kasaka kuwa, sera ya CCM, Tanzania ni ya serikali mbili. Kama kuna mtu hataki hivyo, ahame chama, kwani vipo vyama vyenye kuamini Serikali tatu, nne nk. Nendeni huko, tunaoamini serikali mbili mtuachie CCM yetu!
Huo ndiyo ukawa mwisho wa G55.
Sasa, hili la BANDARI, naona linafanana! Rais, ni Mzenji! Pia, upande mmoja wa Muungano hauhusiki! Kelele zimekuwa nyingi kama wakati ule. Rais, yupo kimyaaaa! Na tunamsifu! Sidhani kama kukaa kimya ni vizuri! Kwa sasa, tumeona kila kukicha, watu wanaibuka wapya, tena wengine wanaongea maneno ya hatari, chuki, kutugawa!
Leo hii, Mwalimu hayupo. Inawezekana washauri waliopo karibu na Rais, sio wazuri. Wao, wapo kwa ajili ya masirahi yao. Wapo wanaotaka AHARIBIKIWE! Yupo kwenye boti ziwani. Ziwa limechafuka. Mizigo mingi botini. Usalama wa abiria na boti lenyewe, ni kupunguza uzito. Kama anaamini atafika nchi kavu salama bila kupunguza uzito kwa kutupa majini baadhi ya mizigo, sawa! Kinyume cha hivyo, asione aibu. Wala haitakuwa ni kushindwa. TUACHANE NALO!
Ila, inabidi, ZA KIKWETE, ZETU HUKU MITANDAONI,ZA WARAKA NK ACHANGANYE NA ZAKE!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…