Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu wahenga walishasema "nyota njema huonekana asubuhi", kwa kazi nzuri na ya kutukuka anayoifanya Mh. Rais katika kuijenga Tanzania mpya, ni dhahiri uchaguzi ujao utakuwa mwepesi Sana kwake kuweza kupita. Kwa Sasa hakuna mpinzani yeyote mwenye mwelekeo wala nguvu ya kuweza kuja kumtikisa Mh. Rais uchaguzi ujao.
Hii inatokana na ukweli kwamba upinzani ulikuwa unategemea makosa ya serikali ili upate ajenda na kujijenga, lakini Mama Samia Suluhu Hassani, punde tu baada ya kuapishwa ni Kama alikuwa analijua hilo. Kwa sasa ndani ya mwaka mmoja na miez kadhaa ameziba mianya yote na kuunyima upinzani ajenda na sera kwa serikali yake, kwa hiyo sasa hivi wapinzani wanashindwa wawaeleze nini wananchi, maana kila kitu kimeguswa na kufanyiwa kazi na Mh. Rais.
Ndio maana unaona wapinzani wengi sana wanamuunga mkono Mh. Rais kwa kazi kubwa anazofanya katika kuijenga nchi yetu. Hakika siasa ni sayansi na mama ameumaliza upinzani kisayansi kwa kufanya kazi wanayohitaji wananchi. Maana wananchi walichokuwa wanahitaji ni mtumishi wao, na kwa sasa Mama Samia Suluhu Hassani amepatikana, hivyo hawana muda tena na habari za vurugu, maandamano, makelele wala matusi kwa serikali.
Mama anaupiga mwingi, ni Mama hadi 2030 hapo ndiyo tutaanza mazungumzo baada ya kufika kituo hicho. Kikubwa ni maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu ili amlinde na kumpigania Mh. Rais wetu, ampatie na kumjalia uzima na afya njema.