Rais Samia Suluhu anakwenda kuzoa kura zote uchaguzi ujao

Rais Samia Suluhu anakwenda kuzoa kura zote uchaguzi ujao

Ndugu zangu wahenga walishasema "nyota njema huonekana asubuhi", kwa kazi nzuri na ya kutukuka anayoifanya Mh. Rais katika kuijenga Tanzania mpya, ni dhahiri uchaguzi ujao utakuwa mwepesi Sana kwake kuweza kupita. Kwa Sasa hakuna mpinzani yeyote mwenye mwelekeo wala nguvu ya kuweza kuja kumtikisa Mh. Rais uchaguzi ujao.

Hii inatokana na ukweli kwamba upinzani ulikuwa unategemea makosa ya serikali ili upate ajenda na kujijenga, lakini Mama Samia Suluhu Hassani, punde tu baada ya kuapishwa ni Kama alikuwa analijua hilo. Kwa sasa ndani ya mwaka mmoja na miez kadhaa ameziba mianya yote na kuunyima upinzani ajenda na sera kwa serikali yake, kwa hiyo sasa hivi wapinzani wanashindwa wawaeleze nini wananchi, maana kila kitu kimeguswa na kufanyiwa kazi na Mh. Rais.

Ndio maana unaona wapinzani wengi sana wanamuunga mkono Mh. Rais kwa kazi kubwa anazofanya katika kuijenga nchi yetu. Hakika siasa ni sayansi na mama ameumaliza upinzani kisayansi kwa kufanya kazi wanayohitaji wananchi. Maana wananchi walichokuwa wanahitaji ni mtumishi wao, na kwa sasa Mama Samia Suluhu Hassani amepatikana, hivyo hawana muda tena na habari za vurugu, maandamano, makelele wala matusi kwa serikali.

Mama anaupiga mwingi, ni Mama hadi 2030 hapo ndiyo tutaanza mazungumzo baada ya kufika kituo hicho. Kikubwa ni maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu ili amlinde na kumpigania Mh. Rais wetu, ampatie na kumjalia uzima na afya njema.
RaisSamia Suluhu hana mpinzani 2025
 
Mh mama Samia suluhu Hassani 2025 usidanganyike kuchukua fomu utaaibika.

CCM viongozi wanakundanganya , CCM wanachama wanakusema vibaya mno.

Sabuni ya Kufulia nguo kipande ni Tsh 1,200 /=
Rais Samia Suluhu hana mpinzani 2025 we ndo unajidanganya wananchi tunamkubali kinyama
 
Hapana ndugu yangu, Naomba uelewe kuwa siyo tume inayokupigia kura, Bali wananchi ndio wanaokupigia kura, utapigiwa kura endapo una Sera na ajenda zinazo gusa maisha ya watu,

Kwa Sasa wapinzani na upinzani umepokwa hoja zote kwa mh Rais kufanyia kazi Kero mbalimbali zinazokuwa zinawatesa wananchi, watu wanaona juhudi za mh Rais katika kuboresha maisha yao, watu wanaona Rais anavyokosa hata muda wa kupumzika ili watanzania wapate maji Safi na salama, Elimu Bora, umeme wa uhakika na Bei nafuu, huduma za Afya zilizo Bora

Sasa utawaambia Nini watanzania juu ya mama Samia wakakuelewa kwa Sasa, utaanzaje kuwakusanya watanzania wamzomee Rais wao ambao kwao Ni mkombozi katika maisha yao

Watanzania wanaona namna mh Rais alivyo msikivu, Namna alivyo na Roho ya huruma Jambo linalomnyima usingizi akiona Kuna watu wanahitaji maji au kituo Cha Afya eneo fulani, Ndio maana unaona anavyopambana kuhakikisha kila Senti inayopatikana inakwenda kupunguza kero kwa wananchi
Aliyeweza utekekezaji na mara nyingine papo hapo ni JPM Hawa wengine wanaendelea na upigaji tu!
Swala maji limekuwa kero kubwa ya Taifa na haitekelezwi
 
Kwa Takwimu hizi hapa unategemea atashindana na nani akamshinda?

Someni wenyewe,hi ni afya tuu bado maji,kilimo,barabara,elimu, biashara nk nk[emoji116]
Nini ya asilimia 5 wakati wengine wako asilimia 80. Hivyo vituo vya afya unavyoongelea hata maji hakuna! Kitanda ya kubebea mgonjwa hakuna. Dawa ndio janga kubwa. Hata umeme hakuna!
Wahufumu Wana majibu Hovyo.
 
Ndugu zangu wahenga walishasema "nyota njema huonekana asubuhi", kwa kazi nzuri na ya kutukuka anayoifanya Mh. Rais katika kuijenga Tanzania mpya, ni dhahiri uchaguzi ujao utakuwa mwepesi Sana kwake kuweza kupita. Kwa Sasa hakuna mpinzani yeyote mwenye mwelekeo wala nguvu ya kuweza kuja kumtikisa Mh. Rais uchaguzi ujao.

Hii inatokana na ukweli kwamba upinzani ulikuwa unategemea makosa ya serikali ili upate ajenda na kujijenga, lakini Mama Samia Suluhu Hassani, punde tu baada ya kuapishwa ni Kama alikuwa analijua hilo. Kwa sasa ndani ya mwaka mmoja na miez kadhaa ameziba mianya yote na kuunyima upinzani ajenda na sera kwa serikali yake, kwa hiyo sasa hivi wapinzani wanashindwa wawaeleze nini wananchi, maana kila kitu kimeguswa na kufanyiwa kazi na Mh. Rais.

Ndio maana unaona wapinzani wengi sana wanamuunga mkono Mh. Rais kwa kazi kubwa anazofanya katika kuijenga nchi yetu. Hakika siasa ni sayansi na mama ameumaliza upinzani kisayansi kwa kufanya kazi wanayohitaji wananchi. Maana wananchi walichokuwa wanahitaji ni mtumishi wao, na kwa sasa Mama Samia Suluhu Hassani amepatikana, hivyo hawana muda tena na habari za vurugu, maandamano, makelele wala matusi kwa serikali.

Mama anaupiga mwingi, ni Mama hadi 2030 hapo ndiyo tutaanza mazungumzo baada ya kufika kituo hicho. Kikubwa ni maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu ili amlinde na kumpigania Mh. Rais wetu, ampatie na kumjalia uzima na afya njema.
Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi vitatoa jibu.
Hii tabia ya kujikomba kwa Viongozi ilichukiwa sana na Baba wa Taifa. Naona Rais SSH anaipenda sana. Nilimsikia alivyojibu wakati wa mahojiano na BBC!
Oh, tunamshukuru sana Samia kwa kutupatia fedha za kujenga Zahanati, wakati pesa hizo tumetoa sisi wenyewe kwenye Tozo, tena sambamba na Kodi nyingine lukuki.
CCM wanajua kuwa hawatakiwi. Ndiyo sababu Katiba Mpya haitakuja wala Tume Huru ya Uchaguzi.
We are in bondage!
 
Wala hujakosea! Kama hakuna marekebisho ya Katiba na Tume ya Uchaguzi atazoa zote.
 
Back
Top Bottom