econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Mama Samia suluhu Hassani hawaogopi wapinzani Bali anawaheshimu Kama ilivyo hulka yake ya kuheshimu kila mtu, Anawaheshimu hata wapinzani kwa kuwa anajuwa kuwa Taifa Hili litajengwa na sisi sote watanzania, lakini pia anaona haipendezi tukajenga Taifa ambalo limegawanyika mapande mapande,
Anataka kuona kuwa kila mtu anajivunia kuwa mtanzania, anataka kuona Kama kikijengwa kituo Cha Afya Basi kila mtu afurahi na kuona kuwa Ni chetu sote, anataka kuona mradi wa maji ukipelekwa mahali fulani unapokelewa na watu wote na kulindwa na watu wote
Anajuwa kuwa ili Hili lifanikiwe hatuna budi kujenga umoja wa kitaifa, anaona kuwa Ni lazima tuheshimiane na kupendana, anaona kuwa Ni lazima Basi ikitokea tunakosoana Basi Tukosoane kwa staha bila kuvunjiana utu wetu, anaona kuwa tunaweza tukaijenga Tanzania Yetu iliyo Bora pamoja na kuwa tunatofautiana katika baadhi ya misimamo yetu ya kisiasa
Ndio maana unaona akitoa fursa ya kuweza kukutana na kufanya mazungumzo na hata viongozi wa vyama vya upinzani ili kuzungumza nao na kukubaliana katika yanayowezekana na kutafuta muafaka katika yanayohitaji mjadala mpana
Anawaheshimu wapi?. Kama angekuwa anawaheshimu angefuta katazo la siasa.