Rais Samia Suluhu anakwenda kuzoa kura zote uchaguzi ujao

Rais Samia Suluhu anakwenda kuzoa kura zote uchaguzi ujao

Ndugu zangu wahenga walishasema "nyota njema huonekana asubuhi", kwa kazi nzuri na ya kutukuka anayoifanya Mh. Rais katika kuijenga Tanzania mpya, ni dhahiri uchaguzi ujao utakuwa mwepesi Sana kwake kuweza kupita. Kwa Sasa hakuna mpinzani yeyote mwenye mwelekeo wala nguvu ya kuweza kuja kumtikisa Mh. Rais uchaguzi ujao.

Hii inatokana na ukweli kwamba upinzani ulikuwa unategemea makosa ya serikali ili upate ajenda na kujijenga, lakini Mama Samia Suluhu Hassani, punde tu baada ya kuapishwa ni Kama alikuwa analijua hilo. Kwa sasa ndani ya mwaka mmoja na miez kadhaa ameziba mianya yote na kuunyima upinzani ajenda na sera kwa serikali yake, kwa hiyo sasa hivi wapinzani wanashindwa wawaeleze nini wananchi, maana kila kitu kimeguswa na kufanyiwa kazi na Mh. Rais.

Ndio maana unaona wapinzani wengi sana wanamuunga mkono Mh. Rais kwa kazi kubwa anazofanya katika kuijenga nchi yetu. Hakika siasa ni sayansi na mama ameumaliza upinzani kisayansi kwa kufanya kazi wanayohitaji wananchi. Maana wananchi walichokuwa wanahitaji ni mtumishi wao, na kwa sasa Mama Samia Suluhu Hassani amepatikana, hivyo hawana muda tena na habari za vurugu, maandamano, makelele wala matusi kwa serikali.

Mama anaupiga mwingi, ni Mama hadi 2030 hapo ndiyo tutaanza mazungumzo baada ya kufika kituo hicho. Kikubwa ni maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu ili amlinde na kumpigania Mh. Rais wetu, ampatie na kumjalia uzima na afya njema.
Mnatumwa mje JF ku TEST nguvu ya mama,sio?
 
ni mapema mno kusema hayo. yako mambo ya kuweka sawa na ujue pia wako wanaolaumu na wengi ni ccm waoiga kura
 
Kwani Tanzania tumepata Uhuru Jana?. Unaongea as if serikali zingine hazikufanya hayo na bado zilipata shida kwenye uchaguzi Hadi kuiba.

Mama aombe sana wafuasi wa Magufuli na wafuasi wa chadema wasiungane la sivyo atapata tabu Sana.
Hakuna wafuasi wa Hayati Magufuli Bali Kuna CCM iliyo moja tu, kwa hiyo acha hizo ndoto za kuomba CCM igawanyike, CCM Ni moja na wanaccm Ni wa moja, na kikubwa ni kuwa Hakuna aliye mkubwa kuliko CCM , Ndani ya CCM kila mtu ana haki sawa
 
Sina cheo chochote Ila nimeridhishwa na utendaji kazi uliotukuka wa mh Rais uliotuheshimisha watanzania, kwa Sasa ndio maana unaona hata mafuriko ya watalii yanavyoendelea kumiminika hapa nchini, hayo Ni matunda ya Royal Tour na uimarishwaji wa diplomasia uliofanywa na mh Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan

Wewe ni chawa. Unawatumia wannchi kwa matamanio yako
 
Hakuna wafuasi wa Hayati Magufuli Bali Kuna CCM iliyo moja tu, kwa hiyo acha hizo ndoto za kuomba CCM igawanyike, CCM Ni moja na wanaccm Ni wa moja, na kikubwa ni kuwa Hakuna aliye mkubwa kuliko CCM , Ndani ya CCM kila mtu ana haki sawa

Ondoa ujinga wako. Mimi naonhelea wafuasi sio wanachama. 2015 Magufuli alipata kura nyingi sio kwa sababu ni CCM Ni kwa sababu ya utendaji wake . Wewe Baki hapo na uccm wako utashangaa.
 
Yah right. Provided that atafanya kama alivyofanya Mwendazake kwa msaada wa Mahera na team yake .....!!
Hata wapinzani wapewe nafasi yakuwa na wajumbe kutoka kamati kui yao kuwa katika tume ya uchaguzi bado hawawezi kumtikisa mh Rais, maana wanaopiga kura Ni wananchi na wananchi ndio hao ambao kwa Sasa wanamuunga mkono mh Rais
 
Mimi mwenyewe Ni miongoni mwa wananchi tunaomuunga mkono mh Rais kwa kazi kubwa anayoifanya

Ndio maana nikasema unawatumia Wanachi Kama ngazi ya kufanikisha uchawa wako. Unaongelea 2025 wakati bado kazi haijafanyika. Madarasa na barabara zimejengwa tangu awamu ya kwanza, Samia sio wa kwanza. Shughulika Bei ya vitu, vifaa vya ujenzi, ajira, mitaji benki nk.

Punguza kusifia Mambo ambayo ni obvious. Shughulika na Mambo yanayogusa .
 
Ondoa ujinga wako. Mimi naonhelea wafuasi sio wanachama. 2015 Magufuli alipata kura nyingi sio kwa sababu ni CCM Ni kwa sababu ya utendaji wake . Wewe Baki hapo na uccm wako utashangaa.
Hata Sasa utendaji kazi wa mh Rais mama Samia suluhu Ndio unaombeba na kumuweka katika vinywa vya watanzania muda wote, Ambapo wanamuongelea namna utendaji na uchapa kazi wake unavyowaridhisha na kutoa matumaini, wanafurahishwa pia na namna anavyoendesha nchi kwa kuzingatia misingi ya Sheria na utawala bora
 
Ndugu zangu wahenga walishasema "nyota njema huonekana asubuhi", kwa kazi nzuri na ya kutukuka anayoifanya Mh. Rais katika kuijenga Tanzania mpya, ni dhahiri uchaguzi ujao utakuwa mwepesi Sana kwake kuweza kupita. Kwa Sasa hakuna mpinzani yeyote mwenye mwelekeo wala nguvu ya kuweza kuja kumtikisa Mh. Rais uchaguzi ujao.

Hii inatokana na ukweli kwamba upinzani ulikuwa unategemea makosa ya serikali ili upate ajenda na kujijenga, lakini Mama Samia Suluhu Hassani, punde tu baada ya kuapishwa ni Kama alikuwa analijua hilo. Kwa sasa ndani ya mwaka mmoja na miez kadhaa ameziba mianya yote na kuunyima upinzani ajenda na sera kwa serikali yake, kwa hiyo sasa hivi wapinzani wanashindwa wawaeleze nini wananchi, maana kila kitu kimeguswa na kufanyiwa kazi na Mh. Rais.

Ndio maana unaona wapinzani wengi sana wanamuunga mkono Mh. Rais kwa kazi kubwa anazofanya katika kuijenga nchi yetu. Hakika siasa ni sayansi na mama ameumaliza upinzani kisayansi kwa kufanya kazi wanayohitaji wananchi. Maana wananchi walichokuwa wanahitaji ni mtumishi wao, na kwa sasa Mama Samia Suluhu Hassani amepatikana, hivyo hawana muda tena na habari za vurugu, maandamano, makelele wala matusi kwa serikali.

Mama anaupiga mwingi, ni Mama hadi 2030 hapo ndiyo tutaanza mazungumzo baada ya kufika kituo hicho. Kikubwa ni maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu ili amlinde na kumpigania Mh. Rais wetu, ampatie na kumjalia uzima na afya njema.
Ngoja kwanza nicheke!
20220816_083220.jpg
 
Hata wapinzani wapewe nafasi yakuwa na wajumbe kutoka kamati kui yao kuwa katika tume ya uchaguzi bado hawawezi kumtikisa mh Rais, maana wanaopiga kura Ni wananchi na wananchi ndio hao ambao kwa Sasa wanamuunga mkono mh Rais

Jisemee mwenyewe acha kuongelea wananchi kana kwamba unawajua wote. Jana kuna mtanzania kataka kujiua kwenye stendi ya mabasi msamvu kisa ugumu wa maisha. Halafu wewe chawa unasema kila mwananchi ameridhika.
 
Hata Sasa utendaji kazi wa mh Rais mama Samia suluhu Ndio unaombeba na kumuweka katika vinywa vya watanzania muda wote, Ambapo wanamuongelea namna utendaji na uchapa kazi wake unavyowaridhisha na kutoa matumaini, wanafurahishwa pia na namna anavyoendesha nchi kwa kuzingatia misingi ya Sheria na utawala bora

Ndio maana nikasema ajitahidi awezavyo wafuasi wa Magufuli na chadema wasije kuungana waendelee kuwa maadui Kama Sasa hivi. Maana akiboronga itafika kipindi atawakutanisha wafuasi wa Magufuli na Chadema.
 
B
Ndio maana nikasema unawatumia Wanachi Kama ngazi ya kufanikisha uchawa wako. Unaongelea 2025 wakati bado kazi haijafanyika. Madarasa na barabara zimejengwa tangu awamu ya kwanza, Samia sio wa kwanza. Shughulika Bei ya vitu, vifaa vya ujenzi, ajira, mitaji benki nk.

Punguza kusifia Mambo ambayo ni obvious. Shughulika na Mambo yanayogusa .
Bei ya vitu pia mama anashugulika na suala Hilo ndio maana unaona kwa Sasa anatoa billioni Mia moja Kama Ruzuku kwenye mafuta, anafanya hivi kwa kutambua kuwa mafuta Ni injini ya uchumi kwa kuwa yakipanda Sana kila kitu lazima kitapanda, Hali ikitengemaa katika soko la Dunia Basi utaona yakianza kurejea Kama zamani, lakini kwa Sasa ili kumsaidia mwananchi Ndio unaona hatua hizo alizochukua

Pia hata katika kilimo ametoa billioni Mia moja hamsini Kama Ruzuku,Jambo ambalo litapelekea mbolea kuuzwa elfu70 kutoka huko kwa laki na 40, hii itamsaidia mkulima kumudu Bei ukilinganisha na msimu uliopita, pia Hali hii itaongeza na kuchochea uzalisha na kuendana na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema kilimo Ni biashara

Kuhusu suala la ajira Nazani Basi hufuatilii Mambo yanavyokwenda, maana tangia mama ameingia madarakani Kama Rais amekuwa akitoa nafasi za ajira, mf majuzi juzi tu hapo akitoa ajira za kada nyingi Sana kuanzia Elimu,Afya,kilimo,Sheria,n,k Jambo lililo wapi nafasi baadhi ya vijana walio kuwa mitaani kwenda kulitumikia Taifa kwa kuwahudumia wananchi
 
Ndio maana nikasema ajitahidi awezavyo wafuasi wa Magufuli na chadema wasije kuungana waendelee kuwa maadui Kama Sasa hivi. Maana akiboronga itafika kipindi atawakutanisha wafuasi wa Magufuli na Chadema.
Ndio mh Rais wetu anaendelea kujitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuwatumikia watanzania, mama Ana kiu ya kuona kila mwananchi anainuka kiuchumi, mama anakiu ya kuona kuwa hakuna mwananchi anayeachwa nyuma kimaendeleo, mama anakiu ya kuona kuwa Rasilimali hizi nyingi tulizo nazo zinakuwa baraka kwa watanzania, mama anakiu ya kuona kuwa watanzania hawanywi maji machafu ilihali tuna vyanzo vingi vya maji, mama Ana kiu ya kuona hakuna mtoto Anaye kaa chini darasani wakati tuna misitu mingi tu ya mbao, mama anakiu ya kuona hakuna mama mjamzito anaejifungulia chini kwa kukosa kitanda, Tumuunge mkono mh Rais na tutoe ushauri tunapoona panafaa maana Naye Ni mwanadamu
 
Hata Mwenyekiti wa Tume awe Mbowe,mgombea awe Lisu na IGP awe Kigaila Benson bado Samia atashinda saa 3 asubuhi 👇

Acha kujifurahisha. Lini IGP anateuliwa kutoka kwa wananchi. Pia Ili uwe Mwenyekiti wa NEC lazima uwe na sifa za kuwa jaji.
 
Naomba uwe mwelewa. Ajira zinatengenezwa sio nafasi za kazi serikalini. Magufuli alitengeneza ajira kiasi kwa kujenga miundo mbinu nchi nzima. Mama Angekuja na akili mpya ya namna ya kutengeneza ajira.
 
Mh mama Samia suluhu Hassani 2025 usidanganyike kuchukua fomu utaaibika.

CCM viongozi wanakundanganya , CCM wanachama wanakusema vibaya mno.

Sabuni ya Kufulia nguo kipande ni Tsh 1,200 /=
Hatuna mashaka na mama katufanyia mambo mengi mazuri yani 2025 hakutakua na wakupinga kwa hii kazi ya maendeleo
 
Hata wapinzani wapewe nafasi ya kupiga kampenii peke yao bado mh mama Samia suluhu Hassani atapitaa kwa kishindo

Punguza dhihaka. Mama mwenyewe anawaogopa upinzani ndio maana amekataa wasifanye mikutano ya siasa. Wafuasi wa upinzani Tanzania ni wengi kuliko ccm. Sema system hairuhusu kufurahia Uhuru wa vyama vya upinzani ndio maana wengi wanajificha.
 
Back
Top Bottom