Rais Samia Suluhu aongeza bajeti kwa asilimia 230 Ujenzi wa JN-HPP

Rais Samia Suluhu aongeza bajeti kwa asilimia 230 Ujenzi wa JN-HPP

kwanza watujibu ile mifuniko ndo imeshindikana kupachikwa mahala pake!!?,au hiyo mihela ndo yakuagiza huo mu winch wa kupachikia hiyo mifuniko!!?,

Tuwakumbushe tu,wasivimbiwe wajipimie!!
Nadharia tu
 

Ujenzi wa bwawa la JNHPP pamoja na Usambazaji wa umeme vijijini Rais Samia ameongeza bajeti kwa 230% kutoka TZS 1.01T FY2020|21 hadi TZS 2.34T FY2021|22,


" Hakuna kama Samia "


Lengo la Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ifikapo mwaka 2026 Tanzania iwe na umeme wa Uhakika unaofikia Jumla ya 5,000MW hapa anamaanisha tunakwenda kuwa electricity donor country hakika Watanzania kesho yetu ni bora sana kuliko leo,
===
Sote tunafahamu mahitaji ya Umeme Tanzania yanaongezeka siku hata siku kwa mfano mwaka 2020 mahitaji ya Umeme yalikuwa 1,151.66MW lakini hadi kufikia mwezi mei 2021 mahitaji ya Umeme yalifikia 1,183.28MW sawa na ongezeko la 3% kwa mwaka.

===
Lakini pia, kwa mwaka huku umeme wetu umetajwa kuwa ndio umeme wenye bei chee zaidi African ya Mashariki kwani tunauuza kwa $0.099/KWh,Kwahakika Tanzania ya Rais Samia ni raha natutegemee bei hii kushuka zaidi baada ya JNHPP kukamilika na kuanza kufanya kazi,
===
Faida ya mradi huu sio umeme tu hata utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020|25 ya kuzalisha ajira 8M ifikapo 2025 kwani tayari mradi huu umeajiri Jumla ya wafanyakazi 7,243 wazawa wakiwa ni 6,452 na wageni ni 791,Mradi huu utakapokamilika unatarajiwa kuzalisha Jumla ya MW 2,115 kamwe tusiache kumwomba Mungu,
===
Mpaka Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani ni 38% tu ya fedha zote za mradi huu wa Tshs 6.55trilioni ndio zilikuwa zimelipwa kwa mkandarasi ambayo Jumla yake ni Tshs 2.495trilioni sawa na Pungufu ya Tshs 4.055trilioni,

===
Hii ni sawa na kusema Rais Samia Suluhu Hassan hadi mwisho wa mradi huu atakuwa ameujenga mradi kwa zaidi ya 62%,Hakika Mama huyu anastahili pongezi sana kwa kiwango hiki cha kizalendo kwa nchi yake,
===
Zikiwa zimesalia miezi kumi ( 10 ) tu kumalizika kwa mkataba huu Rais Samia Suluhu Hassan kupitia bajeti yake hii ya kwanza tayari ameshatenga 58% ya deni lote lililosalia kwani ametoa Tshs 2.34trilioni kwaajili ya usambazaji wa umeme na ukamilishaji wa mradi huu wa JNHPP,

===
Pesa hii ni sawa na pesa yote iliyotolewa tangu kuanza kwa mradi huu wa JNHPP, Unaweza kusema "Bajeti moja ya Rais Samia kwenye usambazaji wa umeme na ujenzi wa JNHPP ni sawa na bajeti zote zilizotolewa kujenga JNHPP tangu ianze Mei 2019 " Watanzania,Kama kuna mtu wa kuombewa kwa nguvu kubwa kwa sasa basi ni Rais Samia Suluhu Hassan.



|
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN YUKO BEGA KWA BEGA NA VIONGOZI WALIOMTANGULIA|

Naanza kusoma
a,e,i,o,u
Nakumbuka wakati gesi story zinaanza tuliambiwa itasababisha kuwa mzalishaji wa dawa za binadamu na mbolea mkubwa kwa Afrika nzima,leo hii tunaambiwa gesi ilishabebwa na mabeberu
 
Naanza kusoma
a,e,i,o,u
Nakumbuka wakati gesi story zinaanza tuliambiwa itasababisha kuwa mzalishaji wa dawa za binadamu na mbolea mkubwa kwa Afrika nzima,leo hii tunaambiwa gesi ilishabebwa na mabeberu
Gesi gani imebebwa na mabeberu?
 
Uzalendo huwa unagusia nyanja zote za nchi, ukiona hicho unachosema uzalendo unaegemea upande mmoja huo siyo bali ni kitu kingine kabisa hata sijui kinaitwaje!.

Unataka kusema nikiwa namzunguzia babu yangu tuu kwa mambo yote kuwa pasipo yeye was nothing, then unasahau kuwa pasipo baba yake na huyo babu unayemsifia also nothing was existed.

Huyo mzalendo anazungumzia raia wanaouliwa na polisi au polisi wanaouliwa na raia?.

👉🏾 Tufuatilie kwa pamoja.
Mkuu tafuta pesa, Samia anafanya vizuri,
 
CM 1774858

Binafsi nikushukuru sana kuwafumbua macho hasa waliokata tamaa baada ya kifo cha Rais Magufuli ,

Samia anafanya vizuri sana ila kwa njia tofauti lazima wamuamini mama yuko vizuri sana na analeta matokeo kwa haraka sana,

Kwakasi ile ya 38% miaka miwili huenda tungekwama,
Sahihi sana,
 
Huu mradi ulikuwa mgumu kuanza kule! Mtu kama Samia na the way anawaangalia wale mabepali asingeweza kuufanya! Ata angekuta ndo atafutwa mkandarasi asingeweza kuendeleanao.

Hata akiongeza she is not going to get value for the money kwasababu wameishajua kuwa hana weledi [ no close supervision of the project payments] hivyo watamuongopea na kuongeza gharama za mradi na bado hautakamilika vizuri!! Makamu wake anajua kinachoendelea lakini hasemi because somehow he is conflicted!!
 
Back
Top Bottom