Rais Samia Suluhu ateua Wabunge wapya watatu na kuteua Baraza la Mawaziri

Tofauti ya bashiru na mzee halima ni nini katika nafasi zao za ubunge wa kuteuliwa!
 
Kilicho nifurahisha zaidi katika mabadiliko aliyo yafanya Mhe. Rais ni;

Kupanga safu za mawaziri kulingana na "professional" zao, hakika hili litaongeza sana ufanisi ktk wizara husika.
reshuffle aliyo ifanya imelenga kuongeza ufanisi zaidi na kuleta tija.
 
Najua hilo Mkuu la kuhusu pesa inayodaiwa kuchotwa pale BoT 300 billions za ''Matibabu ya mgonjwa''
Kuna uchunguzi unaoendelea kati ya BOT na Hazina na yeye ndio yuko katikati ya huo uchunguzi hivyo asingeweza ondolewa, hata hivyo nadhani it is a question of time before hao makatibu wakuu nao wakabadilishwa.
 
Mzee Mangulla alilazwa hospitali halafu unasema ni uongo, wewe una akili nzuli kweli? Naona una mwezi mchanga!
Du umekunywa komoni ukalewa nini? Kwani wanaolazwa hospital wote wamenyweshwa sumu? Mbona unajiweka low namna hii?
 
I second!
Nimewaza kama wewe,wasingeweza kufanya vitu kila mtu ajue wanaelekea wapi
Confusion is necessary in leadership,by the time watu wanakuelewa unakua ushapata utakalo
 
..mtoa hoja analaumu uteuzi wa Dr.Mwigulu[ mvaa skafu] kuwa waziri wa fedha.

PALE MAMA KASHAURIWA VIBAYA. YOU NEED A SOBER PERSON KAMA PROF. MKENDA. MWIGULLU HAWEZI KUENDANA NA HAO WANAOITWA WAHISANI!! HE IS CRUDE WITH NO ETIQUETTE . ANGEFAA PENGINE KWENYE WIZARA YA UTAMADUNI LAKINI SIO FEDHA!!!
 
Kuna siku zitamdondoka ofisini hapo ndiyo itakuwa mshike mshike.
Hahaha... Tusubiri majibu atakayokuwa anatoa bungeni, labda mwendazake alimharibu reasoning yake akawa anacheza kufuata midundo yake
 
Ni ajabu miskafu kupewa hii wizara!
 
Nimeamini leo kuwa cheo nidhamana,unaweza kupanda kama unapanda mnazi vilevile kushuka kwake yaani faster!
 
Huyu kashajiharibia mwenyewe kabla hata kazi haijaanza.

Mwigulu hawezi kuwa na msaada wowote kwake ni heri angetafuta mtu nje ya bunge kama hakukuwa na mtu mwingine mwenye sifa za kushika hiyo ofisi.
Pamoja na kwamba simpendi wala simkubali Mwigulu, Ila kama akiamua kufanya kazi kwa kutumia weledi na elimu yake basi sina shaka nae..

Mwigulu tofauti na vijana wengine wa CCM (Makamba, Nape, Ridhione, Kigwa) ambao wanategemea nyadhifa za Baba zao na majina ya Baba zao, Mwigulu yeye ni kichwa, Mwigulu hana elimu ya kuunga unga kama hao wengine hapo. Mwigulu pamoja na kujipendekeza kusikovumilika ila kichwani yupo vizuri na kapiga shule.

Mwigulu anatakiwa tu aache au apunguze roho mbaya, kujikweza na kujiona yeye anajua kila kitu. Mwigulu ajaribu kuvaa charisma ya Mpango, na kwa elimu yake basi atafika mbali sana huko mbeleni.

Pole Makamba, Nape na kikundi chenu cha mitandaoni.. Ndoto za Urais 2025/35 ndio zimeyeyuka hivo
 
Kwa nini vyeo nyeti vyenye maslahi mapana sana kwa nchi vitumike kushikana mashati?
Kuna vyeo vyengine ni kutafutiana kushikana mashati..[emoji1787]
 
Dr. Mwigulu ni mtu sahihi sana kwa uchumi wetu hata nafasi ya Urais anafaa kwa wakati ujao; Tatizo vijana wengi hapa jukwaani na mitaani huwa hamfahamu hulka na historia ya vijana wetu hawa wenye uwezo kama Kijana Mwigulu. Pia, msitumie mihemko kutoa maoni yenu.
Mhe. Dr. Mwigulu, nakutakia kila la kheri.
 
Ni mule mule Mule Wadaganyika msitegemee Jpya...Ni Wale wale Waliotitesa miaka 5.5 ..Daaaah! Mungu hata haujatukomboa toka kwa watesi wetu...Mungu inaonekana hawajajua wewe ndio Mungu...Ebu basi fanya na tuseme YES...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…