Rais Samia Suluhu ateua Wabunge wapya watatu na kuteua Baraza la Mawaziri

Rais Samia Suluhu ateua Wabunge wapya watatu na kuteua Baraza la Mawaziri

C.V na uzoefu pamoja pia ubobezi wa Balozi Dr. Liberata Rutageruka Mulamula, ikilinganishwa na ya Prof. Palamagamba Kabudi tunawaachia wana great thinkers wa JamiiForums mjadili.
CV ya huyu mama ni nzuri kuwa waziri wa Mambo ya nje na ni mzoefu kuliko le profeseri wa mia kenda
 
Mwigulu ni mbobezi wa uchumi na mambo ya Fedha. Mimi nashangaa mnaosema hafit. That guy is so competent

Hata Dr Bilal naye alikuwa mtaalam wa makinikia,miamba,milipuko,nuclear lakini hakuna kipya tulichokiona kwake,tofautisha madesa na uhalisia ,mwigulu ni mtu wa madesa,hana experience ya kutosha kuwa waziri wa fedha,wengi waliokuwa kwenye hizo nafasi walikuwa picked kwenye taasisi kubwa za fedha ,wengi walikuwa IMF,WB etc.
 
limevunjwa wapi? hivi akili huwa mnaweka wapi?

kasema anafanya mabadiliko baada ya kumtoa mpango....

katiba ulivyoandikiwa na TLS na CDM ulidanganywa...kale malimau

Hao waliapa kwa rais kama taasisi na sio mtu, ebo!!!
Asipokuelewa, pls NITAGI 🙂 nimsomeshe zaidi 🙂
 
Aisee hapa naona mama kama kateleza Mwigulu wizara ya Fedha? mbona simuamini!
Mwigulu mm naamini hana tatizo saana,ila alibadilishwa tabia na mwenda zake.

Mwigulu ni mvumilivu,alichapa kazi wizara ya mifugo vizuri,ilikua likitokea tatizo tu kafika eneo la tukio.
Nyota yake iliwaka vzr kwa wananchi ,ila mwenda zake kwa hila zake za kuhofia kua yupo na timu ile iliomuita mshamba akamnyang'anya gari njiani kwa kumdhalilisha.
Lakini alivumilia na mwisho tumeona kamrudisha tena.

Nafikili kuna watu wanaChuki tu za ujana.
 
Mama kaniharibia Sana ule utamu wa kuniletea Katanga! Mwigulu, Jaffo na Kabudi wa kazi gani Tena? Na kule afya mbona umewaacha wale comedians? Mama hebu funga macho utafakari kwa kina juu ya hao pamoja na pm na ikikupendeza piga chini hao uanze upya na timu mpya yenye ueledi na adabu ya kazi wasioiwazia nafasi yako ya urais mwaka 2025!
Kwani ulidhani atamteua Mbowe?
Umesahau kwamba Samia ni CCM wa kugalagala?
 
Balozi wa nini mkuu?? Sio ameteuliwa kua mbunge nadhani ni zile nafasi 10 alizonazo mh. SSH kama raisi.
Daah ila kutoka katibu kiongozi mpaka ubunge cheo sawa na babu tale 😂😂😂
tena mbunge asie na jimbo upo upo tu ...
Bashiru kapewa ubunge ili aendelee kuwa katibu mkuu wa ccm....
Mbunge ana pato la hadi 11m kwa mwezi, unadiriki vipi kumuita mtu kama huyu eti yupo yupo tu....

Wewe wa laki 7 kwa mwezi ndo utakuaje?
 
Huyu Mama Ana Kusudi Sana Nadhani Hataki Kufanya Kazi Na Mwalimu Wangu Bashiru, Kamteua Kuwa Mbunge Halafu Kamwacha Domant Tu.. Daaaah Dharau Hizi.
Hiyo kwa kizungu inaitwa Horizontal drop...!!
 
Wabunge wapya walioteuliwa kuwa wabunge ni pamoja na Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Bashiru Kakurwa Ali, Mbarouk Nassor Mbarouk na Liberata Mulamula.

Rais Samia Suluhu akitangaza Baraza la Mawaziri amesema...

''Kuondoka kwa Mpango kumefanya nifanye mabadiliko kidogo kwenye Baraza la Mawaziri na nitatangaza hapahapa, zege halilali''

Baadhi ya Wizara zimefanyiwa Mabadiliko na nyingine zimebaki kama zilivyokuwa.

MAJINA YA MAWAZIRI WANAOUNDA BARAZA LA MAWAZIRI

Ummy Mwalimu - Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI

Mohammed Mchengelwa - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Selemani Jafo - Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais

Geoffrey Mwambe - Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji

Dkt. Mwigulu Nchemba - Waziri wa Fedha na Mipango

Profesa Palamagamba Kabudi - Waziri Wizara ya Katiba na Sheria

Balozi Liberata Mulamula - Waziri wa Mambo ya Nje

Prof Kitila Mkumbo - Waziri wa Viwanda na Biashara
Duh,
Sasa Bashiru ubalozi wake nao umetenguliwa?
 
Back
Top Bottom