Rais Samia Suluhu ateua Wabunge wapya watatu na kuteua Baraza la Mawaziri

Rais Samia Suluhu ateua Wabunge wapya watatu na kuteua Baraza la Mawaziri

Ayo mabadiliko uliyosema wewe ni ya serikali.
Ila kwenye U-team bado wapo vilevile,team zote zipo na wachezaji wakiwa full ngwamba.
Haya ni mawazo ya u-team ni ya wale wa ushindani wa makundi makundi. Huko mm sipo boss.

Kilichopo ni kwamba sasa ilani ya chama inaongozwa na binadamu tofauti na aliyekuwepo ghafla na binadamu hatufanani kiutendaji japo ilani ni ile ile ila mtindo hautakuwa sawa.
 
Bashiru kapewa ubunge ili aendelee kuwa katibu mkuu wa ccm....
Mbunge ana pato la hadi 11m kwa mwezi, unadiriki vipi kumuita mtu kama huyu eti yupo yupo tu....

Wewe wa laki 7 kwa mwezi ndo utakuaje?
Mkuu kinachoongelewa hapo sio mshahara anaopokea bali ni cheo alichokua nacho/navyo na hiki alichonacho sasa. Hata asingepewa huo ubunge bado simfikii kwa ukwasi alionao.

Kwahiyo usilete hoja zako za mishahara yake anayopokea kama pesa anayo yule anachotafuta hapo ni vyeo. Namna gani wewe mkuu yaani unadhani watu wanamdhihaki Bashiru kisa mshahara umepungua?? Jiongeze basii
 
Jafo ata kula bata sasa maana TAMISEMI inaonekana ni Mshipa mkubwaa kuutafuna nahisi ule ungemfaa mzee Aggrey Mwanri
Hii wizara ya TAMISEMI ni kubwa mno, kwa ukubwa wake kuiongoza ni ngumu sana, inatakiwa igawanywe na kupunguziwa baadhi ya majukumu. Mfano, masuala ya Elimu yangeoelekwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na masuala ya Afya yangepelekwa Wizara ya Afya.

Vv
 
Huyu Mama Ana Kusudi Sana Nadhani Hataki Kufanya Kazi Na Mwalimu Wangu Bashiru, Kamteua Kuwa Mbunge Halafu Kamwacha Domant Tu.. Daaaah Dharau Hizi.

Influence ya Kikwete hiyo. Samia must be every careful how he handles Kikwete's advice!! Next atamshauri ambadilishe Mzee Mangulla kule ccm kama Makamu wa Mwenyekiti na huo ndio itakuwa mwanzo na mwisho wake; hakuna mtu anaimudu ccm kama yule mzee na akiondoka tu mtayumba!! Huyo mzee anafanya hayo majukumu kutokana na uzalendo wake basi. Sasa mafisadi wanaona anawawekea kiwingu na ndio maana wanamlisha hata sumu lakini Imani yake inamponya!!

Nimeshangaa sana Rais Samia katika hotuba yake ya kumpongeza Mpango hakutambua uwepo wa makamu wa Mwenyekiti wa ccm Mangulla ingawa alikuwepo!!!!
 
Wabunge wapya walioteuliwa kuwa wabunge ni pamoja na Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Bashiru Kakurwa Ali, Mbarouk Nassor Mbarouk na Liberata Mulamula.

Rais Samia Suluhu akitangaza Baraza la Mawaziri amesema...

''Kuondoka kwa Mpango kumefanya nifanye mabadiliko kidogo kwenye Baraza la Mawaziri na nitatangaza hapahapa, zege halilali''

Baadhi ya Wizara zimefanyiwa Mabadiliko na nyingine zimebaki kama zilivyokuwa.

MAJINA YA MAWAZIRI WANAOUNDA BARAZA LA MAWAZIRI

Ummy Mwalimu - Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI

Mohammed Mchengelwa - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Selemani Jafo - Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais

Geoffrey Mwambe - Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji

Dkt. Mwigulu Nchemba - Waziri wa Fedha na Mipango

Profesa Palamagamba Kabudi - Waziri Wizara ya Katiba na Sheria

Balozi Liberata Mulamula - Waziri wa Mambo ya Nje

Prof Kitila Mkumbo - Waziri wa Viwanda na Biashara

Mkuu Copenhagen DN naona ni zamu yenu kufaidi Hongereni. Sisi waislamu tunawaangalia tu.
 
Back
Top Bottom