Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wa mabalozi; wamo Hoyce Temu na Togolani Mavura

Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wa mabalozi; wamo Hoyce Temu na Togolani Mavura

Daaah, nimefurahi sana kwasababu kwenye hii orodha kuna watu wengi walikuwa pale Foreign Affairs kama wamesahaulika yani. Wengi waliopata teuzi wana ufahamu mzuri na masuala ya diplomasia, utawala, biashara na ulinzi. Naona Liberata amekumbuka watu wa wizara yake: Hivi ndivyo inatakiwa iwe.....
Nimewaona waliwekwa bench awamu iliopita,mbaya zaidi walikuwa vijana it's frustrating. Kuna mmoja atafika mbali sana siku ikifika nitakukumbusha.
 
Huyu mama Liberatha ni mtu mmoja smart sana. Niliposikia tu amekuwa waziri nikaanza kusoma mahojiano yake huko Google na taasisi za kimataifa. She's very smart upstairs.
 
Usilazimishe connection mkuu. Mimi kuna mtoto mmoja wa kigogo alikuwa rafiki yangu, I was treating her well, ila akadhani labda ninajitengenezea mazingira ya connection, nilimchana live nikamwambia mimi sina njaa kali kama unavyonidhania.

Nilichokuja kugundua, kujenga connection kunahitaji uvumilivu sana. Faida zake huwa ziko long term sana. Mara nyingi uwe tayari kutumika ili kustawisha mahusiano.

Ni kweli kuna wengine wanaweza kutaka kuku abuse au kukuchukulia poa kwa sababu wanadhani au kujiona unawahitaji wao kuliko wao wanavyokuhitaji wewe.
 
Nimewaona waliwekwa bench awamu iliopita,mbaya zaidi walikuwa vijana it's frustrating. Kuna mmoja atafika mbali sana siku ikifika nitakukumbusha.
Daaah, noma sana mazee tena walianza kugongwa benchi baada ya Liberata kutimuliwa kipindi kile.
Walijifanya wanafanya kijisherehe cha kumuaga Jasusi Mbobezi, kumbe kuna mtu hapendi......
 
Nilichokuja kugundua, kujenga connection kunahitaji uvumilivu sana. Faida zake huwa ziko long term sana. Mara nyingi uwe tayari kutumika ili kustawisha mahusiano.
Hii ngumu sana kwangu mkuu. Nitagombana naye waingereza wanasema "on spot"
 
Hivi kuteuliwa serikalini kibongo bongo ni dili eh?

Kweli mentality zipo tofauti sana.

Wakati baadhi yetu hatutaki kabisa kufanya kazi serikalini, wengine wanaona kufanya kazi serikalini ni zali!

Ndo maana mara nyingi wengine huwa hatuelewani kabisa humu!

I mean…ubalozi nao ni dili? 🤣
Mtu kuwa kiongozi Bongo ni kama kuwa mungu mtu. Nafasi za uongozi zinachukuliwa kama sehemu ya kujineemesha na kuwa mamlaka ya kutenda upendavyo. Ile dhana ya ya kuwa uongozi ni utumishi kwa watu haipo kabisa. Ndiyo maana watu wakipata nafasi ya uongozi wako radhi hata kujilidhalilisha ili tu wapendwe na aliyewateua. Kipindi cha nyuma kuna wakati China ilisema Afrika iko nyuma kwa sababu aina ya demokrasia inayofuatwa Afrika haiendeni na mazingira yake. Kuna ukweli fulani kwenye hili.
 
Back
Top Bottom