Rais Samia Suluhu Hassan akutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi

Rais Samia Suluhu Hassan akutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi

Picha namba 1-2. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alifika kumsalimia Rais Samia Nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Aprili, 2021​

Picha namba 3. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alifika kumsalimia Rais Samia Nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Aprili, 2021.

Picha namba 5. Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akizungumza na Wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Aprili, 2021. PICHA NA IKULU.

3.jpg


5.jpg


1.jpg


2.jpg
 
Huyu mzee 'alimsifia' pia JPM; labda anamshawishi awe 'mama ruksa'!
 
Hamna Mtanzania asiye taka kumuunga mkono Mh Rais, tatizo ni pale anaposhindwa kujipambanunua kuwa alikuwa msaidizi namba moja wa mwendazake. Wakati mwendazake ana chakufuliwa kakaa kimya kama hayuko na hasikii au anafurahia kimoyomoyo?! Ukweli ni kuwa Magufuli hawezi kuchafuliwa na walio tumikia naye wakafikiri watabaki salama. Spika anaona atabaki salama kwa kusema mwendazake alishauriwa vibaya ana sahau anayo skandali ya mabilioni ya matibabu ambayo ilikuwa ina hang somewhere ni suala la muda tu. Wakimaliza hii biashara yao kichaa ya kumpaka oil chafu mwendazake watamgeukia hili halihitaji akili kubwa kulijua. Alishauriwa na nani zaidi ya nyie mlio kuwa mnamzunguka na kufanyakazi pamoja naye?

Mbona Judge Mkuu hatumsikii akiendekeza haya mambo ya kusikitisha na kutaharisha yanayo endelea kwa sasa hapa Tanzania. Huyu amekuwa kiongozi mweledi siku zote. Hotuba aliyoitoa siku ya maziko pale Chato ni kielelezo tosha cha kiongozi mwenye hekima.

Wazee wamshauri huyu ahamie mhimili wa Excutive ifikapo 2025 atawafaa sana Watanzania/Tanganyika.

Nilijua tuu pumba kama hizi haziwezi kukosekana.

Mama hawezi kua mrithi wa Maujinga ya Marehemu. Alishasema historia inakufuata kokote uendako hata kaburini historia yako itakufuata tuu.

Nae anazo taratibu zake za namna ya kuongoza na sio kumtetea marehemu mwenda zake.

Au nasema uongo ndugu zangu
 
Back
Top Bottom