Rais Samia Suluhu Hassan akutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi

Rais Samia Suluhu Hassan akutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi

Amefika kumsalimia Rais Samia nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.Hivi Mh Rais Samia Bado hajahamia Ikulu rasmi kimakazi?.
 
Mzee Mwinyi anatakiwa asamehewe bure popote atakapotereza, kwa umri aliokua nao wazee wengi huwa akili zinaruka kidogo na kurudi utotoni.

Mungu amlinde na amuongoze. Taifa hili wasingekuwepo Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa, nchi ingegawanywa na MATAGA katika vikao vyao vya CCM (Wee Bashilu, chukua mkoa wa bukoba utakuwa wako, na wee nanii, nanii, eenh Hapi chukua mkoa wa ilinga utakua shamba lako - Mtaandika maombi ya kuomba hati muyalete ofisini kwa Lukuvi, mimi ndio laisi wa nchi, ntawapa. Nasema ntawapa.)

Miaka ya hivi karibuni TANZANIA hatutapata raisi mwenye hekma na busara Kama JK(MBAYUWAYU),Trust me🤔
 
Tunasubiria mzee mbayywayu akapige yake ......hamu kubwa tusubiri
 
Mahakama za yule wa tuhuma za mauji ya Kanumba ndio zilikuwa zikitoa haki. Kumbafu mkubwa.
Acha lugha chafu haikusaidii, kama unahoja iweke wazi mie nimetoa data kama una yako weka tuone.
 
Ni sawa kabisa, nami nimejiuliza kuhusu uwezo wake wa sasa juu ya utambuzi na uchakataji - uchambuzi wa kina na yakinifu wa mambo.
Huyu mzee wangemuacha tuu sio wa kumsumbua sumbua maana hata network zinakatakata, isije akaongea mambo ambavyo yatamuaibisha kumbe tatizo ni kumbukumbu
 
Usikute Mzee kuna mtoto wake anamtafutia kazi, ndiyo zake huyu,wakati anamtafutia Hussein Urais alikuwa anamsifia sana mwendazake.
 
Mama Sitti hapa paitwaje vile?.
Ikulu
Ahh Ikuluuuu[emoji28]

Mh Mwinyi tunaomba siri ya kuishi miaka mingi jmn na uko so happy.,
Siri ya kuishi miaka mingi ni 3 tu:

1.Uwe mcha Mungu

2.Usipende kufuatilia mambo ya watu yasiokuhusu

3.Acha kuweka vinyongo kwa waliokukosea
 
Hamna Mtanzania asiye taka kumuunga mkono Mh Rais, tatizo ni pale anaposhindwa kujipambanunua kuwa alikuwa msaidizi namba moja wa mwendazake. Wakati mwendazake ana chakufuliwa kakaa kimya kama hayuko na hasikii au anafurahia kimoyomoyo?! Ukweli ni kuwa Magufuli hawezi kuchafuliwa na walio tumikia naye wakafikiri watabaki salama. Spika anaona atabaki salama kwa kusema mwendazake alishauriwa vibaya ana sahau anayo skandali ya mabilioni ya matibabu ambayo ilikuwa ina hang somewhere ni suala la muda tu. Wakimaliza hii biashara yao kichaa ya kumpaka oil chafu mwendazake watamgeukia hili halihitaji akili kubwa kulijua. Alishauriwa na nani zaidi ya nyie mlio kuwa mnamzunguka na kufanyakazi pamoja naye?

Mbona Judge Mkuu hatumsikii akiendekeza haya mambo ya kusikitisha na kutahayarisha yanayo endelea kwa sasa hapa Tanzania. Huyu amekuwa kiongozi mweledi siku zote. Hotuba aliyoitoa siku ya maziko pale Chato ni kielelezo tosha cha kiongozi mwenye hekima.

Wazee wamshauri huyu ahamie mhimili wa Excutive ifikapo 2025 atawafaa sana Watanzania/Tanganyika.
Hivi hebu kuwa mkweli,ni nani amemchafua mwendazake?
 
Hivi hebu kuwa mkweli,ni nani amemchafua mwendazake?

Na kujibu kwa Neno la Mungu:
Waraka wa Yakobo3:17
Lakini hekima itokayo juu(kwa Mungu mbinguni), kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
 
Ha ha ha!

Huyu mzee Mwinyi huwa ananikosha sana

Jana baada ya kuonana na Mama Samia akawashauri wananchi kuacha balaa, ugomvi na fitna... na kuendeleza mshikamano.

Baada ya kucheka sana hasa balaa, ngoja nifikiri kwanza ili nidadavue maana yake ujumbe huu

ANGALIZO: MATAGA tulieni
 
Back
Top Bottom