Yaani kwa kweli Ndungai katudhihirishia alivyo mnafiki. Mikataba yote nakala zake ziko ofisini kwake bungeni pamoja na huo wa bandari ya Bagamoyo kati ya serikali ya awamu ya nne na kampuni ya serikali ya China. Katika zoezi la kufuta mikataba mibovu ambayo nchi yetu ilikuwa imeingia na makampuni mbali mbali ya kimataifa yeye Ndungai alikuwa kati ya washauri wakuu wa serikali ya awamu hiyo ya tano. Leo anasema rais wa awamu ya tano walimshauri visivyo/ vibaya kufuta mkataba huo wa bandari ya Bagamoyo. Auweke basi wazi mkataba huo watanzania wausome na kama ni kweli walimshauri vibaya basi hao waliohusika kumshauri wawajibishwe. Mbona huyu Ndungai hasemi kuwa na hilo la makao makuu kuhamia Dodoma walimshauri vibaya. Kisa cha aliyekuwa CAG, Prof Asad kutimuliwa kila mtu anajua mbaya wake alikuwa Ndungai. Mbona hasemi kuwa alimshauri vibaya rais kumtimua Prof Asad kwenye nafasi hiyo? Hata kutimuliwa kwa Makonda ukuu wa mkoa kila mtu anajua Ndungai alihusika sana, na kadhalika.
Halafu hivyo viapo wanavyoapa wanapopewa madaraka hayo ya kutunza siri za nchi wanapokuwa madarakani na hata watakapoondoka madarakani, mbona sasa wanazikiuka wazi wazi? Wameanza kuropoka ovyo ovyo hadharani siri za ofisi (Ndungai, Asad, Kichere, Muhongo, Kigwangala nk). Nini adhabu yao kwa mjibu wa sheria zetu?