THOMASS SANKARA
JF-Expert Member
- Nov 13, 2014
- 2,055
- 4,695
Acha kupotosha ana diploma ya Ualimu toka Makerere University ya miaka hiyo.Hana PhD bana, Ana diploma ya kiswahili!
Hata mm huwa namuona jaji mkuu kama mwenye upeo mzuri, lakin hataki katiba mpya.... Mtu wa fani ya sheria ndiye a natakiwa awe rais kwa sasaHamna Mtanzania asiye taka kumuunga mkono Mh Rais, tatizo ni pale anaposhindwa kujipambanunua kuwa alikuwa msaidizi namba moja wa mwendazake. Wakati mwendazake ana chakufuliwa kakaa kimya kama hayuko na hasikii au anafurahia kimoyomoyo?! Ukweli ni kuwa Magufuli hawezi kuchafuliwa na walio tumikia naye wakafikiri watabaki salama. Spika anaona atabaki salama kwa kusema mwendazake alishauriwa vibaya ana sahau anayo skandali ya mabilioni ya matibabu ambayo ilikuwa ina hang somewhere ni suala la muda tu. Wakimaliza hii biashara yao kichaa ya kumpaka oil chafu mwendazake watamgeukia hili halihitaji akili kubwa kulijua. Alishauriwa na nani zaidi ya nyie mlio kuwa mnamzunguka na kufanyakazi pamoja naye?
Mbona Judge Mkuu hatumsikii akiendekeza haya mambo ya kusikitisha na kutaharisha yanayo endelea kwa sasa hapa Tanzania. Huyu amekuwa kiongozi mweledi siku zote. Hotuba aliyoitoa siku ya maziko pale Chato ni kielelezo tosha cha kiongozi mwenye hekima.
Wazee wamshauri huyu ahamie mhimili wa Excutive ifikapo 2025 atawafaa sana Watanzania/Tanganyika.
Nilijua tuu pumba kama hizi haziwezi kukosekana.
Mama hawezi kua mrithi wa Maujinga ya Marehemu. Alishasema historia inakufuata kokote uendako hata kaburini historia yako itakufuata tuu.
Nae anazo taratibu zake za namna ya kuongoza na sio kumtetea marehemu mwenda zake.
Au nasema uongo ndugu zangu
Mbona amezungumza vizuri tu na waandishi wa habari?Ni sawa kabisa, nami nimejiuliza kuhusu uwezo wake wa sasa juu ya utambuzi na uchakataji - uchambuzi wa kina na yakinifu wa mambo.
Hamna Mtanzania asiye taka kumuunga mkono Mh Rais, tatizo ni pale anaposhindwa kujipambanunua kuwa alikuwa msaidizi namba moja wa mwendazake. Wakati mwendazake ana chakufuliwa kakaa kimya kama hayuko na hasikii au anafurahia kimoyomoyo?! Ukweli ni kuwa Magufuli hawezi kuchafuliwa na walio tumikia naye wakafikiri watabaki salama. Spika anaona atabaki salama kwa kusema mwendazake alishauriwa vibaya ana sahau anayo skandali ya mabilioni ya matibabu ambayo ilikuwa ina hang somewhere ni suala la muda tu. Wakimaliza hii biashara yao kichaa ya kumpaka oil chafu mwendazake watamgeukia hili halihitaji akili kubwa kulijua. Alishauriwa na nani zaidi ya nyie mlio kuwa mnamzunguka na kufanyakazi pamoja naye?
Mbona Judge Mkuu hatumsikii akiendekeza haya mambo ya kusikitisha na kutaharisha yanayo endelea kwa sasa hapa Tanzania. Huyu amekuwa kiongozi mweledi siku zote. Hotuba aliyoitoa siku ya maziko pale Chato ni kielelezo tosha cha kiongozi mwenye hekima.
Wazee wamshauri huyu ahamie mhimili wa Excutive ifikapo 2025 atawafaa sana Watanzania/Tanganyika.
Laiti ungejua hizi kesi zote zilikuwa zinatolewa maelekezo kwake na yeye anayatupa kwa watendaji basi usingemsifia kabisa Prof. Juma.
Ameharibu Judiciary vibaya mno, yaani mahakama inatoa maamuzi ya kisiasa kabisa na haikaripii kabisa utungwaji wa Sheria kandamizi. Watu wanakosa dhamana mahakamani kisa kukomoana tu, kosa la jinai ya kwenye penal code linageuka kuwa kosa la uhujumu uchumi, ukiuliza unaambiwa wacha aozee jela maana State Attorney wakiweka kosa la kwenye penal code anaonekana hafai.
Judge anapoona kuna sheria zinamlazimisha kutoa hukumu ambayo sio ya haki huwa anatoa hukumu lakini katika maoni yake binafsi (obiter dictum) huwa anashauri nini kifanyike, Ila hivi karibuni tumeona majaji waliojitoa akili kukazia hili ni wachache sana.
Magereza imejaa watu wamekosa dhamana kisa makosa ya kukomoana, mtu amekosa kulipa tax returns inageuka kesi ya uhujumu uchumi na anakosa bail sasa hiyo hela ya kulipa ataitoa wapi???? Na bail ni haki ya kikatiba kabisa imeorodheshwa kabisa kwenye bill of rights.
So hata Jaji Mkuu amezingua sana sema sababu hawezi kutimuliwa mpaka afikishe 65 au akiomba kupumzika na akikubaliwa na Rais.
Nimeshangaa sana kakutana na Mzee RUKHSA ambaye si ajabu aliuliza hapa wapi vile!? Akajibiwa Ikulu akasema oooohhhhh! Ikuluuuuuuu niliwahi kuishi hapa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 sasa nimekuja hapa kufanya nini? 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Hata mm huwa namuona jaji mkuu kama mwenye upeo mzuri, lakin hataki katiba mpya.... Mtu wa fani ya sheria ndiye a natakiwa awe rais kwa sasa
Jiwe aliingilia mihimili yote hata mahakama; Mpaka akawa anateua majaji kwenye mikutano ya hadhara!! Jaji Mkuu yuko kimyaaa huku akijua utaratibu ulikuwa unavunjwa! Hiyo sio sifa nzuri ya kiongozi.
Huyo Jaji aliepandishwa cheo kwenda mahakama ya Rufaa kwa kuandika judgement kwa Kiswahili; je huo Ndio utaratibu wa kupandishwa cheo katika mahakama? Sio siri kuwa kuna mahakimu [ wanajulikana] walipandishwa vyeo kwa kutoa hukumu kandamizi dhidi ya wapinzani wa ccm!Ukiteuliwa kwenye mkutano wa hadhara inamaanisha mchakato haukufuatwa? Hebu taja majaji walioko ambao hawana sifa za kuwa majaji. Hiki cheo na fikiri vigezo vyake ni international inclusive sio lokali tu.
Huyo Jaji aliepandishwa cheo kwenda mahakama ya Rufaa kwa kuandika judgement kwa Kiswahili; je huo Ndio utaratibu wa kupandishwa cheo katika mahakama? Sio siri kuwa kuna mahakimu [ wanajulikana] walipandishwa vyeo kwa kutoa hukumu kandamizi dhidi ya wapinzani wa ccm!
Waliangalia kigezo hicho tu cha kuandika hukumu kwa kiswahili. Acha ujanja ujanja kama wa Spika Ndugai. Leo amnajidai itangazwe tender wakati aliwapigia chapuo Wachina kwa presentation yao. Contradiction baada ya contradiction nyengine. Ooh sijui wa Oman wanajenga bandari Zanzibar sasa si jambo la manufaa na afya hilo. Hakuna Mtanganyika anayetaka kulipa kodi yake halafu ikatumike kumnunulia Mzanzibari umeme, hakuna.
Kwa hatua hii nampongeza Mh Rais Mwinyi Jr. Makontena ya Malawi ,Congo yakifika bandarini Zanzabar bado yatahitaji kutumia miundo mbinu ya Tanganyika kufika final destinations zake. Kwa nini mwenye akili asimsupport Mh Rais Mwinyi jr kwa ubunifu huu ?
Majibu yako hayaendani na nilichoandika kuhusu uhuru wa mahakama kuingiliwa!! Rais Mwinyi anakujaje hapo?
Unasema uongo mpaka unajidanganya mwenyewe! Hebu ongeza sauti kidogo...Ndugai alisababisha makonda akatimuliwa kazi? Are you serious?Yaani kwa kweli Ndungai katudhihirishia alivyo mnafiki. Mikataba yote nakala zake ziko ofisini kwake bungeni pamoja na huo wa bandari ya Bagamoyo kati ya serikali ya awamu ya nne na kampuni ya serikali ya China. Katika zoezi la kufuta mikataba mibovu ambayo nchi yetu ilikuwa imeingia na makampuni mbali mbali ya kimataifa yeye Ndungai alikuwa kati ya washauri wakuu wa serikali ya awamu hiyo ya tano. Leo anasema rais wa awamu ya tano walimshauri visivyo/ vibaya kufuta mkataba huo wa bandari ya Bagamoyo. Auweke basi wazi mkataba huo watanzania wausome na kama ni kweli walimshauri vibaya basi hao waliohusika kumshauri wawajibishwe. Mbona huyu Ndungai hasemi kuwa na hilo la makao makuu kuhamia Dodoma walimshauri vibaya. Kisa cha aliyekuwa CAG, Prof Asad kutimuliwa kila mtu anajua mbaya wake alikuwa Ndungai. Mbona hasemi kuwa alimshauri vibaya rais kumtimua Prof Asad kwenye nafasi hiyo? Hata kutimuliwa kwa Makonda ukuu wa mkoa kila mtu anajua Ndungai alihusika sana, na kadhalika.
Halafu hivyo viapo wanavyoapa wanapopewa madaraka hayo ya kutunza siri za nchi wanapokuwa madarakani na hata watakapoondoka madarakani, mbona sasa wanazikiuka wazi wazi? Wameanza kuropoka ovyo ovyo hadharani siri za ofisi (Ndungai, Asad, Kichere, Muhongo, Kigwangala nk). Nini adhabu yao kwa mjibu wa sheria zetu?