Rais Samia Suluhu Hassan ampa onyo Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo

waziri husika amepewa warning. akizembea zaid ya hapo kibarua bye bye
 
Ndio hayo aliyoambiwa sasa, Jafo anajifanya kukagua miradi kama kiini macho wakati huku nyuma ya pazia analinda upigaji mtupu.

Na kama hujui tu, zile ziara za kukagua miradi ndio mahali pa maafisa wa serikali kujilipa posho na masurufu mengine.

Rais amehoji, hiyo TAMISEMI imekuwa ikitaka tu kupewa pesa na serikali kuu lakini wao hawakusanyi pesa zao. Wanajipangia matumizi (posho, mishahara, miradi) wanavyotaka wao, wakati pesa sio za kwao na wala hawana uchungu nazo.
 
Nimesema,aliwadhihaki waliomtangulia kua nchi wameihalibu.
Matokeo yake yeye ndio kaihalibu zaidi.
Ila mungu nae hajawahi kuwaacha watanzania wanyonge wasiokua na hatia.
Ogopa sana kumuumiza na kumnyanyasa mtu masikini asie na hatia mungu hawezi kumuacha aendelee kunyanyaswa na kuzibwa mdomo pale anapodai haki yake.

Matokeo yake hata miaka 10 haikuisha nchi imehalibiwa kuliko vipindi vyote tangu kupata uhuru.
 

Ni kweli hata wafanya kazi ambao wapo chini ya Tamisemi wana lalamika sana mfano kada ya afya mtumiwhi wa ngazi ya chini let say nurse huwa wana lalamika sana kucheleweshea malipo yao mbalimbaali mfano overtime, hata mstaafu ambae alikuwa chini ya Tamisemi mambo yao yana chelwweshwa sanaaa urasimu mwingi wakurugenzi + DMO yaan ni kama Mungu watu vilio ni vikubwa hakuna kuoandishwa cheo.
Kwa kweli Jaffo ateremke tu
 
Kwanini TAMISEMI isikatwe kikanda.. iwe na waziri na manaibu waziri sita. NAIBU WAZIRI TAMISEMI 1)lake zone, 2)central zone, 3)northern zone, 4)coast zone, 5)southern highlands zone na 6)west Tanzania zone.

Hawa manaibu wawe specific kwa maeneo hayo sawa sawa na Manaibu Katibu wakuu wao. Labda itasaidia
 
Uendeshwaji huu wa Serikali za mitaa ni wahovyo.. wao badala ya kukaa na kuhudumia wananchi ili wajitoe kulipa kodi kikamilifu.. wanangojea bajeti wakae waanza kuzitumbua..

Katika kumi ni wawili utakuta kweli wana uchungu wa kuleta mabadiliko.. wengine business as usual nimepata kazi nilipwe mshahara.. hakuna drive.. na wakipelekeshwa for a week lawama hakuna mfano.

Huko kwenye kazi za serikali walitakiwa waende wenye nia kweli na wito.. sio watuna matumbo tu.. na kuning'iniza funguo. Wakiajiriwa tu wanaona ulaji..sio kazi..

Kwenye cv utumishi wangekuwa wanaomba na work plan.. ili waone kama hawa watumishi wako in tune na mazingira yao ya kazi au changamoto za wanaoenda kuwahudumia.. labda itasaidia
 
Mswahili alijikita kwenye kusifia tu, Mwigulu, Kabudi, Jafo, Ndalichako na Mkumbo hafai kabisa kuwa viongozi hata kwa dak 1
Mama akitaka kufanya makubwa na kuiendeleza hii nchi..afanye yafuatayo.
  • aunde baraza jipya haraka..
  • sheria za utumishi wa uma na maadili zizingatiwe bila kuoneana soni..
-afanye marekebisho ya katiba haraka..
- Awakataze wasaidizi wake kufanya kazi mbele ya kamera..wengi wanamdanganya na si watendaji bali wanajitafutia umaarufu.
-Amuongezee fungu Cag aweze kufika KILA shirika na taasisi..na ripoti yake ichukuluwe kwa uzito.
-asiwaone upinzani kama maadui bali wabia kwenye maendeleo ..wakiongea upuuzi wapotezee ..wakiongea point zichukue ziboreshe uzifabyie kazi.
-Umeshawahi kujiuliza ni kwa nn makampuni makubwa binafsi yapo KILA siku na yanatengeneza faida ila taasisi na mashirika ya serikali KILA siku hasara? Ni kwa sababu makampuni binafsi KILA mwajiriwa anapewa target..na lazima uzifikishe..utawezeshwa KILA kitu kazi kwako..na KILA quarter wanakufanyia review ya target zako..umezitekeleza vipi na umefika wapi..ni muda saaa serikali ina adopt mfumo wa haya makampuni utumike serikalini ..hii itapunguz mazoea na uzembe kazini..ukijua fika usipopiga kazi na ukizembea unapigwa chini
 
Ataanza kusifia na atasahau yote
 
Kakini pia huyu Jaffo ana nini cha mno mpaka aendelee kupewa maonyo kila siku juu ya utendaji wake na usimamizi wa mali za umma?
Katika hili Jaffo unatakiwa utumie hekima na busara kuiacha TAMISEMI, kiuhalisia wizara hii kubwa imekushinda
Labda anashindwa kugawa muda wake maana tuliambiwa ana bibi wadogo kadhaa
 
Kwani sasa hivi ina Manaibu wangapi? Ni kwamba kazi hajui tu yeye pamoja na timu yake.
 
Wa ukae ajikite kwenye fani yake ya nyungu tu uwaziri unaanza kumkataa kuonywa mara mbili hadharani na mkuu wa nchi ni dalili mbaya kabisa
 
Shida haipo kwa Jafo bali shida ipo kwa wakurugenzi na pia Tamisemi ni wizara ngumu ndo maana akawekwa kijana(Jafo) ili aweze kuimudu.
Upo sahihi kiongozi, Waziri Jafo sio mteuaji wala mwajibishaji wa watendaji wakuu wa Halmashauri (Wakurugenzi) na pia yawezekana mifumo ya uendeshaji wa halmashauri sio rafiki sana katika kudhibiti mambo yasiyoendana na matakwa ya serikali
 

Hivi hata Jafo akitumbuliwa ni nani atakayeweza kufit hiyo wizara?
Naona maccm wote damu zao zinafanana tu!
 
Ila wanzanzibar wana maneno matamu sana "Eti kama umeshindwa tuambie tukusaidie" utadhani ni komplimenti kumbe...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…