Rais Samia Suluhu Hassan ampa onyo Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo

Rais Samia Suluhu Hassan ampa onyo Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Jaffo ni hardworking kila mtu anaona anasukuma kazi ziishe. Yaani yeye mama Samia akishirikiana na marehemu wateue wakurugenzi, wakuu wa wilaya na wasimamizi wengi huko TAMISEMI ambao ni unqualified kwenye supervision roles halafu utegemee wajuzi wasione hizo weaknesses kupiga.

Watu wakishafanya yao baada ya kuwapelekea amateurs who are easy to deceive lawama apewe Jaffo.

Madiwani wakijitungia by-laws za ajabu ajabu sijui kutoza kodi michango ya harusi na wakurugenzi wasione tatizo lawama apewe.

Jaffo can’t be everywhere at once either akague miradi au abaki ofisini anasoma makarabasha ya halmashauri na by-laws zinazopendekezwa huko kila siku.

Kibaya zaidi zigo lote anatupiwa Jaffo wakati ana katibu mkuu wa wizara ambae hayupo pale on merit na wala hana elimu yoyote ya public management ni engineer tu by trade. Kwa ivyo common sense says Jaffo has to fight all the battles alone.

Kwa Jaffo wanamuonea kwa matatizo waliyotengeneza raisi na mtangulizi wake.
 
Hilo la Air Tanzania tulinganishe na mashirika ya ndege mengine kuwa yanafaida kiasi gani na kwa kipindi gani?
 
Hivi hata Jafo akitumbuliwa ni nani atakayeweza kufit hiyo wizara?
Naona maccm wote damu zao zinafanana tu!
Labda ndio maana Hayati Rais John Magufuli alikuwa anawajumuisha baadhi ya Wapinzani kwenye Serikali yake. Mfano ni Kitila Mkumbo.
 
Aisee ni kweli Tamisemi ni wizara iliyo sheheni mambo mengi na miradi na programu nyingi napendekeza baadhi ya miradi na programu zitolewe Tamisemi ziwe serikali kuu
Kimsingi TAMISEMI ndio Wizara inayogusa maisha ya kila siku ya kila Mtanzania. Mfano; Maji, Elimu, Afya, Ardhi, Biashara n.k
 
Kwanini TAMISEMI isikatwe kikanda.. iwe na waziri na manaibu waziri sita. NAIBU WAZIRI TAMISEMI 1)lake zone, 2)central zone, 3)northern zone, 4)coast zone, 5)southern highlands zone na 6)west Tanzania zone.

Hawa manaibu wawe specific kwa maeneo hayo sawa sawa na Manaibu Katibu wakuu wao. Labda itasaidia
We ni kikaza unadhani ni tamisemi ni chama cha mpira
 
The wizara is just too big for him. Am not sure of his qualifications. Too me he looks like a bogan - au muswahili who cares less. I cannot believe he was not sacked today JPM warned him. I think he doesn’t know where to start, the department is just too big. Mashule, hospital, councils- where can he start. Possibly also he has por management so he get very bad ushauri.
Your wrong.think about china there with their population of more thaj 1 billion.being minister there means you lead the wole africa.apambane na hali yake
 
Waliozoea kuimba mapambio ya kusifu na kuabudu kipindi Cha magufuli wakae mguu sawa...
 
Marehemu sijui hayati hata hajaoza nzi wameanza kuchafua hali ya hewa .alijua kutupiga propaganda
 
Kimsingi TAMISEMI ndio Wizara inayogusa maisha ya kila siku ya kila Mtanzania. Mfano; Maji, Elimu, Afya, Ardhi, Biashara n.k
Ni wizara iliyo pewa zamana ya kusimamia tawala za mikoa na serikali za mitaa
Yaan ni wizara inayo beba serikali
 
Yaani juzi tu wala maboga walibwatuka kuwa jiwe ni Rais pekee aliyeweza kuikoa Tz na genge la wezi.

Hata kabla hajaoza kaburini anaonekana ni mwizi. Tulisema mapema tukaonekana wasaliti kiko wapi sasa.

Cha ajabu wala maboga wanajinadi mtaani kuwa kimetoka chuma kimeingia chuma.

Acha kwanza nitafakari hizi kauli labda uwezo wangu wa kuwaza unaanza kuchoka.
Yatafichuka mengi subiri baada ya mwezi ujao utaona.
 
Mh. Rais amesema Wizara ya Tamisemi ina matumizi ya ovyo ya pesa za Serikali, yenyewe haikusanyi ni mwendo wa matumizi kwa kwenda mbele hivyo kamwagiza Waziri Jafo afuatilie vizuri matumizi ya wizara yake na kama akishindwa Basi asaidiwe(atumbuliwe)


Ushauri.

Mh Seleman Jafo jipange; Halmashauri, Hospitali,miradi ya ujenzi wa shule n.k hela zinapigwa sana, vituo vya afya EFD mashine hazitumiki vilivyo. Fuatilia Mama Samia hatakuhurumia atakutumbua shauri yako.
Lukuvi anatakiwa pia kutumbuliwa,ana agenda ya kuuza viwanja vyetu kisa hatuna pesa za ujenzi
 
mkuu kwan unafikir ni kazi lahisi kusimamia wakurugenz wa halimashauli zote nchin? ataenda sasa kuwabana wakulugenz wote maana hao ndio watendaj wake.


Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani hadi aende yeye? Hawa tuliowachagua kwenye Kata zetu wanafanya nini? Hili jukumu la pamoja, kwa hivyo na Rais Aliyewateua Wakurugenzi aende huko kuwafuatilia hebu CCM wajibikeni aisee mlisema mkipewa wawakilishi wa kijani mambo yata flow
 
Punguza speed ili uandike kitu chenye "CONTENT" Makosa ya kiuandishi yanaweza kuondoa credibility yako!!

"Anahonywa" sijui kiswahili gani hiki, huwa nakereka sana na watu msioweza kujua matumizi ya herufi"h"


Anyway, kujiuzuru ni rahisi kuizungumza, hata hivyo watajiuzuru wangapi? Kwakuwa amepewa nafasi nyingine ya yeye kufuatilia agizo hilo, tusubiri utekelezaji wake kisha tutahoji nafasi yake ya uwaziri!!

Ahsante!
Kujiuzuru ni nini???
 
Back
Top Bottom