Rais Samia Suluhu Hassan ampa onyo Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo

huwa nakereka sana na watu msioweza kujua matumizi ya herufi"h"


Anyway, kujiuzuru ni rahisi kuizungumza, hata hivyo watajiuzuru wangapi?


Na wewe ni walewale tu, sasa kujiuzuru ni kitu gani na wewe?
 
Kwani sasa hivi ina Manaibu wangapi? Ni kwamba kazi hajui tu yeye pamoja na timu yake.
Ndio maana nimependekeza ma naibu wake wawe wenye uzoefu na wakali zaidi kuliko waliopo sasa
 
Wa ukae ajikite kwenye fani yake ya nyungu tu uwaziri unaanza kumkataa kuonywa na mkuu wa nchi mara mbili hadharani ni dalili mbaya kabisa
 
Kujiuzulu
 
Upo sahihi kiongozi, Waziri Jafo sio mteuaji wala mwajibishaji wa watendaji wakuu wa Halmashauri (Wakurugenzi) na pia yawezekana mifumo ya uendeshaji wa halmashauri sio rafiki sana katika kudhibiti mambo yasiyoendana na matakwa ya serikali
Aisee ni kweli Tamisemi ni wizara iliyo sheheni mambo mengi na miradi na programu nyingi napendekeza baadhi ya miradi na programu zitolewe Tamisemi ziwe serikali kuu
 
Mbona huyu jaffo wamemuacha kwenye huo uwaziri muda mrefu kiasi hiki?
CCM ni ileile X10.
 
Jafo aachie ngazi tu kila kukicha yeye ni kuonywa tu sema hawawezi wengine maana huko kuna upigaji unaowafanya wabaki na report ya CAG haiwagusi sana
 
Mtaalamu wa nyungu. Na masifa. Yaani alikuwa akimsifu hayati utadhani yeye ni wa kike.
 
The wizara is just too big for him. Am not sure of his qualifications. Too me he looks like a bogan - au muswahili who cares less. I cannot believe he was not sacked today JPM warned him. I think he doesn’t know where to start, the department is just too big. Mashule, hospital, councils- where can he start. Possibly also he has por management so he get very bad ushauri.
 
Tanzania hata umlete Biden hata yeye atakua mwizi tu. Hii iko kwenye damu yetu
 
Waziri mkuu ndie ana leta giza hapa. Maana angekuwa na akili alitakiwa ajiuzulu ili Mh. Rais Samia aunde baraza lake. Sasa huyu kakaa tuu kama boga hajui ana mtesa Rais wetu. Majaliwa ana ogopa akijiuzulu hana tena nafasi. Sasa ata aibika zaidi pale Mh. Rais atakapo amua yeye kulivunja baraza. Maana hawezi kufanya kazi na watu ambao hawajala kiapo cha utii mbele yake.
Alie waapisha kesha pita hivi...
 
Huwa nashangaa pale watu wanapo msifia jaffo kwamba ni mchapa kazi, nabaki najiuliza huo uchapa kazi anaosifiwa nao unatokana na nini na ni mambo gani hasa amefanya huyu kijana kwenye wizara ya tamisemi hadi asifiwe kwamba ni mchapa kazi?

Kwa miaka mitano mfululizo hakuna ubunifu wala cha maana alichokifanya katika wiazara yake(kama kipo mniambie). Kazi yake kubwa kwa kipindi chote ilikuwa ni kusifia na kujipendekeza (uchawa) kwa boss wake.

Hata huo umaarufu alionao ameupata kutokana na media coverage maana wizara anayoongoza inagusa sekta zote na hivyo ni rahisi kwake kuonekana na kusikika kwenye vyombo vya habari kila siku na ndio chanzo cha yeye kuonekana mchapa kazi lakini behind jaffo ni debe tupu ambalo kazi yake ni kupiga makelele tuu.

Angalia hata ziara zake utakuta anaongea maneno mengi mithili ya ndege chiriku lakini utekelezaji wake ni sifuri.

Kwenye kudhibiti matumizi mabaya ya fedha kwenye miradi inayosimamiwa na wizara yake huku ndo hovyo kabisa. Mfano, kwenye miradi ya EP4R pesa zinapigwa lakini yeye yupo anaangalia wala hakuna hatua zozote anazochukua kuhakikisha pesa hizo zinarudishwa.

Baadhi ya halmashauri zilitengewa mamilioni ya pesa na serikali kwaajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi mbaya zaidi pesa zimeisha na ujenzi umeishia kwenye msingi na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa watu waliofanya ubadhilifu. Je kuna waziri hapa?

Huyu kijana apumzishwe tuu maana hata kiutendaji na ufuatiliaji anazidiwa na naibu waziri wake(david silinde)
 
Wapi Mataga wazee wa kuimba na kusifu?
Shirika la ndege lililokuwa linashangiliwa na vijakazi kumbe ni mufilisi
 
Aisseee na mama analielewa. Kila la kheri mchapakazi Jaffo
 
Mama mh Rais awe makini alikuwa msaidizi No 1 wa JPM. Asifikirie wenye akili watamchukulia kama wanavyoweza kumchukulia Waziri wa JPM. Mapungufu ya serikali ya JPM ni mapingufu ya Naibu wa Rais wake pia. Aangalie anavyo siriba kwa kupaka matope maana anajisiriba.

Hili la bandari kampaka matope PM kiaina flani hivi. Walengwa wakupigwa spana tayari wanaanza kuonekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…