Rais Samia Suluhu Hassan ampa onyo Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo

Pesa za miradi ya EP4R zinapigwa hadi huruma. Wahandisi wa halmashauri kwa kushirikiana na maafisa elimu pamoja na wakuu wa shule wanaandika calculations za kufoji kuhalalisha upigaji

Just imagine tofali moja la block unaambiwa limenunuliwa 5000, sink la choo haya yanayouzwa kati ya 15000-20000 unaambiwa limenunuliwa kwa 87000 mara mfuko wa cement umenunuliwa kwa 45000. Si upuuzi huuu?

Jaffo resign kwa hiari yako usingoje kutumbuliwa
 
Mhurumieni jafo Ana wizara 5, maana wake wanne ni wizara nne na tamisemi ya tano.
Kama cheo ndio kilimfanya aoe wake wanne ajiandae na maisha ya useja tuu sasa
Cheo ni dhamana.... cheo ni koti la kuazima
 
Najua hana cha kuwafanya lakini hata kumwambia Boss aliyewateua napo alishindwa? Jaffo mna mkingia kifua tuu lakn niwambie hata kama atapewa miaka 100 kwenye hiyo wizara hakuna mabadiliko yoyote atakayofanya maana uwezo wake wa kufikiri na kutenda ndio umeishia hapo.
 
Nashauri kuwe na zone officer ambae atamonitor kila mradi akishirikiana na pccb na cag .Jafo acheze na hao mabosi kuliko wakurugenzi wezi.
Je wakuu wa mikoa wanafanya nini kwa upigaji huu?
 
Hakupandishwa kwa sababu ya utendaji kazi bali ni kwa sababu ya ushikaji ili waendelee kufichiana siri.
Kumbuka Jafo alikuwa naibu waziri baadae Magu akampandisha. Hiyo inaonesha Jafo ni muwajibikaji ila hawa wa chini ake ndo wanamwangusha.
 
Umeongea kitu kizuri sana TAMISEMI irud kwa waziri mkuu ikuli ina mambo mengi sana ilijirundikia wakati wa bwana yule na yote hii ilikuwa sababu ya ubinafsi
 
Mhurumieni jafo Ana wizara 5, maana wake wanne ni wizara nne na tamisemi ya tano.
Uzee wako utakua wahovyo sana ,utashangaa anamiaka 50 mdomo kuuziba hawezi ,anazibwa wake wa 4,mchezo nakiuno hichohicho kimoja!!
 
Upo sahihi kiongozi, Waziri Jafo sio mteuaji wala mwajibishaji wa watendaji wakuu wa Halmashauri (Wakurugenzi) na pia yawezekana mifumo ya uendeshaji wa halmashauri sio rafiki sana katika kudhibiti mambo yasiyoendana na matakwa ya serikali
Nakuona mdau hongera kwa utetez
 
Nikweli. ,hata uchaguzi serikali za mitaa 2019_ akiwa kwenye dhamana alitumia pesanyingi akijua uchaguzi haupo..akaandaa uchafunzi kwapesa nyingi mama alishauri hakisikilizwa
 
Kujiuzuru [emoji777][emoji777][emoji777]

Kujiuzulu[emoji818][emoji819][emoji736]
 
Jafo wanamuonea tu,wakurugenzi wengi wameingia kwa kiki za uanachama wa kijani pia ni vilaza mno hawawezi kusimamia pesa za serikali.Aanzia kwa hao DED ndo shida zipo
Nayo inachangia pia,..mtu ajira ya kwanza kwenye utumishi wa umma anaanzia kwenye ukurugenz direct..mfano Yule Kamoga alikuwaga clouds, aliteuliwa direct kuwa mkurugenz mbulu huko na wapo wengi wa hivyo ...shida ni cheo cha utendaji kwa mtu aliyetoka nje ya system moja kwa moja lazima apate tabu kwa muda kufit,tofauti ya miaka ya nyuma walikuwa wanawapindisha wakuu wa idara waliofanya vizur
 

Kama anaonewa si nae pia aachie Ngazi!
 
Kama umejitambua sawa ni kweli uwezo wako wa kufikiri ni mdogo yani IQ yako ni ndogo inawezekana ni 0.00000001

Watu walikuwa wanasema JPM anapambana na wala rushuwa pamoja na mafisadi na alionyesha vitendo katika hili

Si dhani kama kuna mtanzania aliyewahi kusema kuwa JPM amemaliza wala rushuwa wote na mafisadi wote nchini

Sasa kama wewe hukuwahi kuziona juhudi za JPM katika kupambana na mafisadi pamoja na wala rushuwa hilo linatokana na uwezo wako wa kufikiri

Ila sisi wenye IQ kubwa tuliliona hilo na tunataka mama Samia aendeleze pale alipoishia
 

Kama uko ushahidi huo si fedha zipigwe pini na zirudishwe na awatumbue na atoe sababu hii kama kitumbulio.

Ila hii ya leo haiko vizuri jinsi inavyotumika. Mfano ATCL imepata hasara miaka mitano accumulative. Je wakati JPM anaishi, CAG alishatoa ripoti ikionesha ATCL walikuwa wanatengeneza faida? Je mashirika mengine ya ndege ya kaliba ya ATCL na makubwa yalitengeneza faida gani kipindi hicho? Tulinganishe.

Lakini mfano Suala la Mh Jaffo, JPM aliuliza kuhusu bei ya Stendi ya Mbezi ya Kimara hii inayoitwa Magufuli. Na alisema alijishauri kumchagua na kumrudidha tena lakini alifikiria anavyojituma usiku na mchana akaona haidhuru ampe another chance. Sasa kwa nini tena litake kutumika kutaka kumchafua JPM marehemu mbele ya macho ya Watanzania na kumpa Mh Rais SSH sifa eti hakujua yanayo endelea.!!

Propoganda za aina hii hazimsaidii wala hazita msaidia huyu Rais wetu zaidi ya kuwaudhi Watanzania na kumharibia asubuhi na mapema katika Urais wake. Yeye ajikite kutenda kazi na matokeo ya kazi yake yataonekana tu, utandawazi uko wa kutosha hasa. Hii ya kutaka kucheza na legacy ya JPM itamgharimu vilivyo. Ndio maana twajiuliza kwa nini kaanza na Riport ya CAG? Kwa nini jimapili huku wapambe nuksi mitandaoni wakikashifu marehemu JPM siku tatu tu baada ya kuzikwa kuwa angalikuwa kwenye mimbari Kanisani. Mara ngapi JPM kateu na baada ye akafanya kazi ya uapishaji jumapili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…