Rais Samia Suluhu Hassan ampa onyo Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo

Rais Samia Suluhu Hassan ampa onyo Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo

Mtendaji Mkuu wa Wizara ni Katibu Mkuu sio Waziri

Kama kukagua hata UV CCM huwa wanakagua miradi ya Serikal
Kwahivyo Jafo abapokagua majengo/madaraja/barabara anaendaga na akili ya Eng. Nyamhanga?
 
Hakuna wizara inaendeshwa kienyeji Kama tamisemi.

Kama vipi ivunjwe Elimu irudi wizara ya Elimu. Afya irudi wizara ya Afya. Kilimo wizara ya kilimo. N.k.

Hapo yabaki Mambo madogo madogo ya kiutawala Fullstop. Vinginevyo hizi story tuzizoee tu hakuna namna.
 
Kwan izo Halmashauri 8 ni zipi izo embu mwenye info ziorozeshe hapa
 
Mtendaji Mkuu wa Wizara ni Katibu Mkuu sio Waziri

Kama kukagua hata UV CCM huwa wanakagua miradi ya Serikal
Tafuta nini majukumu ya waziri kwa wizara yake utaelewa lasivyo utang'ang'ana na katibu mkuu!! Kwahivyo waziri ni mtendwaji sio mtendaji? Kwanini ikitokea shida waziri hushughulikiwa chap?? Acha siasa za kizamani
 
Mh. Rais amesema Wizara ya Tamisemi ina matumizi ya ovyo ya pesa za Serikali, yenyewe haikusanyi ni mwendo wa matumizi kwa kwenda mbele hivyo kamwagiza Waziri Jafo afuatilie vizuri matumizi ya wizara yake na kama akishindwa Basi asaidiwe(atumbuliwe)....
Waziri Jafo ni dhaifu sana TAMISEMI ilishamshinda siku nyingi anastahili kutumbuliwa
 
Praise and Worship gang walishasema Jaffo ni Rais wa JMT anayesubiri muda tu. Leo tena hafai, jamani!!!

Kumbe manyani ni sahihi kushangilia bila kuhofia kufa make kama njaa imetupiga miaka 5 bila kufa sembuse hii miaka 4 iliyobakia ya awamu 5.
Labda hicho cha kuutaka URAIS kinaweza kumfanya awe target au anakusanya nguvu ya kifedha ili aupambanie maana siasa nazo mkono mtupu haulambwi na penye uzia penyeza rupia
 
Kumbuka Jafo alikuwa naibu waziri baadae Magu akampandisha. Hiyo inaonesha Jafo ni muwajibikaji ila hawa wa chini ake ndo wanamwangusha.
Jafo ni muwajibikaji mzuri tu, tatizo ni kwamba ana-deal na idara ambazo kuna uozo wa kutisha. Ni nani asiyejua kuwa halmashauri za jiji, miji, wilaya, nk ni maeneo ambayo huko nyuma watu walikuwa wamejihalalishia kuwa ni sehemu zao za ulaji? Miradi feki, malipo feki, tenda feki, safari feki, almost kila kitu feki, ili kuhalisha ulaji na ugawanaji pesa. Kung'oa kabisa mizizi ya huo wizi inahitaji kazi ya ziada!
 
Mh Jaffo nimeona hii na kuikubali ya kampa kampa tena. Wakurugezi wako mikononi mwa Mh Rais kwa maamuzi ya mstakabali wao Mh Waziri kafanya upande wake. JPM ni Mwalimu mzuri katuachia viongozi wanaojielewa na walio smart kiasi cha kuridhisha. Mh Rais akitumia mitizamo na maarifa ya wanaofikiri bado tuko awamu nne itamuwia vigumu.
 
Zamani wakati viongozi bado ni viongozi, kiongozi alikua akikosolewa hadharani, anawajibika mwenyewe kabla ya kuwajibishwa ili kulinda heshima yake siku za usoni, sisi vioo.ngozi wa doti.komu tunavimba mwanzo.mwisho.
 
Msimponde kwani Tamisemi ni wizara ngumu saaana na ina hitaji uwe na moyo imara.
Unadhani kusimamia halmashaur zaid ya elfu 5 si mchezo wa kitoto.
 
Back
Top Bottom