Sio sawa. Ikizingatiwa pia inayoonekana machoni ni kwamba hakufahumu uteuzi huu (hata kama alizungumza kuhusu uteuzi huu na Rais) mpaka jina lake lilipotangazwa na kupigiwa kura - ingetosha kushuku uteuzi, kuaga bunge na kuahidi kushirikiana na vyombo vyote!! Kuanza kuzungumza mambo ambayo serikali itafanya ni sawa. Direction serikali itafuata huongozwa na Rais. Angempa Rais nafasi ya kutoa mwelekeo atakapolihutubia Bunge.
Dr. Mpango amekosa protokali tu. Lakini atajifunza kadiri muda utakavokwenda.
Mie sijui tukoje kwenye lindi baya la umasikia wakati ni juzijuzi tu hapa alikuwa kinara wa kusema tumetoka uchumi wa chini na kuja wa kati! Au ilikuwa ni hadaa na propaganda???
Ni hivi, viongozi wote wa CCM wanatakiwa kufuata ilani ya CCM, hawatakiwi kufuata mtu.
Huyo Dr. Mpango kashawahi kumkatalia mambo Dr. Magufuli, wakati Dr. Magufuli akiwa rais.
Akampa sababu zake Dr. Magufuli. Dr. Magufuli akamuelewa.
Kwa hiyo si kweli kwamba msaidizi wa rais anatakiwa kufuata yote ya rais.
Kwa hiyo, as long as Dr. Mpango anaijua ilani ya CCM, na kasema mambo ambayo yamo katika ilani ya CCM, hakuna kibaya hapo.
Kwa sababu hata rais Samia Suluhu Hassan anaitekeleza ilani ya CCM.
Tatizo mnaangalia watu, badala ya kuangalia sera. Mmezoea siasa zile za "rais ndiye star, wengine wote wawe kimya kama supporting acts, wao kazi yao kuimba chorus tu".
Sasa alichokisema Dr. Mpango ambacho kipo nje ya ilani ya CCM ni kipi?