Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Dk Mpango alikuwa anafanya kazi World bank ..2007 Kikwete akamleta Ikulu awe advisor wa mambo ya uchumi kafanya kazi na Kikwete miaka 8 na alipokuja JPM akampa uwaziri wa fedha ..Kikwete amewapiga chenga ya mwili
Ukitaka kula nawe ukubali kuliwa kidogo.

Ha ha ha ha ha
 
Jina hilo limepelekwa Bungeni na Mpambe wa Rais (ADC) Kanali Nyamburi Mashauri, na kukabidhiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Spika Ndugai akisoma ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema..

Mheshimiwa Spika, nawasilisha Bungeni Jina la Mheshimiwa Philip Isdori Mpango kwa Nafasi ya Makamu wa Rais Tanzania.

Soma > Wasifu wa Dkt. Philip Isdori Mpango

Bunge lamthibitisha kwa kishindo
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dkt. Philip Isdor Mpango kwa asilimia 100 kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura zote 363 za wabunge waliopiga kura.

Dk Philip Mpango alizaliwa July 14, 1957 alikuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Mpango ni mzaliwa wa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu. Dk Mpango alizaliwa hapohapo Kasumo na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika Magharibi – Kasulu mkoani Kigoma, Dk Gerard Mpango.

Dk Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi. Hata hivyo, hadi sasa taarifa zake za elimu ya msingi, sekondari na shahada za awali za chuo kikuu hazijapatikana naye amekuwa vikaoni Dodoma muda mrefu na alishindwa kuzitoa kwa wakati.

Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, alifanya kazi akiwa mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alikuwa akifundisha “Microeconomics”,

“Macroeconomics” (kwa mwaka wa pili) na “Public Finance” kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili.

Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais. Nyadhifa hizi zote amezishika wakati wa utawala wa Kikwete.

Hayati Magufuli alipoingia madarakani alimteua kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya siku chache akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Dk Mpango ni kiongozi mwenye msimamo thabiti. Baadhi ya watendaji ambao wamewahi kufanya kazi chini yake kwenye ofisi ya Rais wanamuelezea kama mtu anayetaka waliomzunguka wazungumze kwa takwimu na ushahidi hasa katika masuala ya uchumi. Msimamo huo pia aliuonyesha alipokuwa mtaalamu wa Benki ya Dunia. Hakuwa mwoga kuieleza ukweli Serikali pale ambako ilikuwa haifanyi vizuri.

Mathalan, wakati wasomi wengi wa uchumi wakiwa wanapiga kelele za kuisifia Serikali juu ya ukuaji wa uchumi miaka ya mwanzoni ya 2000, Dk Mpango alieleza wazi kuwa lengo hilo la kukuza uchumi kwa asilimia 5.9 haliwezi kufikiwa kwa sababu katika miaka minne iliyopita, Serikali ilishindwa kulifikia.

Alisema: “Angalia kwa miaka minne hadi mitano iliyopita ambayo tulikuwa na sera nzuri za kibajeti, hakuna mwaka ambao ukuaji huo ulifikiwa, hizo ni dalili tosha kwamba hali hiyohiyo ndiyo itajitokeza mwaka huu.”

Hongera Dk. Mpango. Ila wasilisha vyeti vyako kuthibitisha elimu yako ya msingi, secondari, na chuo kikuu ili uzibe midomo ya wanoko.
 
veronica anaongea ukweli? lol jesus man seriously.
am not a fan of bothe of them. but niseme wote ni wazee wa kuspeculate.
atleast maybe kigogoo ana access na inside stories.. ila na yy wale wale.
hamna mwenye nafuu.
Kuna siku nilisema baada ya kumuwahi Magufuli vijana wote wanaoendesha account ya kigogo wataanza kuuliwa ili kulinda ushahidi.

Siku si nyingi wakuu wa huo mtandao wataanza kutajwa
 
Jina hilo limepelekwa Bungeni na Mpambe wa Rais (ADC) Kanali Nyamburi Mashauri, na kukabidhiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Spika Ndugai akisoma ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema..

Mheshimiwa Spika, nawasilisha Bungeni Jina la Mheshimiwa Philip Isdori Mpango kwa Nafasi ya Makamu wa Rais Tanzania.

Soma > Wasifu wa Dkt. Philip Isdori Mpango

Bunge lamthibitisha kwa kishindo
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dkt. Philip Isdor Mpango kwa asilimia 100 kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura zote 363 za wabunge waliopiga kura.

Dk Philip Mpango alizaliwa July 14, 1957 alikuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Mpango ni mzaliwa wa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu. Dk Mpango alizaliwa hapohapo Kasumo na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika Magharibi – Kasulu mkoani Kigoma, Dk Gerard Mpango.

Dk Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi. Hata hivyo, hadi sasa taarifa zake za elimu ya msingi, sekondari na shahada za awali za chuo kikuu hazijapatikana naye amekuwa vikaoni Dodoma muda mrefu na alishindwa kuzitoa kwa wakati.

Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, alifanya kazi akiwa mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alikuwa akifundisha “Microeconomics”,

“Macroeconomics” (kwa mwaka wa pili) na “Public Finance” kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili.

Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais. Nyadhifa hizi zote amezishika wakati wa utawala wa Kikwete.

Hayati Magufuli alipoingia madarakani alimteua kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya siku chache akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Dk Mpango ni kiongozi mwenye msimamo thabiti. Baadhi ya watendaji ambao wamewahi kufanya kazi chini yake kwenye ofisi ya Rais wanamuelezea kama mtu anayetaka waliomzunguka wazungumze kwa takwimu na ushahidi hasa katika masuala ya uchumi. Msimamo huo pia aliuonyesha alipokuwa mtaalamu wa Benki ya Dunia. Hakuwa mwoga kuieleza ukweli Serikali pale ambako ilikuwa haifanyi vizuri.

Mathalan, wakati wasomi wengi wa uchumi wakiwa wanapiga kelele za kuisifia Serikali juu ya ukuaji wa uchumi miaka ya mwanzoni ya 2000, Dk Mpango alieleza wazi kuwa lengo hilo la kukuza uchumi kwa asilimia 5.9 haliwezi kufikiwa kwa sababu katika miaka minne iliyopita, Serikali ilishindwa kulifikia.

Alisema: “Angalia kwa miaka minne hadi mitano iliyopita ambayo tulikuwa na sera nzuri za kibajeti, hakuna mwaka ambao ukuaji huo ulifikiwa, hizo ni dalili tosha kwamba hali hiyohiyo ndiyo itajitokeza mwaka huu.”

Chama na Rais Samia Suluhu Hassan wame-hit the bull.Phillip Isdor Mpango ni mtu sahihi kabisa kwa kazi ya Uwaziri Mkuu.Now I have peace of mind and heart.

Najua sasa kwamba Taifa litasonga mbele kama tulipokuwa na Hayati Magufuli,kama si zaidi.
 
Imepenya hiyooooooo

Hongera sana Philip Mpango kwa uteuzi

Tuna imani kubwa kwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, Mungu akutunze sana Madame

Rest well our hero President John Pombe Joseph Magufuli, ujue tuu ulituachia viongozi makini sana

Ila aliyetungaga haka kawimbo sijui aliwazaga nini

Chama imara, serikali imara...... ngoja nikajiunge rasmi sasa nipate usajili wa chama kwa mara ya kwanza
Chawa kama chawa, mapambio hakuna mwaku huu na utukufu tumeshauzika.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Masikini mwee!

Wewe ni kidagaa tu hapa nchini, hujui chochote utaendelea kushudia ccm wakibadirishana vyeo huku wewe ukiendelea kupiga yowe hapa Jf
Hilo Senge lipuuzie linalipwa na mabwana zake kuuneza uzushi.
 
Huyu mama anaenda kutuibia watanganyika, kwa kutuwekea mtu bomu pale Hazina. Kwa mara ya kwanza tangu napata fahamu Watanganyika tumekuwa na waziri wa fedha asiyetuibia. Sasa ku toa hapo ni mipango ya wizi TU.
Aiseeee
 
Chawa kama chawa, mapambio hakuna mwaku huu na utukufu tumeshauzika.

Hata maneno unayotumia yanaonyesha uwezo wako finyu wa fikra

Kwa taarifa yako Tanzania iko imara sana

Na serikali ya chama tawala iko imara kwelikweli

Hutaki na wewe hama nchi
 
Back
Top Bottom