Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Kama ilivyokuwa 2015 kwa JPM ,sasa hivi tena Chadema wako bize kumsifia, kumfundisha na kumpa maelekezo mbalimbali Rais Samia bila kujua kuwa huyo ni rais anayetokana na ccm na anatekeleza ilani ya ccm.

Godbless Lema ,Tundu Lisu hawazungumzii kabisa maendeleo ya chadema wao ni bize kumpangia cha kufanya rais Samia. !

Tundu Lisu ni kaimu mwenyekiti wa chadema lakini hutakaa usikie akiiongelea wala kuitangaza chadema popote. Kwani haoni kaimu mwenyekiti wa ccm Philip Mangula anavyokinadi chama chake?

Tundu Lisu ni mtanzania lakini hutakaa usikie popote akizungumzia mazuri ya nchi yake ,yeye ni kuchafua tu nchi yake.
Umesahau kuwa siasa zilipigwa ban baada yauchaguzi na mshindi kutangazwa.
 
Nimesikiliza hotuba ya Mheshimiwa Makamu wa Rais Mteule na imenitia wasiwasi kidogo. Pamoja na kusifia idadi ya wananchi watu waliomsindikiza Hayati Mheshimiwa Rais aliyepita, hakutoa neno lelote kuhusu waliojeruhiwa na waliopoteza maisha yao katika tukio hilo.

Nimemshangaa pia kuwalaumu wapinzani kwa misimamo yao ya kupinga bajeti ambazo waliona zina walakini. Hii kwangu mimi inaashiria kuwa imani yake katika mfumo wa vyama vingi ni ndogo. Kutumia nafasi adimu aliyopata kuwapiga vijembe wapinzani badala ya kuanza kujenga madaraja sio ishara njema.

Kwangu mimi amenitia wasiwasi kuwa kwake yeye Chama chake ni zaidi ya Taifa. Namuuomba Mungu kuwa atanithibitishia kuwa sijamtendea haki.

Amandla...
 
Sio sawa. Ikizingatiwa pia inayoonekana machoni ni kwamba hakufahumu uteuzi huu (hata kama alizungumza kuhusu uteuzi huu na Rais) mpaka jina lake lilipotangazwa na kupigiwa kura - ingetosha kushuku uteuzi, kuaga bunge na kuahidi kushirikiana na vyombo vyote!! Kuanza kuzungumza mambo ambayo serikali itafanya ni sawa. Direction serikali itafuata huongozwa na Rais. Angempa Rais nafasi ya kutoa mwelekeo atakapolihutubia Bunge.

Dr. Mpango amekosa protokali tu. Lakini atajifunza kadiri muda utakavokwenda.

Mie sijui tukoje kwenye lindi baya la umasikia wakati ni juzijuzi tu hapa alikuwa kinara wa kusema tumetoka uchumi wa chini na kuja wa kati! Au ilikuwa ni hadaa na propaganda???
Simlaumu maana kila mteule alilazimika kutaja majina yote 4 ya Rais kila mara mara zote
 
Ni hivi, viongozi wote wa CCM wanatakiwa kufuata ilani ya CCM, hawatakiwi kufuata mtu.

Huyo Dr. Mpango kashawahi kumkatalia mambo Dr. Magufuli, wakati Dr. Magufuli akiwa rais.
Akampa sababu zake Dr. Magufuli. Dr. Magufuli akamuelewa.

Kwa hiyo si kweli kwamba msaidizi wa rais anatakiwa kufuata yote ya rais.

Kwa hiyo, as long as Dr. Mpango anaijua ilani ya CCM, na kasema mambo ambayo yamo katika ilani ya CCM, hakuna kibaya hapo.

Kwa sababu hata rais Samia Suluhu Hassan anaitekeleza ilani ya CCM.

Tatizo mnaangalia watu, badala ya kuangalia sera. Mmezoea siasa zile za "rais ndiye star, wengine wote wawe kimya kama supporting acts, wao kazi yao kuimba chorus tu".

Sasa alichokisema Dr. Mpango ambacho kipo nje ya ilani ya CCM ni kipi?
Sio kweli, ilani ni muongozo tu, Rais anaweza kuachana na baadhi ya ahadi na kuchukua uelekeo mwingine naana katiba imempa madaraka makubwa Rais. Anaweza kusema ilani haitekelezeki akaamua kufanya anavyoona inafaa na hakuna chombo cha kikatiba kinachoweza kumzuia Rais. Hata JPM alipoamua kusema wacha niitumie katiba hiihii kwanza kuinyoosha nchi hakuwa anaangalia yaliyomo kwenye ilani
 
Kama ilivyokuwa 2015 kwa JPM ,sasa hivi tena Chadema wako bize kumsifia, kumfundisha na kumpa maelekezo mbalimbali Rais Samia bila kujua kuwa huyo ni rais anayetokana na ccm na anatekeleza ilani ya ccm.

Godbless Lema ,Tundu Lisu hawazungumzii kabisa maendeleo ya chadema wao ni bize kumpangia cha kufanya rais Samia. !

Tundu Lisu ni kaimu mwenyekiti wa chadema lakini hutakaa usikie akiiongelea wala kuitangaza chadema popote. Kwani haoni kaimu mwenyekiti wa ccm Philip Mangula anavyokinadi chama chake?

Tundu Lisu ni mtanzania lakini hutakaa usikie popote akizungumzia mazuri ya nchi yake ,yeye ni kuchafua tu nchi yake.
Kwani wewe ni lini ulisifia mazuri ya nchi yako na chama chako,(sorry kumbe hata chama huna) unataka aongelee hewani wakati wenye nchi yao walishawapiga marufuku au unajifanya umesahau maneno haya"uchaguzi umekwisha hakuna mikutano au siasa (kwa vyama vingine) hapa ni kazi tu.Kwao hakuna shida ni ruksa mikutano na siasa.

Anachafua nchi, si na wewe uchukue dekio udeki au usafishe nchi.Kipi kinakushinda hapo.Acha uvivu,kama anachafua na wewe safisha ngoma iwe droo.
 
Kuna mchezo sio wa bahati mbaya ,ila swala la kila wakati watu sifia marehem Kama vile mpaka mda huu hatuna serikali mpya ,sio mzuri naweza sema Kuna agenda ya kikundi flani , na haya yanatoka karne hii, hivi mbona kipindi kile Mwl Nyerere ameacha kiti mridhi wake,au Mkapa KWA mridhi wake hatukusikia, na je ni kwamba mh kikwete alitenda mema zaidi mzidi mtangulizi wake au mh Mwinyi alitenda zaidi mzidi Mw Nyerere, kola uongonzi na Zama zake,KWA siku hizi Chache Kama anasimama na kuona marehem bado ni zaidi ya uongozi uliokabidhiwa nchi ni muogopen Kama ukoma na ni lazima ashughulikie haraka, anachofanya ni kuaribu psychology ya viongozi walio madarakani ,
Kusifu kuabudu pia KWA Muhimili yetu hakusaidi lolote na hatuwezi songa Kama taifa ,hivi inakeje bunge lenye wabunge 300 et mteule vp anapata asilimia 100 ,kwamba katika wabunge wote fikra zenu ni level sawa, ndio kupitia sio tatizo ila why kuaminisha dunia kitu ambacho hakiwezekaniki? Hata baba ndani ya familia sio kila Jambo anaweza sema likaungwa mkono KWA asilimia 100 sembuse bunge lenye watu tofauti,sifa tofauti, hii ni aibu,
Tumeona nchi mfano SA hata rais mda mwingine anawekewa ungangari je ili tz KWA bunge letu Lina weza kweli pale panapo stahili
Nilitoa wazo hapa jf ili kupata bunge la kumsaidia Rais na nchi bila kujali ghalama livunjwe, ni vichekesho,maana watu au nchi dunian wanatushangaa nakuona kila mtanzania thinking capacity ni sufuli,
Hili ni aina ya bunge ambalo nadhani lilijiandaa kuondoa uko wa uongozi.
 
Kama ilivyokuwa 2015 kwa JPM ,sasa hivi tena Chadema wako bize kumsifia, kumfundisha na kumpa maelekezo mbalimbali Rais Samia bila kujua kuwa huyo ni rais anayetokana na ccm na anatekeleza ilani ya ccm.

Godbless Lema ,Tundu Lisu hawazungumzii kabisa maendeleo ya chadema wao ni bize kumpangia cha kufanya rais Samia. !

Tundu Lisu ni kaimu mwenyekiti wa chadema lakini hutakaa usikie akiiongelea wala kuitangaza chadema popote. Kwani haoni kaimu mwenyekiti wa ccm Philip Mangula anavyokinadi chama chake?

Tundu Lisu ni mtanzania lakini hutakaa usikie popote akizungumzia mazuri ya nchi yake ,yeye ni kuchafua tu nchi yake.
Mkuu kwani kuna ubaya wapinzani kuongelea maendeleo ya nchi?
 
Sio kweli, ilani ni muongozo tu, rais anaweza kuachana na baadhi ya ahadi na kuchukua uelekeo mwingine naana katiba imempa madaraka makubwa rais. Anaweza kusema ilani haitekelezeki akaamua kufanya anavyoona inafaa na hakuna chombo cha kikatiba kinachoweza kumzuia Rais. Hata JPM alipoamua kusema wacha niitumie katiba hiihii kwanza kuinyoosha nchi hakuwa anaangalia yaliyomo kwenye ilani
Wewe unatetea udikteta na mfumo wa kumfuata mtu mmoja.

Mimi natetea mfumo wa utawala wa sheria, kufuata ilani na sera.

Ndiyo tofauti yangu na wewe.

Hatuwezi kuelewana.

I am enlightened. You are still in the dark ages.
 
Kama ilivyokuwa 2015 kwa JPM ,sasa hivi tena Chadema wako bize kumsifia, kumfundisha na kumpa maelekezo mbalimbali Rais Samia bila kujua kuwa huyo ni rais anayetokana na ccm na anatekeleza ilani ya ccm.

Godbless Lema ,Tundu Lisu hawazungumzii kabisa maendeleo ya chadema wao ni bize kumpangia cha kufanya rais Samia. !

Tundu Lisu ni kaimu mwenyekiti wa chadema lakini hutakaa usikie akiiongelea wala kuitangaza chadema popote. Kwani haoni kaimu mwenyekiti wa ccm Philip Mangula anavyokinadi chama chake?

Tundu Lisu ni mtanzania lakini hutakaa usikie popote akizungumzia mazuri ya nchi yake ,yeye ni kuchafua tu nchi yake.

Wewe ni popo
 
March 2012
Dar es Salaam, Tanzania

Dr. Philip Mpango outline Key Strategies for Tanzania, that will enable rapid Socioeconomic Transformation

Dr. Phillip Mpango's keynote address on Socioeconomic Transformation for Poverty Reduction at REPOA's 17th Annual Research Workshop in March 2012.

Dr. Mpango is the Executive Secretary of the Tanzania Planning Commission
Source : REPOA Tanzania
 
19 Apr 2012
Dar es Salaam, Tanzania

Socioeconomic Transformation for Poverty Reduction in Tanzania - Dr. Phillip Mpango - 1

Part 1 of 4 of Dr. Phillip Mpango's keynote address on Socioeconomic Transformation for Poverty Reduction at REPOA's 17th Annual Research Workshop in March 2012. Dr. Mpango is the Executive Secretary of the Tanzania Planning Commission
Source : REPOA Tanzania
 
Dk Mpango alikuwa anafanya kazi World bank ..2007 Kikwete akamleta Ikulu awe advisor wa mambo ya uchumi kafanya kazi na Kikwete miaka 8 na alipokuja JPM akampa uwaziri wa fedha ..Kikwete amewapiga chenga ya mwili
Ni kweli Mpango alikuwa Tume ya Mipango etc Wakati wa JK, lakini utekelezaji wa awamu ya nne ulikuwa kinyume na sera zilizotolewa na Tume ya Mipango.

Waziri wa Fedha Zakia na Baadaye Mkuya ndio waliokuwa watekelezaji " we sera au maamuzi" ya awamu ya nne.

Ingekuwa Mpango anathaminiwa, ilitakiwa yeye ndio apewe hiyo wizara , Baada ya Mgimwa.

JPM aliliona hilo ndio maana kwenye awamu ya 5 akamchagua waziri.

Na sera zao zilikuwa zinaendana, Ile kwenye utekelezaji ndio haikuwa 100%
 
Tanzania sasa ina MPANGO baada ya kupata SULUHU kutokana matatizo yaliyobabishwa na POMBE.
 
Naona sasa kuna nafasi ya wasomi kuongoza mabadiliko katika Maendeleo ya Watu na Maendeleo ya Vitu.

Wachanganua changamoto za utaalamu wa uongozi, uwezeshaji kuanzishwa viwanda , nishati na miundombinu.

Ni matumaini uongozi wa awamu ya 6 chini ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan na makamu wake Mh. Dr. Philip Isdor Mpango watapata wasaa wa kuchukua mapendekezo maana wanaonesha ni viongozi wasikivu.

Published on 23 May 2017

Panel "Leadership as a Meta Institution"​

PANEL 2: Leadership as a Meta Institution Moderator: Dr. Donald Mmari Hon. Judge Joseph Warioba Hon. Basil Mramba Hon. Charles Mwijage Dr. Charles Kimei Prof. Adolf Mkenda Maj.(rtd) Joseph Butiku, Prof. Marcelina Chijoriga Tanzania’s leading think Tank REPOA in collaboration with the European Union Delegation to Tanzania and the East Africa, organized a workshop on how institutions enhance or constrain socio-economic transformation, particularly a transformation which puts industrialization at the centre of its development path.

The workshop held in Dar es Salaam featured international and national high-level researchers, policy makers, development partners, CSOs and media to promote the research on how institutions may ease the industrialization development in Tanzania. The workshop enhanced the understanding of the role of institutions (and individuals) in shaping the character of growth and socio-economic transformation, both in theory and practice in Tanzania.

Furthermore, the workshop brought together researchers and members of governmental bodies, as well as civil society representatives, to further promote research and deepen policy dialogue on the institutional needs for the Second Five-Year Development Plan and Development Vision 2025
Source: REPOA Tanzania
 
Dk Mpango alikuwa anafanya kazi World bank ..2007 Kikwete akamleta Ikulu awe advisor wa mambo ya uchumi kafanya kazi na Kikwete miaka 8 na alipokuja JPM akampa uwaziri wa fedha ..Kikwete amewapiga chenga ya mwili

You might have a point! But my intuition opposes it!

If so, how did VP Mpango come to be hand in glove with the late JPM?

I mean he knows ‘almost’ all the transactions made in this country!

Or maybe he was a doubleheader? For 5years? Mmh!
 
Back
Top Bottom