Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Hivi kwa akili zenu miaka hii 4 mnadhani raisi Samia ataahidi nini zaidi ya kutekeleza tu miradi iliyoachwa!!?..mama samia ili aweze kufaulu inabidi anate mulemule walipokuwa na mzee pombe..
 
Wewe unatetea udikteta na mfumo wa kumfuata mtu mmoja.

Mimi natetea mfumo wa utawala wa sheria, kufuata ilani na sera.

Ndiyo tofauti yangu na wewe.

Hatuwezi kuelewana.

I am enlightened. You are still in the dark ages.
Katiba yetu hairuhusu hivyo unavyotaka, Rais kwa mujibu wa katiba yetu ni kila kitu na hakuna chombo kinachoweza kumpangia cha kufanya wala cha kusema. Alichofanya Mh. Mpango kama angekuwa amenfanyia JPM hivyo sasa hivi tungekuwa tunaongea habari nyingine. Kama unadhani katiba inatakiwa iruhusu hivyo huna budi kuibadilisha kwanza ili iruhusu hiko.

Binafsi sina tatizo na Dkt Mpango kwakuwa ni miongoni mwa viongozi wenye afadhali kwenye serikali iliyopo. Hana makundi na ana hofu ya Mungu, lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba baada ya kupitishwa angeishia kulishukuru bunge na Rais kwa uteuzi na kuahidi kumsadia Rais kikamilifu kwenye majukumu atakayopewa na boss wake. Ikumbukwe kuwa mama Samia halazimiki kufanya kama alivyofanya JPM hasa kwenye mambo ambayo hayavunji katiba. Mfano, Rais Samia halazimiki kuwaachia machinga wachafue mazingira ya mitaa, stendi, masokoni, na kila pahala kama alivyofanya JPM. Mama Samia halazimiki kuacha kuangalia hali ya kipato cha wafanyakazi kama alivyofanya JPM kwa miaka 6. Lazima atatafuta viatu vyake vinavyomtosha yeye kama yeye. Hivyo, usitegee kuwa atafanya kila kitu alichofanya JPM, alichoahidi JPM na kila kilichomo kwenye ilani. Ziko ilani ambazo hazitekelezeki kwa 100% bila ya kuathiri sehemu nyingine muhimu pia. Rais inalazima kuifuata katiba kwa 100% lakini sio ilani (manifesto), hata Rais Mkapa alilisemaga hilo la ilani isiyotekelezeka. Kama ilani zingekuwa zinatekelezwa kwa 100& tangu 1961 sasa hivi kusingekuwa na kijiji Tanzania kisichokuwa na maji, umeme, kituo cha afya, barabara, shule na kilimo cha jembe la mkono.

Tusimbebeshe Rais Samia zigo la JPM ambalo pengine lilikuwa linatekelezwa ndivyosivyo, lazima tathimini ifanyike kwanza ili kuona lipi liendelee na lipi liahirishwe na lipi liachwe kabisa na lipi liliachwa lakini lifufuliwe na sababu zitolewe. Mfano, Mama Samia atalifanyia haki taifa lake kama ataanza kwa kukamilisha uandikaji wa katiba mpya. Hata mafanikio yanayopatikana lazima yalindwe kwa Katiba na sio kwa kulia machozi ya kumuenzi kiongozi. Katiba ndiyo itoe muelekeo wa taifa kwa kila kiongozi anayepokea kijiti na sio kwa kutumia huruma, machozi, utashi, nyimbo za maombolezo, ukanda, mizengwe, udini na ukabila wa kundi fulani.
 
Pia naomba mama awateue pia Maria Sarungi pamoja na Fatuma Karume kwenye baraza lake la mawaziri.
Mama anateua watu watakamsaidia kuchapa kazi kwa weledi na kwa ufasahaa

Nama hateui mashosti wakupiga nao umbea na kuchambana ...ebooooo!!
 
Amenikera Sana aliposema atatekeleza maono ya Magufuli. Kwa mtu ambaye ni bingwa wa uchumi maono ya Magufuli hayana mpangilio.
hatakiwi atekeleze maono ya Magufuli bali anatakiwa akatekeleze maono ya Rais SSH, lazima watu tuelewane hapo maana enzi za nyerere, mwinyi, mkapa, kikwete na magufuli zimeshapita, sasa tunae Rais mwingine. Inatia kichefuchefu kama vichwani bado watu wanaongelea Rais JPM.
 
Kama ilivyokuwa 2015 kwa JPM, sasa hivi tena Chadema wako bize kumsifia, kumfundisha na kumpa maelekezo mbalimbali Rais Samia bila kujua kuwa huyo ni Rais anayetokana na CCM na anatekeleza ilani ya CCM.

Godbless Lema, Tundu Lissu hawazungumzii kabisa maendeleo ya Chadema, wao ni bize kumpangia cha kufanya Rais Samia.!

Tundu Lissu ni kaimu mwenyekiti wa Chadema lakini hutakaa usikie akiiongelea wala kuitangaza Chadema popote. Kwani haoni kaimu mwenyekiti wa CCM Philip Mangula anavyokinadi chama chake?

Tundu Lissu ni mtanzania lakini hutakaa usikie popote akizungumzia mazuri ya nchi yake, yeye ni kuchafua tu nchi yake.
Lissu ndiyo kula yake hiyo, hana uchungu na Nchi
 
Lengo la wapinzani hasa wa huko twitta ni kumuingiza chaka Rais.

Mwanzoni walikuwa wanalaumu kuwa Rais atamteua Nchimbi kuwa nakamo baada ya ubashiri wao kutotimia na Dr Mpango kuteuliwa wanamlaumu Rais na kudai heri Nchimbi kuliko Mpango. Huu ni utnibitisho mmojawapo kuwa hao wapinzani hawana nia njema na Rais na wana lengo la kumyumbisha.

Ni wazi Rais alikuwa anayo kichwani mwake majina kadhaa lakini kwa kuwa amejinyenyekeza mbele ya Mungu na watanzania wengi wanamuombea, nwenyezi Mungu amemsaidia kupata mtu sahihi zaidi Dr Mpango.

Wapinzani wanataka Rais afuate maelekezo yao namna ya kuongoza nchi badala ya kutekeleza maelekezo ya chama chake!

Dr Mpango ndiye aliyesimamia utengenezaji wa long term perspective plan wa miaka 15 ( 2011-2025) ambao ulivunjwavunjwa katika mipango mitatu ya miaka mitano mitano na amesimamia utekelezaji wa mipango miwili tayari na sasa alikuwa anasimamia mpango wa tatu na wa mwisho ambao ndio unaanza mwaka huu. Yeye atamsaidia sana Rais kukamilisha miradi yote inayoendelea kutekelezwa.
 
Hivi kwa akili zenu miaka hii 4 mnadhani raisi Samia ataahidi nini zaidi ya kutekeleza tu miradi iliyoachwa!!?..mama samia ili aweze kufaulu inabidi anate mulemule walipokuwa na mzee pombe..
akipita mulemule mwa JPM itamlazimu pia kuwa na uchaguzi kama wa 2020 kwenye uchaguzi ujao 2025.
 
Lengo la wapinzani hasa wa huko twitta ni kumuingiza chaka Rais.

Mwanzoni walikuwa wanalaumu kuwa Rais atamteua Nchimbi kuwa nakamo baada ya ubashiri wao kutotimia na Dr Mpango kuteuliwa wanamlaumu Rais na kudai heri Nchimbi kuliko Mpango. Huu ni utnibitisho mmojawapo kuwa hao wapinzani hawana nia njema na Rais na wana lengo la kumyumbisha.

Ni wazi Rais alikuwa anayo kichwani mwake majina kadhaa lakini kwa kuwa amejinyenyekeza mbele ya Mungu na watanzania wengi wanamuombea, nwenyezi Mungu amemsaidia kupata mtu sahihi zaidi Dr Mpango.

Wapinzani wanataka Rais afuate maelekezo yao namna ya kuongoza nchi badala ya kutekeleza maelekezo ya chama chake!

Dr Mpango ndiye aliyesimamia utengenezaji wa long term perspective plan wa miaka 15 ( 2011-2025) ambao ulivunjwavunjwa katika mipango mitatu ya miaka mitano mitano na amesimamia utekelezaji wa mipango miwili tayari na sasa alikuwa anasimamia mpango wa tatu na wa mwisho ambao ndio unaanza mwaka huu. Yeye atamsaidia sana Rais kukamilisha miradi yote inayoendelea kutekelezwa.
hakuna anayesema Mh. Mpango hafai, ila tunahoji alichofanya kati ya jina lake kutajwa na kuapishwa kwake basi na sio kingine. Lakini watu wasidhani kuwa Rais Samia hana anachojua kuhusu mambo yalivyokuwa yakiendeshwa na JPM, usifikirie kuwa yooooote ya JPM yalikuwa yakimfurahisha, usifikirie yeye halijui baya na zuri kwa taifa na wananchi wa ngazi zote. Asitokee mtu anataka kumpima mama Samia kwa kutumia JPM. Mfano, ripoti ya CAG inasema shirika la ndege linaingiza hasara ya 6b kila mwaka, kwahiyo mnataka mama Samia afanye nini kwenye shirika kama hili? lazima kuna namna tofauti atafanya kuliko alivyofanya mtangulizi wake. Hizi ni sawa hata askari waliostaafu wasilipwe mafao yao kwakuwa tunataka kujenga uwanja wa mpira Dodoma? lazima kuna mambo ataachana nayo kama sio kuyapunguzia kasima.
 
Ukiingia kwenye siasa, Ph.D unaweka pembeni.

Maneno mengine ni kwa "public consumption" zaidi.

Mpango ni bureaucrat, si mwanasiasa, labda ana overcompensate.

Huyo Nyerere mwenyewe aliyeianzisha CCM alisema CCM si mama yake, ikimzingua anaiacha.
Sija wahi mwona Nyerere akivaa nguo zao za kijani sijui kwanini.....
 
Amepotoka vibaya sana , mwanxo tu unaanza na ujinga wa kuonyesha mwelekeo wa kukandamiza demokrasia na kuchukia vyama vya upinzani , huo ni ujinga wa hali ya juu na utamkosti , time will tell for sure .
 
Nilidhani yeye anakwenda kufanya yale atakayoagizwa na Rais kuyafanya, je ilikuwa sawa kuahidi yale aliyoyaahidi kufanya kabla ya kujua muelekeo wa boss wake?

UPo sahihi hata mimi nimeshanga akuw atafanya atatenda, nilitegemea tu kusema NITAKUWA MTIIFU NA MNYENYE KEVU KWA KAZI ZOTE NITAKAZO PANGIWA NA RAISI.
 
Alivuka mipaka na Kuongea utumbo. Mara atishie upinzani. Mara alete swaga za kuendeleza udikteta za MWIZI JIWE. Yaani utadhani ate uliwa na familia ya Meko. Ali ni boa.
 
Kama tunavyojua Bi Mkubwa ana kazi kubwa ya kuhakikisha anakidhi matarajio ya Watanzania lakini pia kuhakikisha serikali inakua na utulivu ukizingatia mara zote kunakuaga na makundi ya mitazamo kinzani na kila kundi linataka lipewe kipaumbele ktk teuz ili kuwa na usemi na hapo mbilinge ndipo zinapoanzaga.

Nimemuelewa sana Bi Mkubwa ktk uteuzi wa Mzee Mpango kwa kuzingatia alikua mtu muhimu mno ktk utawala uliopita. Naamini huyu alikuwa ndio mkono wa kulia wa Mzee Pombe na hata miradi yote mikubwa kwa midogo huyu jamaa alikua ni kiungo kwa hiyo kitendo cha yeye kumuweka karibu na upeo wake ina maana itakua rahisi sana kujua mienendo yake na kumdhibiti ukizingatia makamu wa rais ktk siasa zetu mara nying ni MTU wa kupangiwa kazi.

Bi Mkubwa katumia busara sana kumtoa Mpango katika post ambayo mara zote kila mtawala huwa anamuweka anayemuamini. Endapo angemtoa bila kutumia aina hii ya busara, bila shaka kungekuwa na maneno ktk kila kundi lakini kitendo cha Bi Mkubwa kutumia mbinu hii walau timu wafiwa wamemuunga mkono na timu twita wanalalamika.

Uhuru wa kujieleza na nina haki ya kusikilizwa kwa mujibu wa katiba ya JMT.
 
Mwambieni Madame President afute zile tozo za Youtube na afanye mpango wa Paypal vijana tujiajiri
 
Maweee!!!
😳😳😳😳😳😳😎😅

1617179486310.png
 
Back
Top Bottom