Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Nilimshangaa aliposema " Nitakuwa mwana CCM hadi mwisho wa maisha yangu" hii kauli haikutakiwa kutolewa na mtu mwenye PhD
Hata baba wa taifa ambae ndiye mwenye CCM yake aliwahi kusema CCM sio baba yangu wala mama yangu naweza kutoka, sembuse yeye. Jamani tujifunze kuweka akiba ya maneno, iko siku itatufaa pasipo kutarajia
 
Mods wana nongwa sana kila nikipandisha Uzi jukwaa LA siasa wanaunganisha na nyuzi nyingine au labda sina vigezo vya kupandisha nyuzi jukwaa LA siasa???
 
Hajahutubia Mkuu..

Ameliaga tuu bunge Chief

Ndio maana amesema atalimiss sana bunge!..sasa ulitaka aondoke kimya kimya ilihali wameshirikiana wote kule Bungeni kwa kipindi chote? How?
Kuliaga bunge unasema maneno machache tu na siyo hotuba ndefu kama ile halafu mwisho akaboronga. Eti hakupendezwa na wapinzani kupinga bajeti yake. hapo alikuwa anatoa ujumbe gani kwa Taifa? mwanaCCM ni MwanaCCM tu. Wameambukizana chuki za kisiasa zisizo na tija yoyote.
 
Hahahah sawa Mkuu...

Ila kwa tamaduni zetu za kiAfrika..sio jambo nzuri kuwakimbia wenyeji kimya kimya bila kuaga au kutoa hata neno la shukrani.

Sasa kama kuna mengine aliyasema na yakavunja taratibu zilizokuwepo nahisi kazidisha sasa tena kaboronga kabisa! na haifai
 
Nilidhani yeye anakwenda kufanya yale atakayoagizwa na Rais kuyafanya, je ilikuwa sawa kuahidi yale aliyoyaahidi kufanya kabla ya kujua muelekeo wa boss wake?
alichemka lakini pia ni kiwewe cha kutoamini kama angefikia ile post
 
Hahahah sawa Mkuu...

Ila kwa tamaduni zetu za kiAfrika..sio jambo nzuri kuwakimbia wenyeji kimya kimya bila kuaga au kutoa hata neno la shukrani.

Sasa kama kuna mengine aliyasema na yakavunja taratibu zilizokuwepo nahisi kazidisha sasa tena kaboronga kabisa! na haifai
Hakuna anayekataa mtu mliyekuwa naye kukuaga. Tatizo kadiri unavyokuwa na maneno mengi utajikuta unaropoka hata ulichokuwa nacho moyoni kama siri. Hotuba ya Mpango ilikuwa nzuri sasa mwishoni akalikoroga, eti hakupenda na aliwashangaa wapinzani kupinga hotuba yake ya bajeti na eti wapinzani wahame tu vyama vyao wajiunge CCM na yeye atakuwa mwana CCM mpaka kufa. Hayo maneno ya mwisho yalikuwa na maana gani na akikuwa serious huku amekunja uso. Yeye kwa cheo kile siyo kwenda kuitumikia CCM bali Tanzania. Mengine ni ya kumezea tu . Wakati wote elewa kwamba siyo lazima kila mmoja akubaliane na wewe. Na hata waliopinga bajeti yake nakumbuka hoja yao ilikuwa ni kwa nini tunapitisha bajeti halafu inatekelezwa kwa 34% tu kwa kukosa fedha. Sasa si ni afadhali tupitisha bajeti ndogo inayotekelezeka kuliko hayo matrilioni ambayo hayana uhalisia. Eti ndio yeye aseme walinkwaza sana! na wasirudie tena.
 
Kikubwa ni dhamira alokuwa nayo katika taifa lake. sioni alipokosea kwenye kuongea pasina kujali kama ataangulia au lah.

Nasepa😎
Tatizo wewe hukumsikiliza vizuri. Kuoga kwa wenzake sawa. Sasa lile na kusema wapinzani walimkwaza kwa kukataa bajeti yake lilikuwa na ulazima gani kuliongea? Halafu eti haoni sababu ya kuwepo upinzani na wapinzani wanatakiwa waondoke kwenye vyama vyao wahamie CCM na wasiwe wanapinga bajeti za serikali. Ujinga huu haukuwa na ulazima wowote.
 
Io aliitoa muda gani mkuu??? mana mimi nilisikiliza maelezo yake. anyway kama aliongea hivo (kuukataa upinzani) basi alikosea hakutakiwa kuiorodhesha upinzani in negative. the rest dhamira ya kuipambania taifa ilikuwa sahihi tu.
 
Mhe Mama Samia, uteuzi huu ni wa kihistoria - for sure umeongozwa na Mungu. Umepata binadamu asiyekuwa na makundi wala makuu "Rafiki wa kila mtanzania".

Tutawapa ushirikiano ndani ya CCM na nje ya CCM
 
Io aliitoa muda gani mkuu??? mana mimi nilisikiliza maelezo yake. anyway kama aliongea hivo (kuukataa upinzani) basi alikosea hakutakiwa kuiorodhesha upinzani in negative. the rest dhamira ya kuipambania taifa ilikuwa sahihi tu.
Kama ulimsikiliza alisemaje juu ya upinzani? Angalia hata Gazeti la Mwanachi la leo 31/013/2021 ukurasa wa kwanza. Au huwa hujui namna ya kumsikiliza msemaji. Usiwe unachati wakati unasikiliza hotuba muhimu.
 
Nilidhani yeye anakwenda kufanya yale atakayoagizwa na Rais kuyafanya, je ilikuwa sawa kuahidi yale aliyoyaahidi kufanya kabla ya kujua muelekeo wa boss wake?
aache kauli ya watanzania wanyonge, hili lilikuwa kichaka cha meko kutunyonya
 
Hakuna anayekataa mtu mliyekuwa naye kukuaga. Tatizo kadiri unavyokuwa na maneno mengi utajikuta unaropoka hata ulichokuwa nacho moyoni kama siri. Hotuba ya Mpango ilikuwa nzuri sasa mwishoni akalikoroga, eti hakupenda na aliwashangaa wapinzani kupinga hotuba yake ya bajeti na eti wapinzani wahame tu vyama vyao wajiunge CCM na yeye atakuwa mwana CCM mpaka kufa. Hayo maneno ya mwisho yalikuwa na maana gani na akikuwa serious huku amekunja uso. Yeye kwa cheo kile siyo kwenda kuitumikia CCM bali Tanzania. Mengine ni ya kumezea tu . Wakati wote elewa kwamba siyo lazima kila mmoja akubaliane na wewe. Na hata waliopinga bajeti yake nakumbuka hoja yao ilikuwa ni kwa nini tunapitisha bajeti halafu inatekelezwa kwa 34% tu kwa kukosa fedha. Sasa si ni afadhali tupitisha bajeti ndogo inayotekelezeka kuliko hayo matrilioni ambayo hayana uhalisia. Eti ndio yeye aseme walinkwaza sana! na wasirudie tena.
sijui atafanya nini kama boss wake atachukua mkondo tofauti dhidi ya wapinzani na upinzani nchini. Angesubiri basi japo kidogo ili aone muelekeo wa boss wake kabla ya kuanza kutoa misimamo na maazimio yake hata kabla ya kura kuhesabiwa wala kuapishwa.
 
Kila neno lingepingwa tu. Ungependa aseme nini au angeongea nao kwa ishara kama trafiki anayeongoza magari!
 
Back
Top Bottom