Pre GE2025 Rais Samia Suluhu Hassan atashinda urais 2025 asubuhi na mapema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama katiba itakuwa bado ni hii tuliyonayo pamoja na tume ya uchaguzi hii tuliyonayo basi ni wazi kwamba hapatakuwa na uchaguzi bali kiini macho tu.
 
Ndio umemaliza ama unaendelea?
 
Iingizwe kwenye hansard ipi ya masaburi yako labda.
Rais anayeongoza watanzania wauawe ili wajomba zake wa nje ya nchi waingie na kujenga mahoteli ya kitalii ?
Rais anayeratibu Rushwa na kugawa raslimali za taifa kwa wajomba wake wa Nje ya nchi hadi ndege ya rais? iliyonunuliwa na kodi za watanzania Kuzuiliwa na rais kujidhalilisha kurudi kwa public transport?
Rais anayehamasisha rushwa kwa viongozi wenzake kwamba kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake?
Huyu atapita kwa mbinde na rushwa tu! ama sivyo itabidi atengeze kesi milioni 60 za uhaini.
 
Hatujakataa ushindi ndugu mleta mada, ila mbona bado ni mapema sana? Bado tupo kwenye DIPI ! 😄
 
Tulia hizi ni rumours tu
 
Haha yaan chama hakina ofisi, hakina hata kiongoz mmoja wa kata au kijiji kitashindaje uchaguzi, na ujue huko vijijin mambo ya mitandao ya kijamii hawana ,hata network kupatikana shida, utawasiliana kwa njia gani ?
 
Haha yaan chama hakina ofisi, hakina hata kiongoz mmoja wa kata au kijiji kitashindaje uchaguzi, na ujue huko vijijin mambo ya mitandao ya kijamii hawana ,hata network kupatikana shida, utawasiliana kwa njia gani ?
Hakuna mwenye tatizo na watu waliolala, tunataka uchaguzi uheshimiwe ili hao wanaoshindia huko kwenye ofisi zwvijijini washindie huko huko. Zamani mlikuwa na propaganda kuwa vijana hawapigi kura, wakawa wanajitokeza kwa wingi mkaamua kuleta magari ya kuwasha.

Sasa hivi mnajifanya sijui mnashindia vijijini, cha ajabu lazima mlete mabox ya kura zilizojaa, na kulazimisha kupita bila kupigwa. Kwa kukusaidia tu, hata wapinzani wasipopata hata kura moja huko vijijini unakosema, bado kwa maeneo ya mjini wanaweza kuwa na kura zaidi ya 40% za urais, na huko bungeni wana uwezo wa kuvuka 40% ambayo itawanyima CCM 2/3 ya kufanya maamuzi watakavyo. Ukiona kuna wizi wa kura sio wanapenda, ila ukweli ndio huo. CCM sio chama cha kizazi hiki, labda useme huko vijijini wako wazee tu.
 
Viva Samia
Viva CCM
 
Urais wa Pemba au?
Hata wanawake wenzake hawataki hata kumsikia
 
Kama kawaida
 
UCHAGUZI AU UCHAFUZI?TANZANIA HAKUNA UCHAGUZI MIAKA YOTE HUWEZI KUWA NA UCHAGUZI WAKATI TUME INAYOSIMAMIA UCHAGUZI SIO HURU NI TUME YA CHAMA CHAKO VIONGOZI NA WATENDAJI WA TUME UNAWATEUA WEWE NA KUWALIPA MISHAHARA .
HUWEZI KUWA NA UCHAGUZI HURU WAKATI KATIBA HAIRUHUSU KUHOJI MATOKEO YA URAIS HATA KAMA UCHAGUZI UNA
DOSARI
HUWEZI KUWA NA UCHAGUZI HURU WAKATI WASIMAMIZI WOTE WA UCHAGUZI NI MAKADA WA CHAMA CHAKO NA WEWE NDIO UNA WATEUA NA KUWALIPA MISHAHARA .
 
Wadau nataka niseme.
Mama Ssmia ni lazima atashinda Urais mwaka 2025.
Kijiti alichorithi toka kwa mtangulizi wake kilikuwa kizito.
Mbowe alikuwa lupango akiwa na kesi ya uhaini.
Akipokea kijiti, mtu akiwa CHADEMA ni kama mtu anayenuka kinyesi.
Hata wana CCM usipounga mkono juhudi za Mwenyekiti unabambikwa kesi ya uhujumu.
Wawekezaji walikuwa wanatokomea kwa kiwango cha kutisha. Wafanyabiashara wengi walikuwa wanarudisha leseni za biashara.
Kwa kifupi tulikuwa tunaishi in a Police State.
Sasa hivi watu wana uhuru wa kuongea bila wasi wasi wowote.
Na sasa hivi watu wanaanzisha biashara kulingana na matakwa yao.
Kwa nini tusimpe mama MITANO TENA?
 
Yote uliyosema ni kweli kabisa lakini sijui ni kwa nini wananchi wengi wa kawaida hawamkubali.

Nafikiri watanzania wengi wanapenda siasa alizofanya jpm na hizi anazofanya Makonda.
Zile siasa za kumkemea mwenye nacho na kumpetipeti mnyonge.
Siasa hizo Rais Samia Hana. Jambo linalofanya wananchi wamwone sio rais wa wanyonge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…