Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

Hayati baba wa taifa alitawala miaka 23....mbona inasemwa ni awamu moja tu?!!!

Ndg.Polepole ataacha lini UROPOKAJI wa kitoto?!!!
 
Angetuundia tume yakuchunguza kifo cha magufuli kidogo sisi sukuma geng tungemuuelewa,hiii kupita hivi kimya kimya na anashuhudia magufuli akinangwa na wapumbavu wachache na hasemi chochote tunaumia sana.tunamuona naye ni walewale chawa
 
Awamu zinahesabika kwa vichwa vya marais so as to document legacy correctly! Hata akikaa mwezi, AWAMU IMEISHA NA LEGACY YAKE TAYARI, HUWEZI KUIUNGANISHA NA YA RAIS MWINGINE.
Swadaktaaaa! Ndiyo maana Zanzibar wapo awamu ya 8 kwasbb kuna vichwa 8 vimekaa ikulu ya Zanzibar
 
Ni aibu kubwa kwake ndg.Polepole...

Ukatibu wake mwenezi haukumpa elimu ya kujua kuwa AWAMU inahesabiwa kwa KICHWA ofisini?!!!!

Aibu kubwa kwa MROPOKAJI HUYU....

SIEMPRE CCM🙏
Awamu ni miaka mitano. Awamu moja inaweza tawaliwa hata na marais wawili.

Assume ndani ya miaka mitano marais watatu wamekufa, hivyo ndani ya miaka mitano tunakuwa na marais wanne. Je tutasema tumekuwa na awamu nne ndani ya miaka mitano. Au tumekuwa na marais wanne ndani ya miaka mitano(awamu moja)?
 
Akili ndogo bhana!Badala ya kujadili mambo madogo ya awamu tujadili jinsi ya kunusuru Taifa hili na ufisadi wa kutisha unaofanywa na serikali ya CCM ya Samia.
202112.jpg
 
Wazee wa legacy wanataka kulazimisha agenda zao[emoji848].
Awamu ni kipindi kimoja cha urais kwa miaka 5 au 10 kama atachachaguliwa tena na kufikia kiwango cha juu kukaa kikatiba kama rais.Rais wa sasa ni rais wa pili wa awamu ya tano...na itaendelea hivyo iwapo rais anapatikana kwa njia nyingine tofauti na uchaguzi...swali hapa kama tunasema ni awamu ya 6 je katiba inasemqje kuhusu muda wa rais kukaa madarqkani kabla ya uchaguzi...je rais anqweza kukaa madarakqni kwa miqkq 4 uchaguzi ukafanyikq?
 
Rais Samia ni awamu ya 6. Kinachohesabu awamu sio kutoka Uchaguzi mmoja na mwingine au kutoka miaka 5 au 10. Kinachotambulisha awamu ni Jina la Rais. Nyerere ni awamu ya kwanza ingawa alitawala karibia miaka 27. Kwahiyo ikitokea Mama Samia leo akaacha Urais kabla ya 2025 akachukua Rais mpya basi tutahesabu awamu ya 7. Jina la Rais ndio awamu yenyewe.
 
Awamu ni kipindi kimoja cha urais kwa miaka 5 au 10 kama atachachaguliwa tena na kufikia kiwango cha juu kukaa kikatiba kama rais.Rais wa sasa ni rais wa pili wa awamu ya tano...na itaendelea hivyo iwapo rais anapatikana kwa njia nyingine tofauti na uchaguzi...swali hapa kama tunasema ni awamu ya 6 je katiba inasemqje kuhusu muda wa rais kukaa madarqkani kabla ya uchaguzi...je rais anqweza kukaa madarakqni kwa miqkq 4 uchaguzi ukafanyikq?
Ndio maana tunataka katiba mpya.
 
Sio kosa la wasomi wala suala la kujiamulia.Bali ni matakwa ya katiba, Kuwa Rais akipokea kijiti ndani ya miaka isiýopungua mitatu hiyo itakuwa awamu yake
 
Kama angepokea kijiti ndani ya miaka miwili iliyobaki,Basi ingebaki kuwa awamu ya tano,Na angeruhusiwa kugombea mara mbili yaani 2025 na 2030
 
Kumradhi:
Naomba nitangulie kusema kwamba kati ya Jambo kubwa linaloigharimu nchi yetu ni kukosekana wasomi 'very competent'; naweza kusema wasomi wetu wengi kwenye hili Taifa ni product ya 'Q & A' kwenye vitini vya hapa na pale. Taifa letu halina wasomi wenye 'natural thinking ability' badala yake tuna wasomi wengi wanao reason kwa kuambaambaa na upepo wa wakati ule. Again, kumradhi!
Kwamba 'wasomi' wetu wakifanikiwa ku"term" hizi awamu basi kero zetu kuu watanzania zitakuwa zimetatulika?
 
Achana na mambo ya awamu, wewe fahamu aliyepo ni Rais wa sita na hiyo inatosha, fuatilia mambo ya msingi.
 
Mods naheshimu msimamo wenu na kazi yenu ya kuunganisha nyuzi zenye mfanano wa aina fulani. Lakini naomba kwa upole na unyenyekevu nkubwa msiunganishe huu uzi na nyingine. Nimeomba, asante sana!

Wana JF wa CCM na Upinzani na wasio na chama, Je ni kweli Rais Samia ni Rais wa awamu ya 6 ama 5?

Kumradhi:
Naomba nitangulie kusema kwamba kati ya Jambo kubwa linaloigharimu nchi yetu ni kukosekana wasomi 'very competent'; naweza kusema wasomi wetu wengi kwenye hili Taifa ni product ya 'Q & A' kwenye vitini vya hapa na pale. Taifa letu halina wasomi wenye 'natural thinking ability' badala yake tuna wasomi wengi wanao reason kwa kuambaambaa na upepo wa wakati ule. Again, kumradhi!

Nasema hivyo kwa sababu, hadi sasa hakuna msomi yeyote wa chuo chochote ama kutoka popote ambaye amewahi ku 'challenge' kisomi uwepo wa awamu ya 6 badala ya kuitwa awamu ya 5.

Awamu ya uongozi inakuwa na elements kuu tatu:
1. Uchaguzi wa urais na makamu wake
2. Uchaguzi wa wabunge kwenye majimbo pia na viti maalum
3. Uchaguzi wa Madiwani pia viti maalum.

Ilivyo ni kwamba, lazima Rais anayegombea awe na makamu wake. Logic ya kuwa na makamu ni kwamba, in case of anything unusual basi makamu wa Rais ndio anashika usukani na kuendelea. Kwa maneno mengine makamu wa Rais ni Rais.

Kuna nyakati Rais anakuwa na hali mbaya ya ki afya hivyo Makamu wake ndio anasimama kwenye nafasi yake hivyo ni Rais.

Kuna wakati mwingine Rais anakuwa yupo nje ya mipaka ya nchi yake hivyo anayesimama kwenye nafasi yake ni makamu wa Rais hivyo ni Rais.

Kipekee sana, kuna mifano mingi mno inayohalalisha kuwa makamu wa Rais ni Rais kwa maneno mengine kiasi kwamba hawezi kujitenga na awamu alioombea kura.

Kama hivyo, ni lini Rais Samia aliomba kura ya kuwa Rais wa nchi hii? Hajawahi, bali aliomba ya kuwa makamu wa Rais wa awamu ya 5.

Ni lini Rais Samia aliomba kura ya wabunge wake? Ameomba akiwa awamu ya 5.

Na Madiwani je? Pia akiwa awamu ya 5.

Kuna mambo mengi yanayoelezea kiwaziwazi kuwa Rais Samia ni Rais wa awamu ya 5 na sio ya 6.

Awamu ya urais ni package (Kuomba kura ukiwa na makamu wako + Kuunda Bunge Jipya + Kuteua Waziri Mkuu mpya + Kuteua speaker qa Bunge mpya) na kuendelea!

Ndio maana, nasisitiza tena ndio maana Magufuli alipochaguliwa awamu yake ya Kwanza aliunda Serikali yake kuanzia Bunge, Madiwani, na kwingine kote.

Alipochaguliwa awamu yake ya pili alifanya hivyo hivyo kama alivyofanya hapo awamu ya Kwanza, yaani as if anaanza kitu kipya tena kama vile hakuwepo.

Sasa, Rais Samia yeye ameunda Serikali yake? Ndio aliunda wakisaidiana na Rais Magufuli na ndio maana hata baada ya Magufuli kufariki aliendelea na serikali ile ile iliyopo maana ndio Serikali yake.

Kwa sasa kama Rais Samia akigombea mwaka 2025 - 2030 basi anakuwa rasmi ni Rais wa awamu ya 6 (sita).

Nawaasa wasomi wa Taifa hili wa kila kada, amkeni kwa ajili ya Taifa lenu!
Kwahiyo Magufuli kaongoza Tanzania kwa awamu mbili? Na kama ni hivyo basi hadi sasa tupo kwenye awamu sijui ya kumi na ngapi!
 
Awamu zinahesabika kwa vichwa vya marais so as to document legacy correctly! Hata akikaa mwezi, AWAMU IMEISHA NA LEGACY YAKE TAYARI, HUWEZI KUIUNGANISHA NA YA RAIS MWINGINE.
Sawa kabisa
 
Awamu haziko kikatiba bali ni jadi tu. Awamu zimezoeleka kumaanisha kipindi cha Rais fulani madarakani. Hata kama Rais Samia alikuwa VP wakati wa Magufuli. Kwa sasa yeye ni Rais kamili wa JMT na kwa hivyo ni Rais wa awamu ya 6.
 
Mods naheshimu msimamo wenu na kazi yenu ya kuunganisha nyuzi zenye mfanano wa aina fulani. Lakini naomba kwa upole na unyenyekevu nkubwa msiunganishe huu uzi na nyingine. Nimeomba, asante sana!

Wana JF wa CCM na Upinzani na wasio na chama, Je ni kweli Rais Samia ni Rais wa awamu ya 6 ama 5?

Kumradhi:
Naomba nitangulie kusema kwamba kati ya Jambo kubwa linaloigharimu nchi yetu ni kukosekana wasomi 'very competent'; naweza kusema wasomi wetu wengi kwenye hili Taifa ni product ya 'Q & A' kwenye vitini vya hapa na pale. Taifa letu halina wasomi wenye 'natural thinking ability' badala yake tuna wasomi wengi wanao reason kwa kuambaambaa na upepo wa wakati ule. Again, kumradhi!

Nasema hivyo kwa sababu, hadi sasa hakuna msomi yeyote wa chuo chochote ama kutoka popote ambaye amewahi ku 'challenge' kisomi uwepo wa awamu ya 6 badala ya kuitwa awamu ya 5.

Awamu ya uongozi inakuwa na elements kuu tatu:
1. Uchaguzi wa urais na makamu wake
2. Uchaguzi wa wabunge kwenye majimbo pia na viti maalum
3. Uchaguzi wa Madiwani pia viti maalum.

Ilivyo ni kwamba, lazima Rais anayegombea awe na makamu wake. Logic ya kuwa na makamu ni kwamba, in case of anything unusual basi makamu wa Rais ndio anashika usukani na kuendelea. Kwa maneno mengine makamu wa Rais ni Rais.

Kuna nyakati Rais anakuwa na hali mbaya ya ki afya hivyo Makamu wake ndio anasimama kwenye nafasi yake hivyo ni Rais.

Kuna wakati mwingine Rais anakuwa yupo nje ya mipaka ya nchi yake hivyo anayesimama kwenye nafasi yake ni makamu wa Rais hivyo ni Rais.

Kipekee sana, kuna mifano mingi mno inayohalalisha kuwa makamu wa Rais ni Rais kwa maneno mengine kiasi kwamba hawezi kujitenga na awamu alioombea kura.

Kama hivyo, ni lini Rais Samia aliomba kura ya kuwa Rais wa nchi hii? Hajawahi, bali aliomba ya kuwa makamu wa Rais wa awamu ya 5.

Ni lini Rais Samia aliomba kura ya wabunge wake? Ameomba akiwa awamu ya 5.

Na Madiwani je? Pia akiwa awamu ya 5.

Kuna mambo mengi yanayoelezea kiwaziwazi kuwa Rais Samia ni Rais wa awamu ya 5 na sio ya 6.

Awamu ya urais ni package (Kuomba kura ukiwa na makamu wako + Kuunda Bunge Jipya + Kuteua Waziri Mkuu mpya + Kuteua speaker qa Bunge mpya) na kuendelea!

Ndio maana, nasisitiza tena ndio maana Magufuli alipochaguliwa awamu yake ya Kwanza aliunda Serikali yake kuanzia Bunge, Madiwani, na kwingine kote.

Alipochaguliwa awamu yake ya pili alifanya hivyo hivyo kama alivyofanya hapo awamu ya Kwanza, yaani as if anaanza kitu kipya tena kama vile hakuwepo.

Sasa, Rais Samia yeye ameunda Serikali yake? Ndio aliunda wakisaidiana na Rais Magufuli na ndio maana hata baada ya Magufuli kufariki aliendelea na serikali ile ile iliyopo maana ndio Serikali yake.

Kwa sasa kama Rais Samia akigombea mwaka 2025 - 2030 basi anakuwa rasmi ni Rais wa awamu ya 6 (sita).

Nawaasa wasomi wa Taifa hili wa kila kada, amkeni kwa ajili ya Taifa lenu!
Ukiniuliza mie ngwini nitakwambia ni awamu ya tano period.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom