Mods naheshimu msimamo wenu na kazi yenu ya kuunganisha nyuzi zenye mfanano wa aina fulani. Lakini naomba kwa upole na unyenyekevu nkubwa msiunganishe huu uzi na nyingine. Nimeomba, asante sana!
Wana JF wa CCM na Upinzani na wasio na chama, Je ni kweli Rais Samia ni Rais wa awamu ya 6 ama 5?
Kumradhi:
Naomba nitangulie kusema kwamba kati ya Jambo kubwa linaloigharimu nchi yetu ni kukosekana wasomi 'very competent'; naweza kusema wasomi wetu wengi kwenye hili Taifa ni product ya 'Q & A' kwenye vitini vya hapa na pale. Taifa letu halina wasomi wenye 'natural thinking ability' badala yake tuna wasomi wengi wanao reason kwa kuambaambaa na upepo wa wakati ule. Again, kumradhi!
Nasema hivyo kwa sababu, hadi sasa hakuna msomi yeyote wa chuo chochote ama kutoka popote ambaye amewahi ku 'challenge' kisomi uwepo wa awamu ya 6 badala ya kuitwa awamu ya 5.
Awamu ya uongozi inakuwa na elements kuu tatu:
1. Uchaguzi wa urais na makamu wake
2. Uchaguzi wa wabunge kwenye majimbo pia na viti maalum
3. Uchaguzi wa Madiwani pia viti maalum.
Ilivyo ni kwamba, lazima Rais anayegombea awe na makamu wake. Logic ya kuwa na makamu ni kwamba, in case of anything unusual basi makamu wa Rais ndio anashika usukani na kuendelea. Kwa maneno mengine makamu wa Rais ni Rais.
Kuna nyakati Rais anakuwa na hali mbaya ya ki afya hivyo Makamu wake ndio anasimama kwenye nafasi yake hivyo ni Rais.
Kuna wakati mwingine Rais anakuwa yupo nje ya mipaka ya nchi yake hivyo anayesimama kwenye nafasi yake ni makamu wa Rais hivyo ni Rais.
Kipekee sana, kuna mifano mingi mno inayohalalisha kuwa makamu wa Rais ni Rais kwa maneno mengine kiasi kwamba hawezi kujitenga na awamu alioombea kura.
Kama hivyo, ni lini Rais Samia aliomba kura ya kuwa Rais wa nchi hii? Hajawahi, bali aliomba ya kuwa makamu wa Rais wa awamu ya 5.
Ni lini Rais Samia aliomba kura ya wabunge wake? Ameomba akiwa awamu ya 5.
Na Madiwani je? Pia akiwa awamu ya 5.
Kuna mambo mengi yanayoelezea kiwaziwazi kuwa Rais Samia ni Rais wa awamu ya 5 na sio ya 6.
Awamu ya urais ni package (Kuomba kura ukiwa na makamu wako + Kuunda Bunge Jipya + Kuteua Waziri Mkuu mpya + Kuteua speaker qa Bunge mpya) na kuendelea!
Ndio maana, nasisitiza tena ndio maana Magufuli alipochaguliwa awamu yake ya Kwanza aliunda Serikali yake kuanzia Bunge, Madiwani, na kwingine kote.
Alipochaguliwa awamu yake ya pili alifanya hivyo hivyo kama alivyofanya hapo awamu ya Kwanza, yaani as if anaanza kitu kipya tena kama vile hakuwepo.
Sasa, Rais Samia yeye ameunda Serikali yake? Ndio aliunda wakisaidiana na Rais Magufuli na ndio maana hata baada ya Magufuli kufariki aliendelea na serikali ile ile iliyopo maana ndio Serikali yake.
Kwa sasa kama Rais Samia akigombea mwaka 2025 - 2030 basi anakuwa rasmi ni Rais wa awamu ya 6 (sita).
Nawaasa wasomi wa Taifa hili wa kila kada, amkeni kwa ajili ya Taifa lenu!