Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

Sasa kama mama kasema hii ni awamu ya sita wewe ni nani kutuambia hii ni awamu ya tano? Tena usishupaze shingo mpaka akajua kuna watu kama nyingi, ndio atafutilia mbali hio legasi sijui legasi
Kwanza jambo lenyewe la awamu haliko mahali popote kwenye katiba wala sheria. Ni mtu mmoja tu alilitunga nyie mkaruka nalo, awamu awamu. Kama mama kasema ni awamu ya sita basi tembea na hilo. Mwenye awamu hata akiwa kaletwa kwa kuhongwa na rais aliyepo madarakani huyo ni rais halali taga. Nani kakwambia rais ni mpaka sanduku la kura. Kwa sasa raisi wa JMT ni Samia ambaye amesema hii ni awamu ya sita. AWAMU YA SITA

Watu wasomi wa ukweli hawalishwi tango pori!! Awamu zinatengezwa na Uchaguzi Mkuu!! Mama kutaja Awamu ya Sita inawezekana alikosea kama Bin Adam yeyote!!! Kama alikosea kutaja siku za maombolezo sembuse Awamu!!! Tumia bongo brother!! Sio unameza tu!!! Period!!
 
Sawa mkuu, hii na awamu ya 5, rais wetu ni JPM, SSH anamshikia tu!
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hii ni Serikali ya awamu ya 6 hivyo atakayeshindwa kasi yake ataachwa njiani.

Namshukuru sana Rais Samia kwa kuliweka sawa hili kwani jana watu wengi walinibishia nilipowaambia mimi naamini hii ni awamu ya 6.

Kila zama na kitabu chake.

Maendeleo hayana vyama!
You are trying to get in 🤣 don't stop mkuu slow but sure, with full of praise.
 
Mwenye urais kasema yake ni awamu ya 6....full stop! Anataka kutengeneza legacy yake.....

BTW, hivi katiba yetu kwa namna ilivyo sasa ina maana kuna uwezekano Samia akawa Rais kwa miaka 15 (hii almost 5 mpaka 2025 na kumi tena mpaka 2035)?
 
Wana bodi nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania [emoji1241]!!! Naomba hili ninalolitamka hapa liwekwe pia kwenye Hansard za Bunge na Ofisi ya Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa JMT. Kumekuwa na upotoshwaji usio na msingi kutamka ya kwamba hivi sasa tupo katika awamu ya sita ya Uongozi/Utawala wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kitu ambacho si Kweli. Ukweli ni kwamba baada ya kustaafu kwa Mwalimu JK Nyerere Katiba ilitamka wazi kuwa Rais yeyote ataweza kuhudumu kwa mihula miwili tu ya miaka mitano mitano kwa kupitia sanduku la kura. Awamu moja ya uongozi ina maana miaka 10 ya Rais husika mara baada ya kushinda chaguzi zote mbili za kuwania Urais. Hayati Magufuli alikuwa Rais wa tano wa JMT na alikuwa akihudumu katika miaka yake mitano ya mwisho ya awamu yake ya Tano!! Hivyo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya Rais JP Magufuli kufariki; Mama Samia kwasababu alikuwa makamu wa Rais moja kwa moja alipewa (Bila Uchaguzi) nafasi ya kushika nafasi hiyo ya Urais ili kuamlizia uongozi wa miaka mitano ya mwisho ya awamu ya Tano. Kwa unyambulifu huu Mama Samia ni Rais wa Sita anaehudumu awamu ya tano ya Uongozi wa Nchi! Na lazima tukumbuke Awamu za uongozi wa nchi hii huanza kwa kufanyika Uchaguzi Mkuu na Vyama kuuza ilani ya Uchaguzi!! Kwa Mama Samia hakukuwepo na uchaguzi wala unadi wa sera za Chama; kwa sababu Uchaguzi ulishafanyika na Ilani inajulikana; yeye Mama anachofanya sasahivi ni kukamilisha Utawala/Uongozi wa awamu ya Tano tu ila akiwa Rais wa Sita. Awamu ya Utawala/Uongozi wa Awamu ya Sita utaanza baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, na Rais atakaechaguliwa atakuwa Rais wa Saba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bilashaka Tumeelewana. Makosa ya kutaja hii ni
Awamu ya Sita Yasijirudie tena.
Naomba kuwasilisha.
Sasa mkuu kwenye Hansard kule Dodoma, pana umbali gani uache kwenda huko, kuandika hiki! Alafu kusema mama SSH amepewa urais ni kumkosea rais wetu! Mama SSH alikuwepo kwenye ballot paper na alipigiwa kura sambamba na Mwendazake, kwa makusudi haya haya ya kuchukua madaraka nafasi ikiwa wazi! Sasa Wewe unaleta mambo ya kupewaa, hata kama mmeumizwa na msiba wa yesu wenu wa lugola, hebu kuweni serious bhana!
 
Watu wasomi wa ukweli hawalishwi tango pori!! Awamu zinatengezwa na Uchaguzi Mkuu!! Mama kutaja Awamu ya Sita inawezekana alikosea kama Bin Adam yeyote!!! Kama alikosea kutaja siku za maombolezo sembuse Awamu!!! Tumia bongo brother!! Sio unameza tu!!! Period!!
Tango pori or no tango pori unapata wapi kama huna reference. Mahaba ya mwendazake yanakusumbua sana. Hakuna mahali hata pamoja palipoandikwa awamu zinatengenezwa na nani au na nini. Tumekwambia habari ya awamu haipo kwenye msamiati wa katiba au sheria yoyote ile. Aliyelileta kwenye siasa za uchaguzi lilikuwa linamfaa yeye. Sasa usitake kulazimisha kwa logic za kutunga kwamba awamu zinaletwa na uchaguzi. Haijaandikwa mahali popote. Argue kama mtu anayejitambua na mwenye utimamu wa akili. Au peleka bungeni hoja kuwa ssh ni rais wa awamu ya tano. SSH ni rais wa awamu ya sita na hanasibishwi na awamu ya tano. Deal with it
 
Tundu lisu, ww hata ukijikwaa huko Imhotep utamtukana Magu! Utakoma sasa Mungu ameamua kumpumzisha na kumficha mbali na matukano yenu mfyuuuuuu 😡!
Taga lenye kivuli cha mwendazake
 
Kinachosababisha vipindi vya uongozi vihesabike kwa 'awamu' ni hesabu ya kawaida ya kuwahesabu viongozi.
1. Nyerere
2.Mwinyi
3.Mkapa
4.Kikwete
5.Magufuri
6.Samia.

Hivyo wewe ndo unapaswa ujitafakari.
 
Ikitokea huyu naye kafariki na mpango kuingia kisha naye kafariki na mwingine kuingia tutasema tumekuwa na awamu nne ndani ya miaka kumi!!?
Naam, Mbona tulikuwa na awamu moja ndani ya miaka 24?.
 
Mnachamnganya ninyi mapopoma [emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787]! Samia ni rais wa 6 anayehudumu awamu ya 5 period [emoji23]!
Nini kinasababisha tuite awamu ya kwanza,ya pili n.k?
 
Civics ni somo muhimu sana. Hii ni awamu ya tano. Awamu inabadilika pale kunapokua na uchaguzi mkuu na akachaguliwa Rais mwingine
Awamu ni hesabu ya kawaida ya kuhesabu viongozi personally.Haijaloshi katawala kwa miaka 24 (Nyerere),Miaka 10 au sita (Magufuri).

Haijalishi kaingiaje, uchaguzi wa Chama kimoja, uchaguzi wa vyama vingi au Kwa kuiba kura kama fulani.Haijalishi aliingia kwa kura ama kwa kuapishwa baada ya Mtangulizi kufa.

Hivyo Samia ni Rais wa awamu ya Sita.
 
Aisee ..soma vizuri kisha uchanganue vyema mzee..mama ni Rais wa Sita katika Serikali ya awamu ya tano ambayo kimsingi ukomo wake ni 2025...akitokea akagombea tena 2025 atakuwa Rais wa Sita katika Serikali ya awamu ya Sita...2030 Rais ajaye atakuwa Rais wa Saba katika awamu ya Sita.

Mathalani..uchaguzi wa 2020, Angeshinda Tundu Lissu angekuwa Rais wa Sita katika awamu ya tano BADO..na Magufuli angekuwa Rais wa awamu ya tano kwa miaka mitano tu.

Refer USA , Biden ni Rais wa 46 katika awamu ya 44 Kama sikosei..na Trump alikuwa Rais wa 45 katika awamu ya 44, uchaguzi ujao Trump akigombea akashinda anakuwa Rais wa 47 katika awamu ya 45 na akishinda Biden tena atakuwa Rais wa Rais wa 46 katika awamu ya 44.
Kwa maelezo yako,je Nyerere anakuwa na awamu ngapi hapo?.
Jitahidini kuvumilia maumivu,mkubali ihalisia wa Mambo.

Mh Samia ni Rais wa awamu ya Sita.
 
Naichukulia awamu ni kama safari ya basi kutoka Dar- Tandahimba!
Ni kama dereva wa basi akipatwa na la kumpata njiani, afu utingo ashike usukani, huwezi iita hiyo kuwa ni safari mpya au nyingine, unless urudi ulikotoka na kuiandaa nyingine!
Kama mnakerwa sana na kuitwa awamu ya tano
Basi tuiite 'awamu ya tano-sita! Maana inatekeleza maono na ilani ya awamu ya tano!
Kwa sasa tofauti ni kama utingo ndie anayeendesha basi letu la safati ileile ya kwenda Tandahimba😂🤣😂!
Mapuvu ni ruksa😂😂😂!

Hii ni Awamu ya 6 maana awami ni rais.

Nyerere ni awamu ya kwanza japo hakuongoza miaka 10 bali 23...Kwahiyo dhana yako ya vipindi basi umekosea,what if 2020 oct NEC wangetenda haki akaingia lissu,je ingekuwa ya 5 au 6? Kwahiyo awamu sio miaka bali ni rais.
 
Tango pori or no tango pori unapata wapi kama huna reference. Mahaba ya mwendazake yanakusumbua sana. Hakuna mahali hata pamoja palipoandikwa awamu zinatengenezwa na nani au na nini. Tumekwambia habari ya awamu haipo kwenye msamiati wa katiba au sheria yoyote ile. Aliyelileta kwenye siasa za uchaguzi lilikuwa linamfaa yeye. Sasa usitake kulazimisha kwa logic za kutunga kwamba awamu zinaletwa na uchaguzi. Haijaandikwa mahali popote. Argue kama mtu anayejitambua na mwenye utimamu wa akili. Au peleka bungeni hoja kuwa ssh ni rais wa awamu ya tano. SSH ni rais wa awamu ya sita na hanasibishwi na awamu ya tano. Deal with it

Kama Awamu hazipo ( kwa mujibu wa kauli yako) ilitakiwa baada ya Rais Magufuli kufariki uitishwe Uchaguzi Mkuu!! Na Mama angegombea na kama angeshinda kweli angeita hii ni Awamu ya 6. Ili kuondoa Awamu za uongozi inabidi Katiba ibadilishwe na iseme wazi pindi Rais anapofariki Nchi itakuwa chini ya Jaji Mkuu kwa kipindi cha Miezi 6 ili kupisha maandalizi ya Uchaguzi wa kuchagua Rais Mwingine. Sio hii ya kupasiana kijiti ndani ya Awamu then mnaita ni Awamu yenu ndani ya Awamu ilitowapa Madaraka!! Nonsense!!
 
haya waambie waitishe uchaguzi ili mama agombee kama unavyotaka. maana anachokitambuab rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mheshimiwa samia ni kuwa hii ni awamu ya 6. halafu kama kama uko dodoma hebu waone wataalamu wa afya pale kwenye hosptali yetu pendwa hapo dom
 
Tango pori or no tango pori unapata wapi kama huna reference. Mahaba ya mwendazake yanakusumbua sana. Hakuna mahali hata pamoja palipoandikwa awamu zinatengenezwa na nani au na nini. Tumekwambia habari ya awamu haipo kwenye msamiati wa katiba au sheria yoyote ile. Aliyelileta kwenye siasa za uchaguzi lilikuwa linamfaa yeye. Sasa usitake kulazimisha kwa logic za kutunga kwamba awamu zinaletwa na uchaguzi. Haijaandikwa mahali popote. Argue kama mtu anayejitambua na mwenye utimamu wa akili. Au peleka bungeni hoja kuwa ssh ni rais wa awamu ya tano. SSH ni rais wa awamu ya sita na hanasibishwi na awamu ya tano. Deal with it
Neno awamu tumelitumia sana kwa marais wa Zanzibar ambako Karume alikufa na Aboud Jumbe alijiuzulu.
 
Back
Top Bottom