Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

fafanua unataka kusema nini
Haihitaji ufafanuzi kan kwamba nimeleta jambo jipya. Si jipya kama unaijua Zanzibar.

Karume alikufa awamu ikafa. Jumbe akajiuzulu awama ikafa.

Idrisa Abdulwakili alitawala miaka mitano tu awamu ikafa.
 
Kwa maelezo yako,je Nyerere anakuwa na awamu ngapi hapo?.
Jitahidini kuvumilia maumivu,mkubali ihalisia wa Mambo.

Mh Samia ni Rais wa awamu ya Sita.
Awamu hizi zilianza kuhesabiwa mara baada ya Nyerere kutoka madarakani..na na awamu haijalishi miaka ya utawala wa Rais mmoja...ndiposa nikakueleza kuwa mfno JPM wangemuongezea miaka still angekuwa Rais wa tano..katika awamu za vipindi tofauti tofauti, kulingana na muda ambao angeongezewa...

Awamu zinaenda sambamba na vipaumbele vya Serikali kwa wakati huo..ambavyo vinatokana na Ilani ya chama tawala..sasa swali kwako na kwenu vichwa maji..Rais mama Samia anasimamia Ilani ipi na vipaumbele vyake ni vipi katika hio Serikali mnayosema ya awamu ya Sita?

Yeye mwenyewe alsisema anaendela alipoishia Mwendazake ...inamaana vipaumbele na mikakati ya Mwendazake itaendelezwa na Rais Samia.

Akigombea 2025 ndiposa atakuwa na vipaumbele vyake ambavyo vitakuwa vimeratibiwa na kuongozwa na chama chake cha Siasa.
 
Neno lenyewe awamu limekaa vibaya, tulipige chini. Nchi nyingi wanasema Rais wa Kwanza, watatu, watano nk. Kutumia awamu ni kujichanganya .
Ni kweli wamarekani wanasema Rais wa 44 au 43, Kama wangetumia awamu sijui wangekuwa awamu ya ngapi, Ni vizuri itumike Rais wa sita,itapendeza
 
Rais Samia anaweza kuumaliza mjadala wa tuko awamu ipi ya uongozi kama alivyomaliza mjadala wa salamu nyingi nyingi za kidini zisizo na tija katika shuguli za kiserikali alipokuja na salumu yake tofauti kabisa.

Katika suala la awamu ni vyema atumie au yatumike maneno Rais wa sita wa JMT pale kinapotambulishwa kipindi cha utawala wake. Neno awamu lifutike kabisa kutajwa katika shuguli zake kwa sababu kwanza haliko kisheria wala sio lugha rasmi ya kutambulisha kipindi cha utawala bali ilikuwa ni utamaduni tu uliozoeleka.
 
 
Uchaguzi wa vyama vingi ulianza mwaka gani mkuu na mbona hujaulizia nyerere
Na ndo maana kwa Tanzania Awamu ni Rais na sio uchaguzi....mwinyi hakufanyiwa uchaguzi ila uongozi wake tunauita wa Awamu ya Pili....Uchaguzi ni vipindi tu vya kuongoza...Soma Katiba ya Tanzania hakuna sehemu uchaguzi umeitwa Awamu bali wanasema Rais ataongoza kwa kipindi cha miaka miaka mitano...so lugha inayotumika katika uongozi ni kipindi na sio awamu. Awamu ni Rais aliopo madarakani.
 
Mama angesema hii ni awamu ya 5 namalizia kipindi cha Magufuli kisha angeweka mtandao wake sawa 2025 angeanza rasmi kipindi chake cha awamu ya sita 2025-2035.

Waliomshauri aseme ni awamu ya sita walimuingiza chaka, angetumia ile mbinu ya Piere Nkurunziza.
 
Kwani si anamalizia awamu ya 5 halafu agombee awamu yake ya sita yenye miaka 10 jumla 14
 
Miaka 10 itamtosha.Hivi hii mambo ya kufufua viwanda vilivyokufa,,unaweza fufua kiwanda chenye outdated tech?

Hapo ni kuleta wawekezaji wapya hakuna kitu kama kufufua viwanda.
 
Kwani si anamalizia awamu ya 5 halafu agombee awamu yake ya sita yenye miaka 10 jumla 14
Ha ha ha alijichanganya akajiita yeye ni awamu ya 6. Ilibidi aseme namalizia hii miaka 4 ya awamu ya marehemu kisha naanza yangu.
 
Wasomi, wanazuoni, wanasheria naomba tujadili kama ni sahihi kwa mujibu wa katiba yetu kumuita Rais Samia kama rais wa awamu ya sita badala ya kuitwa rais wa pili wa awamu ya tano?

1. Katika Uchaguzi mkuu uliofanyika 2020 Vyama vilinadi ilani zao ili kuchaguliwa kuongoza nchi na ilani ya CCM ndiyo inayotekelezwa na ni makubaliano baina ya wananchi na serikali ya chama tawala na hiyo ilani ndiyo inatekelezwa na mama Samia.

2. Je, katiba inapotamka makamu wa rais kushika wadhifa wa urais inapotokea rais aliyechaguliwa kufariki haikuwa na lengo la kuhakikisha kila awamu inakamilka na ahadi za wananchi zinatekelezwa?

3. Kama serikali hii ni sawa kuiita serikali ya awamu ya sita je inatekeleza ilani ipi? Na hayo wanayotekeleza kama ni mapya ridhaa hiyo inatoka wapi wakati hakuna uchaguzi uliofanyika?
 
Ni vema tukihesabu Marais. Hivyo Samia ni Rais wa sita wa nchi hii. Hii ya kuhesabu awamu ni kujichanganya bure.

Kama tukitaka kuhesabu awamu basi tuanze na tafsiri rasmi ya awamu. Awamu ni nini?
 
Back
Top Bottom