Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

Leo wakati anamwapisha Makamu wa Rais Dr. Philip Mpango na kutangaza Baraza lake jipya la Mawaziri, Mh Rais amesema; Hii ni AWAMU YA SITA na tunataka kuanza upya. Mliokuwa mnauliza hii ni awamu ya ngapi mmepata jibu.
 
Nimemsikia hata mimi,ila inatafakarisha kweli kweli.Maana awamu ni miaka mitano,na Rais wa kina awamu huwa anachaguliwa kwa sanduku la kura.Mimi nilidhani huyu ni Rais wa sita,ila awamu ni ya tano!Labda tungepata ufafanuzi wa kisheria kutoka kwenye vyombo vyetu vya sheria,maana nilisikia mwanasheria mmoja aliyekuwa amealikwa TBC akisema hii ni awamu ya tano.
Mkuu uko sawa huyu ni raisi wa awamu ya 5, kwani lini tumefanya uchaguzi mpya wa hiyo awamu ya 6 ?angesema tu mimi ni raisi wa 6 kwenye awamu ya 5, nilipiga kura uchaguzi wa awamu ya 5 ya sita bado hadi uchaguzi ujao. mara hii tumeanza kujikana!
 
Kuna namna mbili za kuwa raisi Tanzania kulingana na katiba. Si uchaguzi tu. Mbona mambo madogo tu haya hayaitaji akili kubwa. Awamu inahesabiwa kwa raisi si miaka. Nyerere alitawala awamu ngapi kama awamu ni miaka? Kwann tupo awamu ya tano?
 
MH Rais amekosea..yeye ni Rais wa 6 katika awamu ya Tano..kila awamu inakuwa na vipindi viwili...akigombea mwaka 2025 atakuwa Rais wa 6 katika awamu ya 6 ..mwaka 2030 itakuwa Serikali ya awamu ya Sita Rais wa Saba ..hivyo hivyo kadri itakavyoenda
 
Mfano Marekani Biden ni Rais wa 48 katika awamu ya 47 nadhani..so huwa iko hivyo
 
Awamu moja ni miaka mitano, sasa yy atarun kwa miaka mitano?
Mkuu awamu sio miaka Ila awamu ni viongozi,huyu ws Sasa ni rais wa sits ,hivyo awamu ya Kwanza au rais wa Kwanza ni Mwl Nyerere,awamu ya pili au rais wa pili ni mzee Mwinyi,awamu ya tatu au rais wa tatu ni hayati Mkapa......
Mpaka unampata mama Samia,ni rais wa sits au awamu ya sits.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hii ni Serikali ya awamu ya 6 hivyo atakayeshindwa kasi yake ataachwa njiani.

Namshukuru sana Rais Samia kwa kuliweka sawa hili kwani jana watu wengi walinibishia nilipowaambia mimi naamini hii ni awamu ya 6.

Kila zama na kitabu chake.

Maendeleo hayana vyama!

Sawa mkuu ,tushapata precedent maana tukio lililotupata tar 17.03.2021 ni geni mkuu.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hii ni Serikali ya awamu ya 6 hivyo atakayeshindwa kasi yake ataachwa njiani.

Namshukuru sana Rais Samia kwa kuliweka sawa hili kwani jana watu wengi walinibishia nilipowaambia mimi naamini hii ni awamu ya 6.

Kila zama na kitabu chake.

Maendeleo hayana vyama!
Umemuamini ?
 
Back
Top Bottom