Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hussein Mwinyi kuwa wageni Rasmi Kongamano la Viongozi wa Dini nchini

Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hussein Mwinyi kuwa wageni Rasmi Kongamano la Viongozi wa Dini nchini

Kongamano hilo kubwa la Viongozi wa Dini litafanyika Aprili 18, 2021 katika Ukumbi wa Chimwaga Dodoma.

Mheshimiwa Rais wa Tanzania Mama Samia pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi watahudhuria wakiwa wageni rasmi


Picha ya 'Public Enemy' hapo juu katika Tangazo hili ni ya nini? Kwanini mnampenda Kujipendekeza ( Kujikomba ) Kwake wakati ameshakuwa Historia na wengine tumeshaanza hata Kumsahau Akilini mwetu? Mmeboa!!
 
Kongamano hilo kubwa la Viongozi wa Dini litafanyika Aprili 18, 2021 katika Ukumbi wa Chimwaga Dodoma.

Mheshimiwa Rais wa Tanzania Mama Samia pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi watahudhuria wakiwa wageni rasmi

Sasa hiyo picha ya Magufuli Ni ya nini hapo wakati anaendelea kutumikia adhabu yake huko aliko
 
tushajua yanayoenda kutendeka....

1. kumsifia jiwe
2.kumsifia samia

3. kuomba amani,haki haita tajwa


Nonsense kabisa.
 
Imani ziko tofauti. Sisi wakristo hatuamini kuwa mtu anaweza kumuombea mtu mwingine msamaha, kila nafsi itaomba msamaha peke yake. Kama hakuomba alipokuwa na pumzi, ndio imetoka.
Usijumuishe wakristo wote, ainisha dhehu lako. Cc wakatoliki huwa tunawaombea marehemu. Ila kama marehemu alikuwa na dhambi ya mauti eg kuuwa, kudhulumu watu fedha yao kama bureau de change, wafanya biashara, kuiba kura na mabaya mengine, hawezi kunufaika na maombi hayo. Badala yake Mungu huwarehemu wengine waliokuwa na dhambi ndogondogo
 
Kongamano linakwenda kujadili nini?
Ni kongamano la kumuombea Magufuli huko alipo na kutoa nafasi kwa Mama kuwasamahe mashehe wa uhamsho ndio sababu ya Rais Husein Mwinyi nae kualikwa.
 
Wangeitoa hiyo picha ya Mwendazake sababu siku 21 za maombolezo zilishapita
 
Jambo jema inatupasa kama Taifa kuendelea kwa umoja wetu kumuweka Mungu wa Mbinguni kwanza na kumtegemea. Kumshukuru Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi na vyote vivijazanyo vinavyo onekana na visivyo onekana.

Zaburi 106:1 na 118:1(Agano la Kale) Maneno haya ya Mungu yanafanana Neno kwa Neno, Nukta kwa Nukta.
Yanasema hivi:
"Haleluya Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema. Kwa maana fadhili zake ni za milele."

Nani atabisha kwamba fadhili za Mungu ni za milele katika Taifa la Tanzania?

1Thessalonike 5:17-18(Agano Jipya)
Maneno ya Mungu yanasema hivi:

"Ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya mwenyezi Mungu kwenu latika Kristo Yesu."

Kiongozi yeyote wa kisiasa na kiserikali mwenye hikma atawaleta karibu na yeye viongozi wa dini maana wanamsaidia kuongoza nyoyo za watu anaowatawala kumuelekea Mungu na kufanya matendo mema.
 
Back
Top Bottom