Rais Samia Suluhu kuhutubia Bunge Alhamisi Aprili 22, 2021

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Rais Samia Suluhu Hassan atalihutubia Bunge Alhamisi Aprili 22 2021 jioni

Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa Mama Samia kulihutubia Bunge tangu alipoapishwa kuwa Rais Machi 19 mwaka huu.

===

Rais Samia Suluhu Hassan atahutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 22, 2021.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amelitangazia Bunge leo Jumatatu Aprili 19, 2021 kuwa Rais Samia atalihutubia Bunge Alhamisi ya wiki hii kuanzia saa 10 jioni.

Hivyo, Spika Ndugai amewaagiza wabunge wote walioko nje ya Jiji la Dodoma kurudi na wale wanaotaka kuondoka wazingatie kuwapo kwa shughuli hiyo kwanza.

Rais Samia atalihutubia Bunge kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kuwa Rais Machi 19, 2021 baada ya kifo cha Rais wa tano, John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.

UPDATES:
Leo Alhamisi Aprili 22, 2021 kuanzia saa 10 jioni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atalihutubia Bunge kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi Machi 19, 2021.

Kwa mujibu wa ratiba ya Bunge iliyotolewa leo inaonyesha kuwa hotuba ya Rais itaanza saa 10:10 jioni lakini asubuhi kuanzia saa 3:00 hadi saa 5:00 kutakuwa na kikao cha kawaida cha Bunge.

Saa 5 asubuhi hadi saa 8 mchana ndani ya ukumbi wa Bunge kutakuwa na shughuli za kiutawala zitakazosimamiwa na katibu wa Bunge au mkuu wa itifaki bungeni na kuanzia saa 8 mchana hadi saa 9 alasiri utakuwa ni muda wa wabunge na wageni waalikwa kuingia ukumbini na maeneo maalum ya wageni.

Saa 9:15 hadi saa 9:50 alasiri utakuwa ni muda wa viongozi mashuhuri kuingia bungeni ambao ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais – Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Saa 9:55 alasiri Spika wa Bunge, Job Ndugai ataingia ndani ya ukumbi wa Bunge na mara watakapowasili wimbo wa Taifa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaimbwa kisha Spika atatoa maelezo kwa dakika tano hadi saa 10:10 jioni.

Baada ya hapo Rais Samia atatoa hutuba yake kwa muda ambao haujatajwa na akimaliza mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba atatoa neno la shukrani kwa niaba ya Bunge kisha Spika atafanya utambulisho wa viongozi na wageni waalikwa.

Baada ya hatua hiyo Ndugai na Samia watatoka ndani ya ukumbi wa Bunge na kuelekea kwenye chumba maalum wakifuatiwa na viongozi mashuhuri kisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atatoka ukumbini kuelekea eneo la picha kisha wabunge nao watafuata kuelekea eneo hilo.
 
Ni wakati Sabufa ajiuzulu Ile Jimbo lake nalo lipate mbunge mchapakazi. Wakati jpm anaendeleza kwao kwa kupeleka hospital, benki, veta, mbuga za wanyama, kiwanja Cha ndege, mataa ya barabarani, shule, mwalo, soko, hoteli ya nyota tatu nk.

Huyu Sabufa ambae nae Ni mkuu wa mhimili hajapeleka hata kisim Cha maji, shule zinahali mbaya sana isitoshe hata hela zilizopelekwa kwenye halmashauri ya kwao zimeota mbawa(ripoti ya CAG) msimamiaji wa hizo hela Ni mtu wa karibu sana na Sabufa.
 
Ni wakati Sabufa ajiuzulu Ile Jimboa lake nalo lipate mbunge mchapakazi. Wakati jpm anaendeleza kwao kwa kupeleka hospital, benki, veta, mbuga za wanyama, kiwanja Cha ndege, mataa ya barabarani, shule, mwalo, soko, hoteli ya nyota tatu nk. Huyu Sabufa ambae nae Ni mkuu wa mhimili hajapeleka hata kisim Cha maji, shule zinahali mbaya sana isitoshe hata hela zilizopelekwa kwenye halmashauri ya kwao zimeota mbawa(ripoti ya CAG) msimamiaji wa hizo hela Ni mtu wa karibu sana na Sabufa.
Ndugai hawezi kujiuzulu.. labda asaidiwe kwa kutumbuliwa
 
Ni wakati Sabufa ajiuzulu Ile Jimboa lake nalo lipate mbunge mchapakazi. Wakati jpm anaendeleza kwao kwa kupeleka hospital, benki, veta, mbuga za wanyama, kiwanja Cha ndege, mataa ya barabarani, shule, mwalo, soko, hoteli ya nyota tatu nk. Huyu Sabufa ambae nae Ni mkuu wa mhimili hajapeleka hata kisim Cha maji, shule zinahali mbaya sana isitoshe hata hela zilizopelekwa kwenye halmashauri ya kwao zimeota mbawa(ripoti ya CAG) msimamiaji wa hizo hela Ni mtu wa karibu sana na Sabufa.
Kapeleka jina lake kwenye Soko la Ndugai
 
Back
Top Bottom