Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

Chato haina hadhi ya kua mkoa hata miaka 20 ijayo.

Vitu vya ajabu kabisa ,watu wanataka kugeuza pori la mkoa wa geita liwe mkoa.

Angalau morogoro unaweza kufkiria kuigawanya ukapata mkoa mwngne kwa ilipo fika sasa na jinsi mkoa ulivyo mkubwa.
 
Hiyo haitoshi kumuenzi jiwe wetu. Awekwe kwenye fedha yetu kama alivyo Nyerere
nahisi pesa zitajielekeza kwenye ujenzi, yani ukiipata utashaangaa unawaza ujenzi ujenzi, mwishowe tutakufa maana hatutawaza kujitibia, kujivalisha vizuri, kujinunulia chakula
 
Tabora kuna idadi ya watu wangapi
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, idadi ya watu (na eneo la mkoa kwa km za mraba); Tabora: 2,291,623 (76,150), Morogoro: 2,218,492 (70,624)

Makadirio ya watu mwaka 2019: Tabora - 2,974,400; Morogoro - 2,662,500
 
Hii ni kwa watu wa kanda ya Ziwa

Piganeni usiku na Mchana. Orodhesheni vigezo vyote ili Chato iwe Mkoa.

Faida za Chato kuwa mkoa ni nyingi Sana kulingana na miundo mbinu iliyo nayo hususani.
1. Mbuga za Wanyama.
2. Poli la Misitu.
3. Ziwa victoria.
4. Airport.
5. Jicho la Serikali.
6. Hospital ya Kanda
Hiyo miundo mbinu inahitaji usimamizi wa karibu na makini ili ilete faida ya karibu kea wananchi wote. Hii ni nafasi kwa watu wa kanda ya Ziwa kuinua uchumi wao na Hari zao za kiuchumi. Msiache kupambania hii kitu.

Acheni Geita iendelee kuchimba Madini. Bukoba Ndizi na kahawa. Kigoma mawese.

Ila uwepo wa Chato utainua sana Hari ya watu wa Kanda ya Ziwa.
 
Mikoa ya...
Tabora ina ukubwa wa eneo la mraba ............ 76,151km2
Rukwa ina ukubwa wa eneo la mraba...............75,250km2
Morogoro ina ukubwa wa eneo la mraba .......73,139km2
Lindi ina ukubwa wa eneo la mraba ..................67,000km2
Ruvuma ina ukubwa wa eneo la mraba ............66,477km2

GEITA INA UKUBWA WA ENEO LA MRABA 19,595KM2

Humo tutapata mkoa wa Chato!!!


Nini maoni yako
 
Umewahi kujua ukubwa wa mkoa wa Daresalaam pia??

Kwa nini haukuunganishwa tu na mkoa wa Pwani Ikiwa ni mkoa mmoja??

Unadhani kigezo ni ukubwa wa eneo pekee??

Kwa mfano, Morogoro ni Kweli ni kubwa Sana, lakini huwenda eneo linalokaliwa na watu linaweza kuwa ni dogo kuliko lile linalokaliwa na wanyama pamoja na sehemu kubwa ya milima na mabonde ya mipunga,

Kwa hiyo inakuwa ni shida kuumegamega mkoa wa Morogoro
 
Compare population ya Dar na Geita, na ukiweka Population ya Chato kwa raha zaidi!
Sasa basi hoja yako isiwe ni ukubwa wa kieneo pekee, Bali iko namna inayosababisha mkoa uundwe, ni Kweli ni pamoja na papulation ya watu, kimapato pia, kijiografia na vigezo vingivingi, lkn pia wakati mwingine na nguzu za kisiasa na upendeleo tu
 
Sasa basi hoja yako isiwe ni ukubwa wa kieneo pekee, Bali iko namna inayosababisha mkoa uundwe, ni Kweli ni pamoja na papulation ya watu, kimapato pia, kijiografia na vigezo vingivingi, lkn pia wakati mwingine na nguzu za kisiasa na upendeleo tu
Kwa hoja yako basi, Kilimanjaro ilitakiwa kuwa mikoa mitatu hivi!
 
Sasa basi hoja yako isiwe ni ukubwa wa kieneo pekee, Bali iko namna inayosababisha mkoa uundwe, ni Kweli ni pamoja na papulation ya watu, kimapato pia, kijiografia na vigezo vingivingi, lkn pia wakati mwingine na nguzu za kisiasa na upendeleo tu

Hivi katika yote uliyo orodhesha kuna kigezo hata kimoja kinacho kidhi uundwaji wa MKOA wa sijui Chato/Robondo - hakipo kabisa.

Sijui kwa nini watu wanaendelea kupoteza Mega Calories kuzungumzia mambo ya kulazimishana uundwaji wa Mkoa ambao hauna kigezo wala ulazima wa kuanzishwa in the first place - kama kigezo ni kutaka kumkumbuka/muenzi Magufuli, basi Mkoa wa Geita upewe jina la Magufuli au Chato nk. Mbona Mkoa wa Ziwa magharibi ulibadirishwa jina na kujulikana kama Mkoa wa Kagera.
 
Back
Top Bottom