Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

upuuzi tupu, na jiwe angesha ugawa huu mkoa, tunataka umoja wa afrika huku sisi tukiendelea kugawana kidogo kilichopo badala ya kuungana.
Kifikra bado sana kwa sasa kuwa na umoja wa Africa, kuongeza mkoa ni kuleta serikali karibu zaidi na wananchi
 
Walilewa madaraka hawa...Chato!
Badala ya kufikiria kugawa mkoa kama Moro,Tabora nk ...ukagawe Geita...very primitive argumentation...alichowafanyia vinawatosha!
Mkoa wa Geita na Tabora ni upi una idadi kubwa ya watu na nguvu ya kiuchumi ? Jibu ni rahisi Geitaaaa
 
Serikali ikiamua kupandisha hadhi huwezi kuzuia huku jf. Acha tu pawe mkoa kwani inakuuma nini.
Kuna watu kufuata miundo mbinu na miundo mbinu kufuata watu. Ukitaka kuthibitisha hilo katika sehemu ulipo linganisha gharama ya eneo lililoko karibu na huduma za kijamii kama barabara,soko, shule, hospitali, n.k na eneo lililombali na huduma kama hizo
Hupo sahihi sana. Leo hii hata ukiweka barabara za lami mitaa yote ya Chato na shule nzuri za msingi, bado hakuna atakayehama toka Dar, Mwanza au Arusha, akaishi Chato eti kwa sababu kuna barabara nzuri. Isipokuwa mjini Dar au Mwanza, au Arusha, kukiwa na eneo lenye miundombinu mizuri, ni kweli hilo eneo litavutia watu wengi kuishi.

Chato, pamoja na uwanja wa ndege wa kimataifa, hakuna atakayeenda huko.

Mimi siumizwi na eneo lolote kuwa mkoa au wilaya bali naumizwa na ujinga wa viongozi wetu kushindwa kuelewa mambo yaliyo muhimu kwa ustawi wa watu na Taifa letu.

Tunaweza kuwa na mikoa hata 200, lakini tukabaki tunakokotwa na nchi zenye mikoa 9. Eneo fulani kulilia liwe mkoa ni upuuzi na upungufu wa uelewa. Mikoa tuliyokuwa nayo miaka yote ilikuwa inatosha. Kilichokuwa kinahitajika ni kusogeza huduma za kiserikali kwenye maeneo ya watu, na ofisi za chini kuziongezea uwezo na maarifa. Yaani mtu akienda kituo kidogo cha polisi, huduma atakayopata iwe sawa na akienda ofisi ya polisi ya wilaya. Mtu akienda hospitali ya wilaya, hudima iwe kama hospitali ya rufaa, imtu akienda ofisi ya afisa kilimo wa kata awakute wataalam wenye uwezo na taaluma zote, n.k.
 
Toa takwimu zako halali na unishawishi. Uchumi wa Tanzania utajengwa na watanzania wote siyo serikali tu.
Sasa hiyo tarafa ya Chato ina uchumi gani zaidi ya matumizi mabaya ya fedha za Watanzania Shs 2.4 zilizoibiwa na Mwendazake
 
Back
Top Bottom