Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

sasa ubaya utakua wapi kama wakielekezwa ikawapa vigezo
Unaifahanu Chato? Ni Wilaya ndogo, ipo mkoa wa Geita, Geita nayo ilikuwa sehemu ya mkoa wa mwanza Kisha awamu ya Kikwete ndio ikagawanywa

Kugawa sio mbaya, lakini je, hakuna mikoa yenye uhitaji mkubwa zaidi ya Chato?

Mkoa wa Morogoro unaufahamu ukubwa wake?
 
Kajibu hivi

'Suala la Chato kuwa Mkoa nimeambiwa tayari mchakato umeanza naelekeza lishughulikiwe kama vigezo vimekidhi Chato iwe Mkoa na kama vigezo havijakidhi tuwaelekeze nini cha kufanya ili viweze kukidhi na tumuenzi Hayati Magufuli.'


Ni jibu zuri sana sana na nijibu la kiuongozi na sio jibu la kukurupuka.
Ingekuwa mwamba angeshakurupuka hapo hapo kua kuanzia sasa nasema huu ni mkoa, asante mama unaanza vzr.
 
Kumekuwa na tetesi za muda mrefu tangu Mh. Magufuli aingie madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2015 kwamba alikuwa na mpango kabambe wa kuifanya wilaya ya Chato kuwa mkoa.

Habari hiyo imekuwa ikikanushwa kwa hisia kali na wafuasi wa CCM ndani ya JF kuonesha kwamba wanaosema hivyo ni wazushi na wana nia mbaya ya kuonesha labda MH. Magufuli alikuwa anajipendelea ukizingatia udogo wa mji na uchanga wa wilaya ya Chato.

Lakini mtu aliyeandaliwa kuwasilisha salaam za Wanachato siku ya mazishe, Mzee maarufu pale Chato aitwaye Magambo ameweka wazi kwamba marehemu katika uhai wake aliwaahidi kuigeuza Chato kuwa mkoa kabla ya 2025.

Akijibu hoja hiyo Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kulifanyia kazi kama litakidhi vigezo vilivyowekwa. Lakini facial expression yake imeonesha mshitumko juu ya jambo hili kwa kuliona kama jipya. Baadhi ya maneno aliyotumia ni "Nasikia mmeshaanza mchakato".

Jambo jema Kama hili la kuliongezea thamani eneo mojawapo katika nchi hii halikupaswa kuwa siri hata kwa watu muhimu na wawezeshaji. Tulifichwa mchakato huu ili iweje? Yaani walitegemea siku moja tuamke na kukuta Chato ni mkoa ghafla?

Tabia hii ya kuweka siri vitu vinavyopaswa kuwa wazi haileti Afya kwa Utangamano wa nchi yetu. Mh. Samia asikubali kuendelea na utaratibu wa usiri usio wa lazima unaiweza kuibua fikra za upendeleo.
 
Back
Top Bottom