Rais Samia Suluhu pamoja na taasisi zako za haki: Tafadhali, waache Chadema wafanye maandamano yao. Wape ulinzi, kwani wewe ni kiongozi wa wote

Rais Samia Suluhu pamoja na taasisi zako za haki: Tafadhali, waache Chadema wafanye maandamano yao. Wape ulinzi, kwani wewe ni kiongozi wa wote

S.M.P2503

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2008
Posts
2,421
Reaction score
4,344
Nakuita kwa jina la Jamhuri ya Muungano wetu mheshimiwa Raisi.

Waache hawa Chadema na Wananchi wengine waandamane.

-Wape ulinzi,
-Hakuna kitakacho haribika
-utaithibitishia dunia kuhusu zile 4R
-utapunguza malumbano ya kulilia haki.

Baada ya Maandamano:

Baaada ya Maandamano, utajitokeza na kuzijibu hoza zao na kutoa suluhisho la namna ya kusonga mbele.
Uta- prove leadership skills zako kwamba sio za mabavu
Utapendwa zaidi na wapinzani wako na supporters zako kwa pamoja.

Kama nchi:
-Tutaendelea kujadiliana mambo yetu kama mchwa na nguchiro bila wanaoishi ndani ya kichuguu bila mkwaruzo.
-mambo yetu ya nchi yataendelea bila mkwamo.

kwa wateule wako:
-Toa mfano kwa kwao kuachia nafasi ili liwe funzo kwa wengine wajao , hata kama haitakupendeza.

Nchi yetu imekuwa na kelele nyingi sana kwa sasa za kutaka haki sana kwa sasa. Na wewe kama kiongozi wetu, onyesha leadership ya haki inayoliliwa na wanao sema hawana haki maana wewe ni kiongozi wa wote bila kujali vyama vyao.

Mungu wetu ni Kiongozi wa sisi sote bila kujali madhambi yetu.

Povu kwa yeyote ruksa, muda wa suluhuhisho bado upo, tusisubiri hadi mambo kuharibika ndio tuongee.
 
Wazo zuri ila binafsi nilimhusudu sana Samia alipochukua mamlaka kamili baada ya Magu,alipobironga mwanzoni nikamsamehe due to lack of experience, ila sasa noooo...to hell, akosee weee ili dunia imwone uchi!
 
Ana muda bado hadi kesho- Nchi yetu tunaipenda sana hata kwa tofauti zetu. Ni numba yetu, tumo watoto tofauti tofauti. Mama na baba na watusikie watoto tunasemaje pia
 
Tatizo ni kwamba Rais Samia anaburuzwa na hawa wanaomdanganya na kumtisha. Hawa wasiotumia akili bali maguvu wamekuwa ndio viongozi wakuu wa Rais, wanampeleka kokote wanakotaka, naye anawasikiliza na kuwatii!!
 
Ana muda bado hadi kesho- Nchi yetu tunaipenda sana hata kwa tofauti zetu. Ni nyumba yetu sote, tumo watoto tofauti tofauti. Mama na baba na watusikie watoto tunasemaje pia
 
Wazo zuri ila sasa wapambe ndio wanamharibia Mama Rais kwa kumjazo uongo. Akiendelea kuwasikiliza wanaenda kumharibia kabisa ndani na nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom