#COVID19 Rais Samia Suluhu: Tutalichukulia kwa uzito suala la COVID-19

#COVID19 Rais Samia Suluhu: Tutalichukulia kwa uzito suala la COVID-19

Katika eneo la kazini kwangu kawaida kwa mwaka ni nadra kutokea kifo Cha mzazi wa mfanyakazi mwenzetu, na ikitokea huwa ni kimoja viwili.

Toka January Hadi mwezi huu tumezika tayari wazazi 18 wa wenzetu.
Unadhani hii ni coincidence?

Kima we
 
Hakika huyo anayemshauri Mh. Rais Samia Suluhu kwamba Tanzania kuna corona anampotosha!

Kwa nchi ilipofikia huko tumevuka na tumepita, mabeberu walituaminisha tutakufa na kuokota maiti barabarani lakini hii haikutokea
Wameenda mbali zaidi kututisha kwa second version ya corona ni tishio lakini Waswahili tunaendelea na maisha yetu kama kawaida.


Tanzania hii haina corona, rais tuwache tuendelee na maisha tuliyozoea kwani naziona dalili za kuzuia mikusanyiko na lockdown
Wafuasi wa Jiwe hamuamini macho yenu. Jiwe limeondoka na jalirudi tena. Na Sera za ubabe wa kupereka maabara kuu ya taifa kware, makondoo, mipapai na mimbuzi kama vipimo havipo tena.

Na kama hamridhiki nendeni mkamuombe ainuke. Aone kuwa watu sasa wanaongozwa kwa kufuata sheria , na si matamko.

Odhis *
 
Nakumbusha tuu kuwa "Mwendazake" naye alishauriwa na kamati flani.Ndiyo ilipelekea kutoa maamuzi yake yaliyoifikisha nchi hapa tulipo.

Pendekezo la kwanza :ili kupata ushauri mpya wenye mantiki, kamati ya mara hii itakayoundwa na Mhsehimiwa Raisi iwe na akili nyingine mpya(huwezi solve tatizo lilelile uliloshindwa kwa kutumia akili ile ile).Yaani wasiwepo wale wajumbe waliotoa ushauri mara ya kwanza(Ninaamini miongoni mwao ni Mganga mkuu wa serikali,PS health,waziri wa afya,naibu waziri wa afya).Kwa sababu hawataweza kuji-contradict wenyewe.

Kama ni watu wenye ushawishi wanaweza sababisha kamati isije na jambo jipya.Tupate watu ambao ni profesional, huru,objective bila kuangalia maslahi yao binafsi.Pia tuwaepuke wale waliokwisha onyeshaga msimamo yao hadharani kuhusu namna ya kupambana na covid 19 hapo kabla,eitha kwa manufaa yao ya kisiasa au ki-popularity wanaweza kutupotosha pia.

Angalizo la pili ni kwamba,kamati inaweza kununuliwa na wakubwa wenye maslahi ya kunufaika na covid 19 pandemic.Hivyo nashauri wanakamati wafanyiwe veting ya kutosha kwa sababu ya umuhimu na uzito wa mapendekezo tarajiwa.

Asanteni kama kuna mwenye nyongeza anaweza kutuwekea pia
 
Wataalamu wenyewe si ndio akina Kigwa magangala? ambao leo wanashika microscope kesho wanashika tunguli?
aliekwambia kuwa kigwa ndio ata lead hiyo team ni nani?
viko vichwa kutoka kwenye sekta ya afya. yako majembe mengine yamesomeshwa nje, wamefanya kazi nje.
wataunda team bora tu.

kigwa ni light headed. si mtaalam ni mwana siasa
 
Hata malaria imetuchukulia ndugu wengi tu.
speed ya maambukizi ni kubwa kuliko malaria.
malaria ugonjwa umekuwepo toka enzi za mitume. yes lazima uchukue watu wengi over the years.

corona ni ya juzi tu. lakin check speed yake ya kuondoka na watu.. inavyo spread fast + its a virus. malaria si virus
 
Rais Samia kuunda kamati kushughulikia COVID 19. Amesema ataunda kamati ya kushughulikia kitaalamu.

Amesema hatuwezi kujitenga kama kisiwa, lazima tuunde kamati ijulikane kama tunakubali au tunakaa na si kusikia habari tu za nchi nyingine na ikifika kwa Tanzania hamna kitu.




Rais Samia amesema haya

''Tutaunda Kamati ya Wataalamu kuhusu Covid 19 watuambie kitaalamu hayo yanayopendekezwa na Ulimwengu kuja kwetu yapoje, hatuwezi kujitenga tu kama Kisiwa na hatuwezi kupokea yanayoletwa bila kuweka cha kwetu, bila kufanya utafiti wa kwetu.

Rais Kikwete alituambia akili za kuambiwa changanya na zako, tuweke na zetu tuwe na msimamo maalum unaoeleweka, sio tunasoma tu mambo ya Covid 19 Ulimwenguni, Tanzania deshi deshi deshi haieleweki, tueleweke kama tunakubali au tunakataa

Suala la Covid 19 nafikikiria niunde Kamati ya Wataalamu waliangalie kwa upana wake kitaalamu halafu watushauri Serikali, halifai kulinyamazia aidha kulikataa au kulikubali bila kufanya Tafiti za kitaalamu''



Kamati inaweza kuwa daraja tu lakini maamuzi tayari yapo?Ngoja tusubiri,time will tell.
 
Nakuhakikishia kuwa baada ya muda mfupi sana ataanza kuikana nyungu!😁
Sasa hivi hata ccm wanamkana mwendazake na matendo yake yote, kila mtu amekuja na mbinu mpya ya kuonyesha umma kwamba walikua wanashangazwa na matendo ya mwenda zake soon polepole ataitisha press conference kuiomba msamaha corona
 
Leo nimethibitisha kwa rasilimali CCM walizo nazo wana uwezo wa kushikilia dola miaka mingine 100 ijayo.

Hongera sana rais wetu Samia Suluhu Hassan🔥🔥🔥🔥 Unaweza sana mama.

Mwendazake huko aliko kama anayaona haya au kuyasikia haya atakuwa anasema hiiiiii!

Ila mwendazake alituingiza chaka wandugu.

Hiiiiii!
 
Hivi Tanzania haikuwa na ushauri wa kitaalamu na JPM marehemu maamuzi ya corona na hatua alizochukua hakuzingatia ushauri wa wataalamu?

Fitina za aina hii kwa marehemu na utafutaji uungwaji mkono kwa njia hii hazitamsaidia mtu.

Je, anataka Watanzania wa amini suala la corona halikuchukuliwa kwa uzito? Ama ndio njia ya mzunguko kwenda kukubaliana na chanjo za WHO na wajasiriakorona.
Siyo fitina mkuu. Corona ipo nailifika ikulu. Balozi Kijazi alikufa corona na ilitangazwa kabisa.
 
Mwendazake huko aliko kama anayaona haya au kuyasikia haya atakuwa anasema hiiiiii!

Ila mwendazake alituingiza chaka wandugu.

Hiiiiii!
Tena chaka kubwa sana. Ni kama hadithi ya yule mfalme aliyekuwa uchi hakuna mtu aliweza kumwambia mpaka mtoto mdogo ndiye alisema mfalme yuko uchi!
 
Shalom "Bwana Mungu akasema nami juu ya ujio wa chanjo ya Corona kwa kasi sana barani Africa ikiwemo Tanzania ingawa baadhi ya nchi za Africa zinaendelea na udungaji wa chanjo hizo pia Bwana akanionyesha Contena saba ziko kwenye kama behewa kubwa ila ndani ya maji na ndani yake kuna sindano kama ndogo ndogo hivi nyingi na gloves nyingi na madwa mengi kisha Bwana akanionyesha watu wengi humo ndani ya behewa wazungu na watu weusi wengi lakini cha ajabu watu hawa walikuwa wakisheherekea hivi wengine wakisema tumeshinda na haya ni maono ya wazi wazi kisha Bwana akaniambia niwaambie watanzania wenzangu niwaambie watumishi wa Mungu wote tuombe sana juu ya taifa letu ila rehema na toba ya ndani kwa kanisa lote na taifa,Tuziombee familia zetu na tuwaombee bila kuchoka viongozi wa taifa letu la Tanzania maana Lucifer ameandaa uharibifu mkubwa kupitia wakala zake ambao ni baadhi ya watu katikati ya wanadamu Mungu atupe kutii amen.
 
Back
Top Bottom